Ukisema Jini tayari kuna majini miatatu karibu yako. Kila mtoto mchanga huguswa na jini dakika moja bada ya kuzaliwa. Vitabu vya dini vinasemaje?

Mkuu kila mtu ana alipotoa maelezo yake kuhusu hao viumbe,sasa wewe unadhani maelezo ya kwamba majini kuwa ni malaika yanaendana na uhalisia?
Amini unavyotaka kuamini lakini UKWELI nimeshakuambia. Narudia tena kuandika; hakuna tofauti kati ya Majini na Malaika Waasi, jini ni shetani na shetani ndiyo huyo huyo jini, hakuna tofauti yoyote ile.

Uamuzi ni wako mwenyewe, kuichagua KWELI au kuchagua uongo.
 
Mimi ningetamani kujua kama majini yanamuabudu mungu, kitabu chao ni kipi? Na kimeandikwa na nani?
Yaani jini au mtu?
 
Amini unavyotaka kuamini lakini UKWELI nimeshakuambia. Narudia tena kuandika; hakuna tofauti kati ya Majini na Malaika Waasi, jini ni shetani na shetani ndiyo huyo huyo jini, hakuna tofauti yoyote ile.

Uamuzi ni wako mwenyewe, kuichagua KWELI au kuchagua uongo.
Mkuu hapa hatulazimishani bali tunajadiliana tu,Ila kama umeamua kuamini hivyo unavyoamini na hautaki mjadala juu ya hilo basi sawa.
 
Hakuna majini wazuri Yote ni mashetani.
Sifa za malaika zinajulikana na sifa za majini zimeshaelezwa,sasa nyie sijui kinawapata kipi hadi mkachanganya majini na malaika!

Hata majini wote wangekuwa wabaya Ila majini watabaki kuwa majini na malaika watabaki kuwa malaika.
 
Duh kaka!yaani unamaanisha kama boeng 787 dreamliner ikitua airport basi bomberdier zote zitimke kuelekea zanzibar?YESU NI YEYE YULE JANA LEO NA KESHO.
Kwa sababu umesema jina Yesu likitamkwa mashetani wote(malaika) hukimbia,maana hao mashetani asili yao ni malaika hivyo unasema mashetani basi unazungumzia malaika.
 
Hapo sasa sijaelewa,wewe unasema kifo kinatupata kwa sababu in adhabu na wengine wanasema kifo kinatupata kwa sababu ya kuwa na hii miili,kwa maana hivyo wasio na maumbo ambao ni roho hawafi.
Ukisoma Biblia unaona baada ya Adamu na Hawa kuifanya dhambi ndio Bwana Mungu akasema hakika utakufa, utayarudia mavumbi ambamo ulitwaliwa. Tatizo sio mwili bali dhambi hata tukifufuliwa tutakuwa na miili mipya lakini hatutakufa tena. Kwaiyo suala la kufa ni kufa tuu hata kisicho na mwili chaweza kufa na kilicho na mwili chaweza kuishi milele kwa mapenzi ya Mungu
 
Hata mie najua mwenye sifa ya kutokufa ni Mungu pekee ila nashangaa watu humu wanasema roho zisizo na mwili nazo zina sifa za kutokufa kama Mungu.
 
Mkuu sijataka watu waamini uzuri wa jini au ubaya wake ila nilileta mada tujifunze pamoja bila kuingilia muhimili wa dini zetu

Lakini naomba nikuulize ni malaika wangapi walimwasi mungu?! Na kwanini katika wingi huo ulioutaja ila Bible inamtaja Lucifer kama ndie malaika alie muhasi Mungu na si hao makabila 72 elfu wa majini?!

Je unaamini kwamba shetani ni kiumbe yeyote mwenye kufanya yasiopendeza akiwemo mwanadamu?!

Sijajua lengo lako ni nini hasa mana mada imeeleza maisha ya viumbe hao na si wema ama ubaya wao na bado nimeonesha njia za kukukabiliana nao lakini pia hat

,Mkuu shetani si kiumbe yeyote mwenye kufanya yasiyopendeza. Shetani ni Mmoja ni mmoja tu ambaye ni Lucifer au Ibilisi.
Ni kama kusema Mungu ni kiumbe yeyote atendaye mambo yanayopendeza. Hasha Mungu ni mmoja.

Ila kwa kigezo cha sifa, unaweza muita mtu shetani ingawa yeye si shetani.
Unaweza kumuita mtu simba ingawa mtu huyo si simba.
Ndio maana wakristo humuita Yesu kutokana na uwezo aliouonyesha hapa dunia lakini Ukweli ni kuwa Yesu si Mungu, Bali anasifa za kiungu.

Idadi ya malaika walioasi haijawekwa wazi bila shaka haina umuhimu wala haina athari kwa mwanadamu.
Lusifa ni mmoja ambaye ni shetani, mtu akitenda uovu husemwa ameingiliwa na roho yab uasi ambayo ndio shetani huyo ijapokuwa anaweza asiwe yule joka kuu
 
Sifa za malaika zinajulikana na sifa za majini zimeshaelezwa,sasa nyie sijui kinawapata kipi hadi mkachanganya majini na malaika!

Hata majini wote wangekuwa wabaya Ila majini watabaki kuwa majini na malaika watabaki kuwa malaika.
Sijazungumzia malaika. Usidandie ndege kwa mbele!
 
Sijazungumzia malaika. Usidandie ndege kwa mbele!
Basi hakuna kiumbe kilichoumbwa kinaitwa shetani,tunaambiwa malaika waliyoasi ndio mashetani.

Sasa hapo nimedandia nini?au mnaposema shetani kichwani mwenu mnajenga picha ya kiumbe tofauti na malaika Ila mkija hapa mnasema majini na mashetani ni malaika waliyoasi.
 
Ukinilimit namna ya kukujibu sitaweza kukujibu,ila tambua ya kuwa majini waliishi hii dunia katika miaka mig nyuma kabla ya uwepo wa mwanadamu na alijengea himaya kubwa ya utawala katika enzi ya Jann na Jadda,
Kuumbwa kwa mwanadamu kwa udongo ni kama kureplace kuumbwa kwa mwanadamu kwa Moto ambapo mwanadamu wa udongo amekuja kuwa juu ya moto na nadhani waona moto hauwezi kuwaka juu ya udongo ila udongo huweza kukaa juu ya moto

Soma taratibu nilichokujibu utaelewa kwa sababu gani moto umekuwa wa kwanza kuwapo duniani kabla ya udongo
Mkuu naomba ufafanuzi zaidi kwa paragraph ya mwisho unaposema "moto umekuwa wa kwanza kuwepo Duniani kabla ya udongo"
 
Basi hakuna kiumbe kilichoumbwa kinaitwa shetani,tunaambiwa malaika waliyoasi ndio mashetani.

Sasa hapo nimedandia nini?au mnaposema shetani kichwani mwenu mnajenga picha ya kiumbe tofauti na malaika Ila mkija hapa mnasema majini na mashetani ni malaika waliyoasi.
Ok naomba nieleweke hivi:

Majini ni evil spirits.
 
Hawawezi kuongezeka maana wao hawana mfumo wa "uzazi" kama viumbe wengine, malaika hawazaliani kama binadamu. Ukisikia watu wanasema majini wanazaliana huo ni uongo mtupu, ni hadithi tu za "alinacha", mambo ya kufikirika, maana majini ndio hao hao malaika waasi na hawana uwezo wa kuzaliana wao kwa wao. Idadi yao ni kamili, haiongezeki wala haipungui.

Ndiyo binadamu naye anaweza kuitwa "shetani", sababu maana ya shetani ni adui, kama nilivyokuambia malaika waasi jina lao la asili siyo "shetani" bali ni "Malaika" au "Wana wa MUNGU".

Jina lingine ambalo MUNGU alilitumia kuwaita hawa malaika ni "Azazel". YESU alisema hivi; "ukitenda dhambi unakuwa mtoto wa Shetani na baba yako anakuwa ni Shetani, ukitenda mema unakuwa ni mtoto wa MUNGU na BABA yako anakuwa ni MUNGU".
Kaka nikusaidie kitu,unapokuwa hujui kitu jaribu kuwa makini wakati unatetea hoja ya kile usichokijua,ukiwa msomaji mzuri wa biblia utaona imeeleza wazi kuhusu majini,na malaika lakini ukisoma vitabu vile vilivyotolewa utakutana na vitabu kadhaa vikieleza maisha kabla ya mwanadamu na ulimwengu wa kwanza,

Soma tena Bible ikibidi weka na Quran utaona bado hujajua undani wa viumbe wa mungu
 
Inaonesha wazi hili jambo linawachanganya.
Ni kweli linawachanganya na hawajui wanachotetea
Wakubali tu mada hii imewazid uwezo na mimi nawaomba tena wasome upya biblia,wasome hata vile vitabu vilivyoondolewa hakika hawatachangaya malaika na jini ya kuwa ni kitu kimoja wanatofautina kwa utii na usaliti

Unajua watu wengi hawajui hata kwanini tunatumia kalenda ya jua ikiwa hata majini nao anatumia jua kuhesabu siku zake
 
Kaka nikusaidie kitu,unapokuwa hujui kitu jaribu kuwa makini wakati unatetea hoja ya kile usichokijua,ukiwa msomaji mzuri wa biblia utaona imeeleza wazi kuhusu majini,na malaika lakini ukisoma vitabu vile vilivyotolewa utakutana na vitabu kadhaa vikieleza maisha kabla ya mwanadamu na ulimwengu wa kwanza,

Soma tena Bible ikibidi weka na Quran utaona bado hujajua undani wa viumbe wa mungu
Acha kujidanganya mkuu, utasoma vitabu utamaliza dunia nzima, lakini ukweli utabakia palepale, hakuna tofauti yoyote ile kati ya Jini na malaika waasi wote hao ni kitu hicho hicho kimoja. Jini ndiye shetani na shetani ndiye jini.
 
Back
Top Bottom