Ukishangaa ya Uamsho, haya utasemaje?

Hoja mfu ni ipi? wewe hujisalimishi kwa muumba wako?
.........mmmh! hapa mkuu ungekuwa wazi kidogo unamzungumzia muumba yupi? maana kuna muumba yule aliyemuumba kwanza Adamu na Hawa halafu kuna yule muumba mwingine aliyeumba kalamu. Sijui unamzungumzia yupi?. Na hawa waumbaji wawili wapo tofauti kutokana na mafundisho yao kwani mmoja anahimiza amani, upendo na mshikamano wakati mwingine anahimiza mauaji, chuki, kujilipua, uzinzi n.k
 
Mbona mnajichanganya, mi nimeona tume ni waislam na mafisadi nao ni waislam. Mi sijaona mchango wa uislam hapo wala kosa la uislam. Nimeona mafisadi wametajwa majina na walichofanya.
Tumezoea kusikia majina yakitajwa lakini hakuna hatua. Tusubiri tuone itakavyokuwa au hiyo hotuba kukaririwa na watu kama bongo fleva au taarabu.
 
.........mmmh! hapa mkuu ungekuwa wazi kidogo unamzungumzia muumba yupi? maana kuna muumba yule aliyemuumba kwanza Adamu na Hawa halafu kuna yule muumba mwingine aliyeumba kalamu. Sijui unamzungumzia yupi?. Na hawa waumbaji wawili wapo tofauti kutokana na mafundisho yao kwani mmoja anahimiza amani, upendo na mshikamano wakati mwingine anahimiza mauaji, chuki, kujilipua, uzinzi n.k

Qur'an.2:117. Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa.
 
TATIZO SI KATOLIKI NDO WANAONGOZA ZANZIBAR? hii tuiitayo MoU?

JUMAMOSI STAR TV KULIKUWA NA KIPINDI CHA TUONGEE. MWENDESHA KIPINDI MWISHONI ALIULIZA MASWALI.

1. Ni kweli umaskini wa Tanzania na Zanzibar unatokana na watu wa dini fulani kuwa ndio wanaongoza dola?
2. Ni kweli ili tuendelee tunahitaji uwiano wa wafanyakazi mfano, wanaume wangapi, wanawake wangapi, waislam wangapi na wakaristo wangapi? je sababu hizo ndo kigezo cha kufanikiwa kama nchi?

Unapokuwa na Wafanyakazi 83% wa elimu ya Ubaguzi wa Ujinga wakashindwa kuiendesha nchi kwa miaka zaidi ya 50 kwa mafanikio inabidi ujitazame upya ni wapi penye utata.
 
Hapana. Siamini kama asiyekuwa Muislaam ni mjinga bali naamini kwamba asiyekuwa Muislaam amejazwa ujinga asiokuwa nao, hali kadhalika kuna Waislaam waliojazwa ujinga wasio nao.

Jee, wewe hujisalimishi kwa mola wako?

Sina haja ya kupoteza Almasi yangu kwa kipande cha chupa...Rejea Mathayo 28:18
....Nimepewa Mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu; na kukwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Kwahiyo zomba haya maneno yalisemwa mwaka 33 sasa sina haja ya kumsikiliza mwingine awaye yeyote aliyekuja miaka mia sita baadaye kwani hayo sio maagizo.... Rejea nilipoweka rangi ya blue ukizingatia kuwa ukamilifu wa dahari haujafikia... Huo ndio "ujinga" wangu/wetu kushika na kufuata maagizo halali..Ni hayo tu. Hatupepesi macho wala hatumung'unyi maneno....Aksante!
 
Mie nadhani tuwachane nao tu, hivi wanatusaidia nini katika huu Muungano hata sisi ndio tuung'ang'anie?.......


zomba
, leo kwa mara ya pili umepokea like yangu, Kuhusu suala la kuachana na hawa Jamaa, adui yetu number moja ni CCM.
CCM wanajua kabisa without Zanzibar they are Nothing, mark my words.
 
Hapana. Siamini kama asiyekuwa Muislaam ni mjinga bali naamini kwamba asiyekuwa Muislaam amejazwa ujinga asiokuwa nao, hali kadhalika kuna Waislaam waliojazwa ujinga wasio nao.

Jee, wewe hujisalimishi kwa mola wako?

Hahahahaaaaa!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo elimu ni madrassat pekee? hata waislamu walioenda kwenye elimu za sekondari na vyuo vikuu wamejazwa ujinga nao? Muislamu aliyesoma Madrassat tu bila kwenda hata chekechea yeye ndo hajajazwa ujinga?
 
Mnh! Hii habari ndefu kama barabara inahitaji muda. Bora ungeweka summary na link ya habari yenyewe. Labda ntarudi kupitia comments tu bila kuisoma.

pitia habari yote ndipo utoe comments,wewe ,comments zako si lolote pasipo kusoma habari, au ndio unataka kuleta ya ubunge wa kunga mkono hoja na kupiga makofi .........
 
pitia habari yote ndipo utoe comments,wewe ,comments zako si lolote pasipo kusoma habari, au ndio unataka kuleta ya ubunge wa kunga mkono hoja na kupiga makofi .........

Mkuu nisome vizuri kabla ya kuponda. Sijasema nita comment kuhusu hii habari bali nimesema nitarudi kupitia comments yaani kusome comments za wadau.
 
Hahahahaaaaa!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo elimu ni madrassat pekee? hata waislamu walioenda kwenye elimu za sekondari na vyuo vikuu wamejazwa ujinga nao? Muislamu aliyesoma Madrassat tu bila kwenda hata chekechea yeye ndo hajajazwa ujinga?

Wapo waliojazwa ujinga sana tu. Ambao ujinga hauwaingii kirahisi ni wale wanaoanza chuo halafu ndio darasa. Upo hapo ulipo?
 
Mtanisamehe hii habari ni ndefu, lakini ndivyo ilivyo kwani hii ni taarifa kamili ya kamati moja huko Zanzibar, endelea:

Serikali yavuliwa nguo

Posted on April 18, 2012 by zanzibarkwetu
manoor4.jpg

Mansour Yussuf Himid Machano Othman Said ni miongoni mwa mawaziri waliotajwa katika kamati teule ya baraza la wawakilishi ya kuchunguza ubadhirifu uliofanyika katika sekta mbali mbali na kutumia madaraka yao vibaya wakiwemo maafisa wa Ikulu Zanzibar

Kamati imebaini kwamba, Mikataba yote ya mauziano iliyofungwa baina ya Serikali na Ndg. Juma Ali Kidawa na baina yake na Ndg. Amina Aman Abeid Karume ni batili na ya udanganyifu. Aidha, Hati ya Matumizi ya Ardhi aliyopewa Ndg. Amina Aman Abeid Karume na Mhe. Mansour Yussuf Himid, kama tulivyoitolea ufafanuzi wake katika ukurasa wa 182-183, imekiuka taratibu za kisheria na kiutawala.

Mhe. Spika: Pia tumegundua kuwa: Mzee Juma Ali Kidawa sio Mmiliki halali kisheria wa Nyumba. iliyokuwa imefuatiliwa na wala hakuhusika na Uuzaji wa Nyumba hiyo kwa mtu yoyote na hakuwahi kufuatilia Utengenezaji wa Warka wa Nyumba hiyo.

Mhe. Spika:Hata hivyo, kwa mujibu wa nia njema na mazingira halisi yalivyojitokeza yanaonesha Mzee Juma Ali Kidawa alihusika na kufanya kazi kwa Mhindi aliyeimiliki nyumba hiyo kabla ya kutaifishwa na Serikali.

Mhe. Spika: Kamati imejiridhisha kwamba: Ndg. Ramadhan Abdalla Songa na Mama Fatma Karume walishiriki katika Udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano uliofungwa baina ya Serikali (Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati) na Ndg. Juma Ali Kidawa.

Mhe. Spika: Maelezo haya yanafafanuliwa katika ukurasa wa 178 hadi wa 180 wa ripoti yetu.

Mhe. Spika: Mbali na taarifa hizo, lakini pia Kamati imebaini kwamba: Ndg. Mwalimu Ali Mwalimu kama Katibu Mkuu, amechangia kufanyika kwa udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano baina ya Wizara yake na Ndg. Juma Ali Kidawa.

HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA BARAZA LA WAWAKILISHI-ZANZIBAR.

Endelea - Serikali yavuliwa nguo
Mansour nje ya serikali analiongeleaje hili kwa sasa?
 
Back
Top Bottom