Ukishangaa ya musa .....Manji versus Kagoda, ngoma inogile | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukishangaa ya musa .....Manji versus Kagoda, ngoma inogile

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ngambo Ngali, Mar 1, 2011.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kampuni ya Quality Finance Corparation Ltd (QFC) amefungua madai ya fidia ya Sh. bilioni 18.7 Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, kama hasara kwa kiuka makubaliano ya mkopo katika ya yao Septemba 12, 2005.
  Kadhalika, kampuni ya QFC, imeomba mahakama itoe amri kwa kampuni ya Kagoda kulipa riba ya fedha iliyozidishwa.
  Kupitia hati ya madai hayo pia, kampuni ya QFC, imeomba kulipwa fidia ya hasara na usumbufu kutokana na mahakama itakavyoamua.
  Katika madai ya msingi, mlalamikaji aliingia kwenye makubaliano ya mkopo na mlalamikiwa Septemba 12, 2005, ambapo alipokea Sh. 31,710,000,000 ambao ulitakiwa kurejeshwa na riba kwa miaka mitatu.
  Ilidaiwa kuwa makubaliano hayo yalitekelezwa nusu. Mlalamikaji alipokea Sh. bilioni 31.7 kama mkopo ambapo aliweza kurejesha Sh. 18,710,000,000 kama walivyokubaliana kwenye mkataba wao.
  Ilidaiwa kuwa Januari, 2008 mlalamikaji alijulishwa na mamlaka husika kwamba kumegundulika ukiukwaji wa taratibu kwenye vyanzo vya fedha hizo.
  Aidha, baada ya taarifa hiyo, mlalamikaji alilazimika kuzirejesha Sh. bilioni 31.7 ambapo alilipa zaidi kwa kuzidisha Sh. bilioni 18 ambazo alimlipa mlalamikiwa na kujikuta anapata hasara.
  Hata hivyo, baada ya mlalamikaji kumtaka mlalamikiwa kumtejeshea zile fedha za ziada jitihada hizo hazikuzaa matunda hivyo anaiomba mahakama kumuamuru amlipe kabla ya muda wa makubaliano haujapitwa na wakati. Kupitia hati ya madai, mlalamikaji anaona ana haki ya kulipwa hasara hiyo aliyoipata kutoka kwa mlalamikiwa, kwa kuwa kitendo hicho kimemvunjia hadhi na heshima kwa jamii.
  Mlalamikaji ameomba mahakama itoe amri ya kumrejeshea Sh. bilioni 18.7 na riba ya asilimia 18 kwa fedha hizo tangu siku mkataba ulipokosewa hadi siku hukumu itakapotolewa. Pia, hasara za jumla alizozipata, gharama za kuendesha kesi vyote vilipwe na mlalamikiwa pamoja na malipo mengine ambayo mahakama itaona yanafaa kufanyika.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  ????????
   
 3. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii Kesi imefunguliwa lini???.....Mimi na badilisha fani..naenda kusomea uwakili maana naona kuna kesi nyingi kukubwa zenye lengo ya kuchakachua mambo na wala sio serious!!! aaaghhrr
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Washaanza mazingaombwe tena :A S 13:
   
 5. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tanzania inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno, tuwang'oe meno walaji ili wenye moyo wasijekata tamaa ya kuijenga!!!!:msela:
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Tukumbuke jinsi viongozi wote wa nchi hii ikiwamo IGP Mwema walivyodai kutoifahamu KAGODA! ...kama rais alivyodai kutoifahamu DOWANS!!! Sasa fikiria wanagawana mali zao za wizi mpaka wanaanza kugomabana tena kwenye MAHAKAMA (sina uhakika kama ni zetu tena). hii inanikumbusha zamani utotoni baba akiondoka nyumbani tunacheza na kurukaruka kila sehemu lakini akirudi wote tunakuwa kimya. JE, SISI BABA YETU (sijui rais!!??) (WA-TZ) ATAREJEA LINI NYUMBA ITULIE???? AIBU KWA KILA MTANZANIA
   
 7. M

  Matarese JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mh hivi jamani, nakumbuka waziri Meghji alisema fedha ya kagoda imetumika kwenye mambo ya usalama wa Taifa. Sasa huyu Manji ndio usalama wa Taifa?
   
 8. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Hii habari imenishangaza. Imenikumbusha moja ya vielelezo vilivyotolewa na upande wa Mengi kuthibitisha kuwa Manji ni "fisadi papa" vilivyokataliwa na mahakama katika kesi ya kudaiwa fidia ya sh. moja na kuomba radhi. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia ushahidi unaomhusisha Manji na Kagoda. Siku zote nilikuwa najiuliza ilikuwaje Manji kurejesha fedha za EPA wakati si mmoja wa waliochukua? Kumbe connection iko kwenye Quality Finance Corporation?

  Hata hivyo, kwa jinsi na namna habari ilivyotoka kwenye gazeti la Nipashe pekee natilia shaka huenda ni mkakati wa "fisadi nyangumi" kumkandamiza "fisadi papa" hadharani ili hata anachodai mahakamani kionekane ni ubabaishaji tu. Aidha, nashindwa kumuelewa Manji anamdai nini Mengi mahakamani endapo kweli hizo connection za QFC na Kagoda zipo? Anatafuta kusafishwa sifa ya ufisadi? HAsomi alama za nyakati? Anafikiri vinara akina RA, Somaiya, EL et al waliominya ni wajinga?
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,607
  Trophy Points: 280
  Hapo game ilikuwa Money Laundering zile fedha za EPA kupitia KAGODA, good news kumbe fedha zote za Kagoda zilirejeshwa!, no wonder Kagoda kamwe haitashitakiwa kwa vile haidaiwi chochote.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, gemu limechezwa kama ifuatavyo
  1. Kagoda imelipwa cheki ya Bilioni 40 toka BOT, ikakata commision yake ya na kubakisha bilioni 8, 390,000 na balansi ya bilioni 31,710,000,000 ikapitishiwa Quality Finance Corparation Ltd (QFC) ikionekana Manji amekopa Kagoda. Kwa vile Kagoda sio financial institution, haiwezekani Manji akakope fedha nyingi hivyo na kuzipata on the spot!. Kwa vile mhusika wa Kagoda ni RA aliamuakusafishia fedha kwa Manji just incase likibumburuka asifilisiwe.
  2. For banking proposes, ilibidi Manji ajifanya amekopa toka Kagoda ili transifer ya kiasi kikubwa hicho cha fedha kisilete mashaka. Kwa wale ambao ni wazuri wa kukonect the dots, fuatilieni mtashudia tarehe za ukwapuaji zinafana na tarehe za kukopeshana huku. Fedhailikuwa inaingia account ya RA na keshoyake inahamishiwa accounti ya Manji eti ni mkopo na keshukutwa wanairudisha eti wamelipa deni?.
  3. Baada ya Manji kupewa zile bilioni 31,710,000,000 alizojifanya amekopa, akatoa bilioni 18,710,000,000 na kuzilipa CCM kwa matumizi ya kapeni ya JK huku kwenye vitabu vyake, ikionekana ndio kama amelipa deni, kwa ahadi zilizobakia, watagawana na RA kwa wakati wao, kwa sababu pesa hizi tayari zimeshatakatishwa!.
  4. Scandali ya Kagoda ilipofumka, vitabu vilionyesha 31,710,000,000 imelipwa kwa Manji, na Manji alipofuatwa alikubali kweli kiasi hicho alikopeshwa, nadhani baada ya kutiwa ja...ja.., alikubali kukirudisha kiasi chote cha 31,710,000,000 kwa BOT na sio kwa Kagoda, ili aepuke kusimamishwa kizimbani.
  5. Baada ya Manji, kurudisha ile fedha ya wizi ya Kagoda, ndipo sasa akamrudia RA kumuuilizia vipi kuhusu ile 18,710,000,000 aliyoilipa CCM akijifanya amelipa deni?. Ndipo RA akamtolea nje, kwamba kwa vile dili imebumburuka, hiyo hiyo 18,710,000,000 imekula kwake!. Manji ndio sasa hakubali eti anataka kwenda mahakamani kuishitaki Kagoda!.
  6. Kama ungekuwa ni mkopo wa halali, na ni kweli alishalipa zaidi ya nusu, alipofuata na ile tume ya EPA, kwanini alirudisha fedha zote 31,710,000,000 badala ya kupunguza kwanza zile 18,710,000,000 alizodai, alikwisha lipa na kurejesha 13,000,000,000 tuu?!.
  7. Mkifuatilia tangu tarehe Manji alipokopa, mpaka tarehe ilipolipa hiyo nusu mtakuta there was no time ya kufanya biashara na kupata faida hiyo na kuilipa zaidi ya diliya kuzungusha tuu fedha.
  8. Hata kama ilikuwa ni biashara halali ya kukopeshana fedha, kama kweli Manji alikopeshwa hizo 31,710,000,000 na baadaye kulipa kwanza 18,710,000,000 na baadaye kurudisha ile 31,710,000,000 kamili, akajikuta amewazidishia ile 18,710,000,000 aliyolipia deni, bado hawezi kuidai hiyo 18,710,000,000 kama ilivyo, maana atakuwa hajalipia riba yoyote, na maani mkopo huowa mabilioni ulikuwa hauna riba yoyote ndio maada nasisitiza hii ilikuwa ni dili yao tuu.
  9. Kwa mchezo huu, sasa na mimi ndio napata picha, Mzee Mengi, alipata wapi guts za kuwataja kwa majina MAFISADI PAPA bila kumungunya maneno.
  10. Mwenye kisu kikali ndie atakula nyama, kwenye kesi ya Manji kumdai Mengi shilingi 1/=, Manji ndie atashinda ila Mengi atagoma kushindwa na atakata rufaa ambayo nayo itatupwa na hapa ndipo sinema ya kweli itaanza!.
  Pasco.
   
 10. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Jamani jamani na mimi umenifungua akili kwa hili lazima tuandamane.
   
 11. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Uende wapi???!!
   
 12. A

  Anold JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Nimelazimika kujifunza vitu kadhaa kwenye hili;

  1. Kuna haja ya kujua ukweli wa jambo kabla ya kuingiza ushabiki na hisia
  2. Kuna mambo mengi yamefichwa ukweli wake kiasi kwamba taarifa nyingi
  tunazopata kupitia vyanzo ambavyo wakati mwingine havina taarifa sahihi.
  3. Makampuni/Watu wanaolalamikiwa wamekuwa wazito kutoa taarifa sahihi
  kwa umma kitu kinachosababisha waeleweke vibaya kwa jamii wakati
  mwingine bila sababu za msingi.
  4. Kuna siri nyingi ambazo zimefichika ambazo ninaamini hata vyombo
  vinavyosimamia sheria vimedanganywa au niseme havina taarifa sahihi juu ya
  mambo fulani; kwa mfano tuliambiwa Dowans ni kampuni kutoka COSTARICA
  lakini mtu aliyejitambulisha kuwa ni mmiliki sio mtu wa Costarica mbaya sana
  kuna tetesi kuwa kampuni hiyo ipo falme za kiarabu japo waziri alituambia kuwa
  ni kampuni ya Costarica
  5. kwa hali hii, mambo mengi kumegubikwa na usiri mkubwa kiasi cha
  hata kumdanganya hata waziri. Ni wazi kuwa kazi iliyopo ya kusimamia raslimali
  za taifa ni kubwa ni nyeti kwani mambo mengi yenye maslahi kwa taifa
  yamefanywa kuwa siri kiasi cha kuruhusu wapotoshaji na watu wenye nia
  mbaya watoe taarifa za kiuchunguzi ambazo nyingi naamini sio sahihi.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Ninavyomjua Manji anavyoijua pesa hilo la kukosea na kulipa 18bn zaidi kwa makosa halitaingia akilini mwangu asilani....
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sheria ya mikataba kifungu cha 24 kinasema:

  Agreements void if considerations and objects are unlawful in part
  If any part of a single consideration for one or more objects, or any one or any part of any one of several considerations for a single object, is unlawful, the agreement is void.

  Kwa kifungu hicho naona kama hakukuwa na mkataba.
   
Loading...