Ukishangaa ya Uamsho, haya utasemaje?

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Mtanisamehe hii habari ni ndefu, lakini ndivyo ilivyo kwani hii ni taarifa kamili ya kamati moja huko Zanzibar, endelea:

Serikali yavuliwa nguo

Posted on April 18, 2012 by zanzibarkwetu
manoor4.jpg

Mansour Yussuf Himid Machano Othman Said ni miongoni mwa mawaziri waliotajwa katika kamati teule ya baraza la wawakilishi ya kuchunguza ubadhirifu uliofanyika katika sekta mbali mbali na kutumia madaraka yao vibaya wakiwemo maafisa wa Ikulu Zanzibar

Kamati imebaini kwamba, Mikataba yote ya mauziano iliyofungwa baina ya Serikali na Ndg. Juma Ali Kidawa na baina yake na Ndg. Amina Aman Abeid Karume ni batili na ya udanganyifu. Aidha, Hati ya Matumizi ya Ardhi aliyopewa Ndg. Amina Aman Abeid Karume na Mhe. Mansour Yussuf Himid, kama tulivyoitolea ufafanuzi wake katika ukurasa wa 182-183, imekiuka taratibu za kisheria na kiutawala.

Mhe. Spika: Pia tumegundua kuwa: Mzee Juma Ali Kidawa sio Mmiliki halali kisheria wa Nyumba. iliyokuwa imefuatiliwa na wala hakuhusika na Uuzaji wa Nyumba hiyo kwa mtu yoyote na hakuwahi kufuatilia Utengenezaji wa Warka wa Nyumba hiyo.

Mhe. Spika:Hata hivyo, kwa mujibu wa nia njema na mazingira halisi yalivyojitokeza yanaonesha Mzee Juma Ali Kidawa alihusika na kufanya kazi kwa Mhindi aliyeimiliki nyumba hiyo kabla ya kutaifishwa na Serikali.

Mhe. Spika: Kamati imejiridhisha kwamba: Ndg. Ramadhan Abdalla Songa na Mama Fatma Karume walishiriki katika Udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano uliofungwa baina ya Serikali (Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati) na Ndg. Juma Ali Kidawa.

Mhe. Spika: Maelezo haya yanafafanuliwa katika ukurasa wa 178 hadi wa 180 wa ripoti yetu.

Mhe. Spika: Mbali na taarifa hizo, lakini pia Kamati imebaini kwamba: Ndg. Mwalimu Ali Mwalimu kama Katibu Mkuu, amechangia kufanyika kwa udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano baina ya Wizara yake na Ndg. Juma Ali Kidawa.

HOTUBA YA MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA BARAZA LA WAWAKILISHI-ZANZIBAR.

Endelea - Serikali yavuliwa nguo
 
zomba, umefika wakati sasa turudi tukaijenge Zanzibar na kuwarudi bila huruma watu wanaokula pale wasipopanda....hiyo imekaaje? Naona hata kelele za muungano sitapungua kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Mnh! Hii habari ndefu kama barabara inahitaji muda. Bora ungeweka summary na link ya habari yenyewe. Labda ntarudi kupitia comments tu bila kuisoma.
 
Kuna viongozi wana-take advantage ya hii migogoro iliyopo huko visiwani kufanya ufisadi.by the time watu wanashtuka wanakuta tayari ni too late. Wazenji wawe makini sana na viongozi wao maana wengi wao wamejivika ngozi za kondoo
 
Uislaam ni kwa walimwengu wote, hata wewe, basi tu umejazwa Ubaguzi wa Ujinga ndio maana hujielewi.

TATIZO SI KATOLIKI NDO WANAONGOZA ZANZIBAR? hii tuiitayo MoU?

JUMAMOSI STAR TV KULIKUWA NA KIPINDI CHA TUONGEE. MWENDESHA KIPINDI MWISHONI ALIULIZA MASWALI.

1. Ni kweli umaskini wa Tanzania na Zanzibar unatokana na watu wa dini fulani kuwa ndio wanaongoza dola?
2. Ni kweli ili tuendelee tunahitaji uwiano wa wafanyakazi mfano, wanaume wangapi, wanawake wangapi, waislam wangapi na wakaristo wangapi? je sababu hizo ndo kigezo cha kufanikiwa kama nchi?
 
Inafurahisha kuona wenzetu wanaripuana kiukweli kabisa wala hawamumunyi maneno.

Hakuna Tofauti ya:-

1. Mkapa na Mkewe pamoja na familia zao na marafiki.
2. KIkwete na mkewe, wanawe na familia zao na marafiki.

By the way mbona husemi kuhusu kikwete na Mkapa? au hawa sio wazanzibari?
 
Mie nadhani tuwachane nao tu, hivi wanatusaidia nini katika huu Muungano hata sisi ndio tuung'ang'anie?
Akhuu...mimi siung'ang'anii labda wewe hapo na huyo jirani yako. Mimi kama naenda Zenj au Mombasa basi fahamu fika naenda kutembea. sio kula sikukuu wala kwenda semina mkuu.
 
Kwahiyo asiyekuwa muislamu ni mjinga?

Hapana. Siamini kama asiyekuwa Muislaam ni mjinga bali naamini kwamba asiyekuwa Muislaam amejazwa ujinga asiokuwa nao, hali kadhalika kuna Waislaam waliojazwa ujinga wasio nao.

Jee, wewe hujisalimishi kwa mola wako?
 
Akhuu...mimi siung'ang'anii labda wewe hapo na huyo jirani yako. Mimi kama naenda Zenj au Mombasa basi fahamu fika naenda kutembea. sio kula sikukuu wala kwenda semina mkuu.

Kilio cha nini? tulilie kuuvunja huu Muungano, usio na manufaa kwetu. Au unasemaje?
 
Hakuna Tofauti ya:-

1. Mkapa na Mkewe pamoja na familia zao na marafiki.
2. KIkwete na mkewe, wanawe na familia zao na marafiki.

By the way mbona husemi kuhusu kikwete na Mkapa? au hawa sio wazanzibari?

mkapa na Kikwete inawahusu nini? au unalo unalotaka kufunguka? funguka!
 
Back
Top Bottom