..Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kampeni za Uraisi 2020 Lissu aliwataja kwa majina wadada wawili, pamoja na dereva wake, ambao walimtoa eneo aliposhambuliwa na kumuwahisha Dodoma Hospital.
..Kwa hiyo majina yao yapo na yeyote anayetafuta ukweli anaweza kuyahakiki kwasababu ni mambo ambayo Lissu ameyasema hadharani.
..Kuhusu dereva, aliwahi kuhojiwa na Shirika la Habari la Ujerumani DW na alijitambulisha kwa majina yake, na pia alieleza kilichomtokea yeye na Tundu Lissu.
..Kuhusu suala la Tundu Lissu na dereva kuhojiwa naamini Polisi ndio wanaopiga danadana. Kama vyombo vya habari vimeweza kumfikia na kumhoji Lissu haiingii akilini Polisi nao kushindwa kufanya hivyo.
..Vilevile habari zilizoingia hivi punde ni za Lissu kufika kwa RPC Dodoma kuona gari lake ambalo alishambuliwa akiwa ndani yake. Kwa hiyo mpaka hapo utaona kwamba hoja kwamba Polisi hawawezi kumfikia Lissu haina ukweli wowote.
..Mwisho, upo uwezekano mkubwa kwamba kuna majirani wengi ambao waliona kilichotokea wakati Lissu anashambuliwa. Ni bahati mbaya kwamba vyombo vya habari havikufanya jitihada kuwahoji majirani wanaoishi eneo aliposhambuliwa Lissu.
Mkuu kama huna ushahidi wa jambo lolote isipokuwa hearsay ndio yale nayosema ya Wachungaji - Changanya na zako!
Kama Tundu Lissu aliokolewa na Wasichana wawili katika eneo nyeti la makazi ya Viongozi huoni kama kuna mushkeri katika habari hii? Yaani hapakuwa na wwtu wentine isipokuwa wasichana wawili vijakazi!
Yaani block nzima wasitokee watu isipokuwa wasichana wawili ambao wewe huwajui ila unanambia nikasome hotuba yake. Najua aliwahi mtaja Rehema mfanyakazi wa Naibu Spika lakini mpishi wake yeye ni nani? Unamjua au ndio habari ya kuambiwa!
Dereva wake nimesema hapo nyuma tulipewa majina matatu tofauti, wewe una hakika gani alohojiwa Ujarumani ndiye dereva wake alokuwa naye siku ile. Huyo Dereva kenda Ujarumani kufanya nini? Kwa nini kenda kuhojiwa na vyomvo vya habari Ujarumani na sio Polisi ya Tanzania? Na Ili iweje? Kama sii kampeni za kuendelea kutafuta wafadhili.
Okay, Lissu karudi nchini kwa nini dereva hajarudi? Nina hakika Chadema wanamjua, Bunge linamjua na akiwepo yeye atasaidia sana Uchunguzi pengine yeye anajua ndiye suspect namba moja! Kuna tatizo gani kumleta dereva!
Hakuna anayepinga Lissu kupigwa risasi lakini msala wake haukukaa vizuri kama kwamba kuna vitu wanaficha mpaka leo. Mimi nadhani ilitokea nje ya pale wakajivuta mpaka pale kisha akajenga hoja ya kuilaumu serikali maana risasi 30 naa watu wasitokee kabisa ila hao wasichana sijui wanawake!
Lissu kenda kwa RPC kulitazama gari lake lakini hataki kuhojiwa na vyombo vya Serikali kwa sababu yeye ni victim. Ati kama angekufa wangefanyaje? Alaaa upo hai unataka waanzie wapi kama sio kwako? What if sii sababu kabisa.
Yaani Lissu yupo radhi kwenda kwenye vyombo vya habari kueleza kisa mkasa lakini hataki kukutana na maswali ya kiintelejesia! Okay mbaya wake hayupo tena kwa nini bado hataki kuhojiwa akiulizwa anasema mbona hakuhojiwa akiwa Nairobi wala Belgium! So what? Upo hapa sasa hivi kwani shida iko wapi? Je unataka hili swali liwe resolved au unataka iwe hadithi ya maisha yako!
Binafsi simuani huyu jamaa toka namjua. Najua he is very ambitious to be the next President kwa kutumia huruma ya Wananchi lakini sii kwa njia hizi. Kweli haikufaa kabisa madhara alopata lakini he is not cooperating na vyombo vya sheria.
Yeye kila siku ni Ushindani iwe na wanasheria au Serikali. Utawezaje kuwa rais wa nchi ikiwa vyombo vya Sheria huviamini wala hutaki kushirikiana navyo? Wee ni kualaumu tuu basi itabidi watumishi wote wafukuzwe kazi uunde jeshi lako!
Am sorry, mimi naishia hapa nisije poteza mwelekeo wa.mada hii kwa sababu ya mpuuzi mmoja Tundu Lissu.