Ukishuka Nakumeza

Given Edward

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
850
Reaction score
203
Katika shule fulani ya kishua ya ghorofa 5 hivi ilitokea katika darasa la juu kabisa mwalimu alimtuma mwanafunzi mmoja akamchukulie chaki chini kwenye ground floor. Hasa wakati amebakisha ngazi nne kufika chini ile anataka kukunja tu anasikia sauti inasema "UKISHUKA NAKUMEZA". Jamaa kila akijikaza kwenda sauti ndio inazidi "UKISHUKA NAKUMEZA".
Mwisho wa siku akamfuata mwalimu na kumwambia kuna mtu anataka kummeza. Wakabebana na mwalimu wake hadi ile sehemu."MKISHUKA NAWAMEZA". Mwalimu akajiuliza amejuaje tuka wawili bila kutuangalia? Mwalimu woga ukamjaa balaa kwa vile shule imeingiliwa na jambazi linaloua watu. Akapiga simu polisi na baada ya dk 15 polisi wakaja na FFU ndani wakiwa wamechafuka bunduki na risasi. Wakapanda mpaka ile sehemu wakajipa ujasiri wakatokea mbele ya yule jamaa na mibunduki yao.
Cha ajabu wakakuta kumbe ni chizi anaongea na makamasi yake. Pale mara ya kwanza lilikuwa kutoka tundu moja hivyo akawa anasema "UKISHUKA NAKUMEZA" halafu baadaye wakati na mwalimu anakuja ikawa matundu yote mawili ndo akawa anasema "MKISHUKA NAWAMEZA".
 
hahahahayeeee ahh makubwaaanwga haya, madogo yana nafuu. Na huyo alikuwa chizi kweli kwasababu hayapi hata sapoti ya kuyasukuma yatoke ila anayasubiria. Dah lkn mwalimu alionekana kuwa ni zaidi ya chizi kwa uoga wake....
 
hahahahayeeee ahh makubwaaanwga haya, madogo yana nafuu. Na huyo alikuwa chizi kweli kwasababu hayapi hata sapoti ya kuyasukuma yatoke ila anayasubiria. Dah lkn mwalimu alionekana kuwa ni zaidi ya chizi kwa uoga wake....
haaa,haaaa, uuuuwiiiii......ticha anaogopa lisije lika m-swalo.
 
Dah nimecheka xa imalizie kuwa wale polis walikuwaje wadogo ka pilton.
 
Machizi wanaingiaje shule za kishua wakati 24 mlinzi getini.
 
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa u made ma day
 
ha ha ha ha......hii nimekubali....sekyuuu..Police walijilaumia....ila nao ili wasionekana machizi watambeba chizi..
 
Uuwiiiiiiiiiiiiiii...mbavu zangu zitamezwa....mjini shule!
 
dah afadhali imekuwa hivi...............nilichelea isiwe makubwa zaidi!
 
Walienda na mabunduki chungu nzima sijui walizani ni maandamano ya chadema? Hah hah ,shame on'em.!
 
Haaaa haaaa haaaaa haaa,uwiiii mbavu zangu mie lol!
 
Kidogo n'tapike makamasi ya huyu chizi !!!! Si unajua tena makamasi mazito ya rangi ya njano hivi au kama anavuta sigara yanakua na partical nyeusi maziiitooo halafu yana chumvi chumvi ukiyala.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…