Ngoja niongee kiutu Uzima. Mkinambia Magufuli alitegeneza maadui kwa kujaribu kuitoa shilingi mfuko wa matajiri na kuiweka kwa maskini na maendeleo, hilo nakubali kabisa. It was some sort of Socialism ambayo kwa Tanzania ni Siasa isotakiwa kabisa. Mambo matatu ya kutazama.
1. Kukisafisha Chama kurudisha mali za chama kina Kinana wakajiuzuru.
2. Swala la Makinikia na madini (Wawekezaji kina Barrick na Symbion).
3. Swala la Chanjo ya Uviko 19 (Hili big Corparates za madawa). Haya yote yalipongezwa na Wananchi walio wengi lkn Maadui wachache wenye nguvu kubwa.
Now, Tundu Lissu pia mkinambia alitengeneza maadui na ndani ya TISS kwa kuwatukana mara kwa mara, sijui mwambieni alowatuma aje! Kutwa akidai wanataka kumuua toka akiwa Dar! Siku moja alifikia kusimama akatoka nje ya gari na kukaripiana nao (kwa madai yake). Yawezekana Usalama walimweka kilema ajue nguvu yao lkn nia yao sii kumuua.
Pili, Lissu akitafuta Urais kwa nguvu kubwa akijihusisha sana na Mashirika ya nje, jambo ambalo ndani ya Chadema hawakuliafiki. Hii ni katika fikra tu japo haingii akilini.
sasa kama walinzi hawakuondolewa walifanya nini wakati Lissu anashambuliwa?
Unauliza walijuaje kuwa Lissu ataenda kula lunch?
Niliwahi kusikia kwamba Lissu alikuwa na tabia ya kula lunch nyumbani kwake kipindi anapokuwa kwenye vikao vya bunge.
Masuala ya CCTV nilisoma kwenye gazeti wakimnukuu RPC wa Dodoma. Sijasikia Polisi wakikanusha kupatikana kwa camera hizo.
masuala ya Lissu na dereva Polisi wanatakiwa kutoa wito kama wanaamini watasaidia uchunguzi.
Na Lissu amefika kwa RPC Dodoma zaidi ya mara mbili toka ashambuliwe Polisi wangeweza kumhoji.
Umesoma majibu yako? Unasema Uliwahi kusikia Lissu alikuwa na tabia ya kwenda kwake kula chakula! Ya kuambiwa hayo huna hakika.
Yaani Lissu arudi kula lakini viongozi wabunge wengine wote wasiende kula makwao siku hiyo! Hata kumkaribisha Mbowe, mwenyekiti wake!
Okay, nambie ni nani alokuwa mpishi wake, wewe umeambiwa nani, unamjua? Kwa nini mpaka leo hii Lissu anasema sijui mfanyakazi wake alikuwa akifanya kazi kwa Naibu Spika! Sio kwake, Na kamtaja jina lakini sio mke wake wala mpishi wake wa wakati wote huo! Nani alokuwa akimpikia chakula Tundu Lissu? Yuko wapi mpishi huyo?
Na wakati anapigwa risasi mpishi wake alikuwa wapi hadi aje asaidiwe na mpishi wa naibu Spika! (Kwa madai yake)
Kuhusu Walinzi, mimi nakumbuka mh. Kitwanga amewahi kusema palikuwa hakuna walinzi getini ila kila kiongozi alikuwa na mlinzi wake haswa wakati wa usiku. Sikumbuki kama alizungumzia haya wakati ule au Kisa cha Mbowe kuvunja mguu.
Namalizia kusema hivi hata picha za pale kwenye tukio hakuna hata picha moja inayoonyesha getini, aidha hata Mbowe na viongozi walikwenda Hospitali alikopelekwa na sio pale kwenye tukio. Kifupi, nimalizie intelejensia yangu. Sehemu ile haiwezekani kabisa kusiwe na watu waloona tukio hilo likifanyika mchana jua kali hata kama Viongozi hawakuwepo.