Ukipingana na Viongozi Wako wa Juu ni Lazima Ujiuzulu Nafasi Zako

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
40,000
Mazoea yanajenga tabia; na mazoea mabaya yanajenga tabia mbaya. Katika utendaji wa kazi au utumishi wa aina fulani kuna mambo ambayo yamezoeleka na mengine yanakuwa kama tabia tu iliyozoeleka. Katika siasa za nchi yetu sasa hivi kuna hili la watu kuanza kuzoea miongoni mwa tabia za kiwoga na zisizo na nidhamu; mtendaji wa chini au mtumishi wa chini anaposimama kupingana na mabosi wake na wakati huo huo anataka kuendelea na nafasi yake aliyokuwa nayo. Haya ni mazoea mabaya.

Katika kudumisha nidhamu ya kazi au kuhakikisha ufanisi unaonekana mahali pa kazi ni lazima watendaji waaminiane na waweze kufanya kazi pasi ya kushukiana. Inapotokea tu kuwa hakuna imani kati ya watumishi basi ufanisi na utendaji kazi hauwezi kufanikiwa kwani mahali pa kazi panaweza kugeuka kuwa ni mahali pa mipasho, majungu, tetesi na tuhuma zisizokoma.

Hata hivyo inatokea wakati ambapo watumishi wa juu wanaona walioko chini hawaenendi na utaratibu wa kazi hivyo watumishi wa juu kwa madaraka yao wanaweza kuwaita kuwahoji walioko chini na hata kuchukua kile kinachoitwa "hatua za kinidhamu" kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao. Kuna mambo mengine hatua za kinidhamu zinahitaji mamlaka ya juu zaidi. Meneja au Mkurugeni wa Idara fulani anawajibika kwa mambo yanayofanyika chini yake na ana jukumu (kwa mujibu wa taratibu za mahali) kusimamia nidhamu kwa walio chini; inapotokea kuwa hakuna nidhamu basi ni yeye atakayewajibishwa na ngazi za juu.

Hili ni kweli katika makampuni au mashirika ya binafsi na hata ya umma; na nikweli kwa Tanzania kama ilivyo kweli kwa Marekani, Japan au Uchina. Kiongozi wa chini anapokuwa na matatizo na kiongozi wake wa juu ambaye anawajibika kwake moja kwa moja basi ana njia ya kutoa malalamiko yake kwake na kama hilo haliwezekani basi kwenda kwenye chombo cha juu zaidi. Hili linafanyika kwa taratibu zilizowekwa.

Hata hivyo, kiongozi anapoamua kwenda hadharani kutoa tuhuma dhidi ya watu walio juu yake basi hatakiwi kuishia kufanya hivyo tu; naomba kupendekeza kuwa mtu huyo au watu hao wanapotoa tuhuma hizo dhidi ya viongozi wao ni lazima waachie ngazi zao katika kupinga (resigning in protest). Hili ni muhimu katika kuyapa uzito tuhuma walizonazo lakini pia katika kuhakikisha kuwa wanachotuhumu ni kizito mno.

Hivi juzi kikundi cha watu kimejitokeza kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wa juu wa CDM na kwa tuhuma ambazo kwa tunaofuatilia siasa za nchi yetu tunajua si ngeni sana. Sidhani kama kuna lolote ambalo limesemwa sasa ambalo hatujalisikia huko nyuma. Tuhuma za ukabila, ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka n.k dhidi ya viongozi wa juu wa CDM zimeshatolewa huko nyuma na mara kadhaa zimeshajibiwa. Hata hivyo inaonekana haziondoki. Haziondoki kwa sababu ni za kweli au haziondoki kwa sababu wanaozitoa wanazirudia mara kwa mara ili ziaminike kuwa ni kweli.

Kuna msemo kuwa "tuhuma peke yake hazitoshi; isipokuwa penye ushahidi". Ni rahisi kutoa tuhuma dhidi ya mtu yeyote na zinaweza kuwa maneno yote mazuri na ukali wake lakini kinachoangaliwa ni ushahidi. Ushahidi ambao hauna majibu.

Waliotoa tuhuma hizi kama nilivyosema kwenye lile sakata la Zitto na wengine ni kuwa ukishatoa tuhuma nzito hivi hadharani ni lazima ujiuzulu nafasi zako. Tuchukulie tu kuwa waliotoa tuhuma kweli ni viongozi wenye vyeo walivyovitaja; kwamba ni viongozi wa ngazi mbalimbali na wajumbe wa vikao halali vya chama. Sasa kutoa tuhuma hizi dhidi ya viongozi wao wa taifa hakuwezi kwenda hivi hivi isipokuwa ni lazima viendane na kujiuzulu nafasi zao. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CDM Bw. Said Arfi alifanya hivyo; hakutoa tu tuhuma bali alitoa na kujiuzulu nafasi yake. Wengine ni lazima wafanye hivyo hivyo kwa sababu kubwa mbili.

Kwanza, hawawezi tena kufanya kazi chini ya viongozi wa kitaifa ambao wanaendelea na madaraka yao. Hivi kweli kuna Waziri anaweza kutoa tuhuma dhidi ya Rais halafu akataka kuendelea kuwa Waziri kwenye serikali ile ile? Kwamba asimame Waziri aseme Rais ni mdini, anampendelea mke na watoto wake, na anaendeleza huko kwao zaidi kuliko kwingine halafu Waziri huyo huyo aendelee kukaa na kutumika kwenye Serikali ya rais yule yule?

Labda mfano wa Waziri si mzuri sana; vipi kama Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya au hata Mkurugenzi wa Halmashauri fulani; anaweza kweli kumtuhumu Waziri aliye juu yake au Rais kwa tuhuma nzito kama hizi na bado akataka kuendelea kushikilia nafasi ile ile? Ati akaenda mahakamani kusema mahakama imlinde asichukuliwe hatua na viongozi wa juu yake?

Ndio maana kwa mfano, ninaamini Kosa kubwa la aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kuhusiana na Richmond - ukiondoa kuingilia mchakato wa tenda na kutangaza hali ya dharura - ni yeye kutokujiuzulu pale alipotoa ushauri wa kutowapa Richmond tenda. Lowassa alitakiwa kwenye jambo zito kama lile kutoa maoni yake na kama amekuwa overruled na Rais basi apeleke barua ya kujiuzulu kwa Rais siku iliyofuatia ili kuhakikisha kuwa alichosema anakiamini. Lakini yeye alitoa ushauri kwa Rais na anadai kuwa Ushauri huo ukakataliwa na akaendelea na mchakato ambao tayari aliupinga. Angejiuzulu kupinga Richmond kupewa Tenda - licha ya hali ya dharura - angekuwa shujaa.

La pili hata hivyo ni kuwa ukishavunja daraja la mahusiano kati yako na bosi wako huwezi kuendelea kufanya kazi chini yake. Hili ni rahisi sana kueleweka. Hivi leo Mwenyekiti wa CDM Taifa au Katibu Mkuu Taifa wakiamua kufanya mikutano au kutoa maelekezo kwenye maeneo ya hawa jamaa (tukiamini kuwa wanazo nafasi walizodai wanazo) ndugu hawa watakuja kwenye mikutano na kukubali kupewa maelekezo? Hivyo kujiuzulu kwao ni lazima ili kutoa nfasi ya kupatikana viongozi wengine ambao wataweza kufanya kazi na wakubwa hao. Hii ni kanuni ya kawaida sana.

Jambo la mwisho kuangalia hapa pia ni kuwa kwa vile mikutano mikuu ya chama hiki bado haijafanyika basi wale wenye tuhuma dhidi ya viongozi wa taifa wameendelea kupotoka kwa kutoa tuhuma hidi mbele ya vyombo vya habari. Hizi ni tuhuma nzito dhidi ya chama na kuna vyommbo vya juu zaidi vyenye kusimamia chama. Binafsi naamini kuwa yeyote mwenye tuhuma nzito dhidi ya Freeman Mbowe au Dr. Slaa mahali pake hasa pa kutoa tuhuma bila kutaka kukimbilia mahakamani ni kwenye vikao vya chama. Yapo mazingira ambayo yanaruhusu au yanahitaji mtu kukimbilia mahakamani lakini haiwezekani umtwange mtu ngumi na wakati anakukunja shati kukuuliza ukimbilie kwa mwenyekiti wa kijiji! Kama ulijua yupo mwenyekiti wa kijiji kwanini usiende huko kwanza?

Kwa vile tuhuma hizi zimekuwa zikirudiwa katika matoleo tofauti tofauti ni muhimu sana (it is imperative) kuwa mikutano na vyombo vya juu vya chama kutoa nafasi ya uhuru kabisa kwa watu wenye tuhuma hizo kuzitoa na kutoa ushahidi walio nao mbele ya vyombo hivyo na kutaka majibu yapatikane. Na endpao majibu yanapatikana na watu hao hawaridhiki na majibu hayo au hawayataki (maana mtu anaweza kujibiwa vizuri lakini asipende majibu) basi itabidi wajiuzulu nafasi zao bado. Kama watkaubali majibu na majibu yakatosheleza watu hao ni lazima wapewe nafasi ya kuomba radhi viongozi wao na chama na kutokana na uzito wa tuhuma hizo hatua fulani za kinidhamu dhidi yao zichukuliwe. Na wakikataa kuomba radhi ni lazima bado wajiuzulu.

Ni lazima tutengeneze mazoea na tabia mpya katika utendaji wetu wa vyama na taasisi mbalmbali. Vinginevyo, mtu atataka kusema analosema tu mbele ya waandishi wa habari ilimradi anasema lakini hataki kuachia nafasi zake. Ni lazima kuwe na matokeo katika tuhuma.

Huwezi kupingana na bosi wako hadharani tena kwenye mambo mazito halafu ukataka kuendelea kushikilia nafasi yako. Unaweza kupingana naye kwenye vikao halali bila kuwa na tatizo lakini ukishatokea hadharani na kurusha tuhuma huwezi kuendelea na nafasi hizo. Watu wasio na vyeo ndani ya vyama hivi wanaweza kutoa tuhuma zozote kwa mtu yeyote bila kuwa na wasiwasi isipokuwa kama wanaingia kwenye libel na defamation kwani hata huko ulinzi wake ni wa kiwango cha juu - huwezi kumtukana mtu au kumsingizia tu bila ushahidi ukajitetea kuwa ni "uhuru wa maoni".

MMM
 
Rekebisha heading yako haijakaa vema. Nilikuwa nakuamini sana hapo mwanzo ila kwa sasa uwezo wako wa kufikiri umeshuka kwa kiwango kkubwa. Ina maana kupingana na kiongozi wako ni kosa hata kama una hoja za msingi? Organization na leadership inayoruhusu challenge inapiga hatua kimaendeleo. Hata kwenye chama cha siasa, ikiwa kuna utamaduni wa kupingana kwa hoja na kuvumiliana, mambo yanaenda barabara. Najuamdhamira yako imelala wapi.mila nakushauri, think twice and thrice
 
Rekebisha heading yako haijakaa vema. Nilikuwa nakuamini sana hapo mwanzo ila kwa sasa uwezo wako wa kufikiri umeshuka kwa kiwango kkubwa. Ina maana kupingana na kiongozi wako ni kosa hata kama una hoja za msingi? Organization na leadership inayoruhusu challenge inapiga hatua kimaendeleo. Hata kwenye chama cha siasa, ikiwa kuna utamaduni wa kupingana kwa hoja na kuvumiliana, mambo yanaenda barabara. Najuamdhamira yako imelala wapi.mila nakushauri, think twice and thrice
Unajua kuna vikao halili vya vyama..ambavyo vina utaratibu wa kutoa mapendekezo na challange..lkn kuna kitu watanzania tunapoteza kwa kasi sana heshima na mtu kuwa honesty..sisi tunadhani kuwa na heshima na mtu au kiongozi..tunadhani ni udhaifu...lkn haya yote yatakuwepo vp kama watu wametumwa..?!
 
Naona tumaeshajisahau, na muda haujapita!
Tunarudi kwenye "Zidumu fikra za Mwenyekiti"

Udikteta unarudi kwa kasi!
Hakika Mkuu, kiongozi akishindwa kuvumilia challenge, mwisho wa siku anavaa gwanda la udikteta
 
Unajua kuna vikao halili vya vyama..ambavyo vina utaratibu wa kutoa mapendekezo na challange..lkn kuna kitu watanzania tunapoteza kwa kasi sana heshima na mtu kuwa honesty..sisi tunadhani kuwa na heshima na mtu au kiongozi..tunadhani ni udhaifu...lkn haya yote yatakuwepo vp kama watu wametumwa..?!
Kuna kitu wengi wamelishwa yamini. Yaani kila anayempinga kiongozi anaambiwa kuwa katumwa. Huu ni uhuni wa hali ya juu sana
 
Well said mwanakijiji, kwa ufupi viongozi wote wana matatizo kaktika maeneo yao. Yona anawekwa mbele alishatimuliwa Temeke na sasa wanatumika kwa kazi maalum.

Kanuni ya mtu akipingana na bosi wake ni lazima ajiuzulu ni kanuni ya kawaida kabisa duniani kote. Hawa siyo kwamba hawajui ila wanaagenda yao na wanalipwa kwayo. Wewe jiulize, wanafanya yote hayo kwa gharama ya nani? Mtu kutoka Tabora kuja Dsm anaishi hotel nzuri unadhani ni jambo la kawaida bila mfandhili. Kama hakuna ufadhili mtu huyu asingeweza kuja Dsm. Huu ni mchezo wa chama fulani kutafuta pa kutokea.

Ukweli ninaojua ni huu. Wanataka kuchafua chadema kwenye vyombo vya habari na wengine wameandaliwa wakafanye hivyo kwenye baraza kuu ili baada ya hapo wajiunge chama xx taarifa iandikwe kurasa za mbele za magazeti kuwa Chadema imegawanyika na nusu wameenda kwenye chama cha ...... Huu ni mkakati wa kundi mojawapo kubwa ndani ya ccm wakitumia chama x cha upinzani.
Niseme tu, tumeshawashtukia. Hadanganyiki mtu hapa.
 
Mimi najiuliza kwa kutoa tuhuma hewa nzito nao wanauchungu na cdm wanataka ichukue madaraka mwakani,ajabu.
 
rekebisha heading yako haijakaa vema. Nilikuwa nakuamini sana hapo mwanzo ila kwa sasa uwezo wako wa kufikiri umeshuka kwa kiwango kkubwa. Ina maana kupingana na kiongozi wako ni kosa hata kama una hoja za msingi? Organization na leadership inayoruhusu challenge inapiga hatua kimaendeleo. Hata kwenye chama cha siasa, ikiwa kuna utamaduni wa kupingana kwa hoja na kuvumiliana, mambo yanaenda barabara. Najuamdhamira yako imelala wapi.mila nakushauri, think twice and thrice

kila mtu anahaki ya kukosoa na kusifia vilevile,usukufikiri ccm peke ndiyo ina hatimiliki ya kusifiwa kamawewe umeona makosa mwenzio kaona usahihi wake.kanma ni kusoana kila taasisi inautaratibu wake ndani ya chama kama weli hao ni viongozi wa chadena na wako kweli kwenye nafasi nyeti kiasi hicho kwanini wanapiga mayowe hovyo,kama wao wanafanya hivyo na wanachama wa kawaida watafanyaje?.

Kiufupi wamekosa nidhamu ya uongozi na hawafai kuwa viongozi hata wa familia. Kwasababu siku wakinyimwa unyumba tu basi kijiji kizima kitajua.

Usitetee upumbavu hata kama unalipwa,inaonyesha ni kiasigani umeshikiwa akili.
 
Well said mwanakijiji, kwa ufupi viongozi wote wana matatizo kaktika maeneo yao. Yona anawekwa mbele alishatimuliwa Temeke na sasa wanatumika kwa kazi maalum.

Kanuni ya mtu akipingana na bosi wake ni lazima ajiuzulu ni kanuni ya kawaida kabisa duniani kote. Hawa siyo kwamba hawajui ila wanaagenda yao na wanalipwa kwayo.\

Wewe jiulize, wanafanya yote hayo kwa gharama ya nani? Mtu kutoka Tabora kuja Dsm anaishi hotel nzuri unadhani ni jambo la kawaida bila mfandhili. Kama hakuna ufadhili mtu huyu asingeweza kuja Dsm. Huu ni mchezo wa chama fulani kutafuta pa kutokea.
Ukweli ninaojua ni huu. Wanataka kuchafua chadema kwenye vyombo vya habari na wengine wameandaliwa wakafanye hivyo kwenye baraza kuu ili baada ya hapo taarifa isema kuwa Chadema imegawanyika na nusu wameenda kwenye chama cha ......
Niseme tu, tumeshawashtukia. Hadanganyiki mtu hapa.
Hivi siku hizi wewe umekuwa msemaji wa CHADEMA? Vipi nafasi ya Tumaini Makene? Na je kiongozi anapoonekana anaenda kinyume na misingi, taratibu, kanuni, sheria na katiba inayomuongoza mwisho wake unakuwa nini? Tatizo mnawafanya viongozi wenu kuwa miungu watu na kwa hali hiyo hawakosolewi.
 
kila mtu anahaki ya kukosoa na kusifia vilevile,usukufikiri ccm peke ndiyo ina hatimiliki ya kusifiwa kamawewe umeona makosa mwenzio kaona usahihi wake.kanma ni kusoana kila taasisi inautaratibu wake ndani ya chama kama weli hao ni viongozi wa chadena na wako kweli kwenye nafasi nyeti kiasi hicho kwanini wanapiga mayowe hovyo,kama wao wanafanya hivyo na wanachama wa kawaida watafanyaje?.

Kiufupi wamekosa nidhamu ya uongozi na hawafai kuwa viongozi hata wa familia. Kwasababu siku wakinyimwa unyumba tu basi kijiji kizima kitajua.

Usitetee upumbavu hata kama unalipwa,inaonyesha ni kiasigani umeshikiwa akili.
Mkuu, hata kwenye maisha ya kawaida, ukiona mke au mume wako anaanza kupeleka nje masuala ya chumbani basi ujue kuwa chumba akina amani au fursa ya kutoa yale ya moyoni inakosekana. Udikteta wamMbowe na Slaa unanifikisha kwenye kilele cha kuamini kuwa ndani ya CHADEMA kuna ombwe la demokrasia. Ndo maana jana nilianzisha uzi kuwa Nasikia Harufu Mbaya na Kali ndani ya CHADEMA
 
Mkuu huyu si MMKJJ tunayemfahamu, pengine ame outsource uandishi wake!


Hata Mao Dze Dong wa China, aliwahi kuwaambia vijana wake, kama uongozi wa chama unalega lega na kufanya yasiyo tarajiwa - "Bombard the Headquartes"
Nakubaliana na wewe Mkuu. Mzee Mwanakijiji siku hizi amekuwa kama Saed Kubenea ingawa najua kuwa wote hawa ni pro chadema
 
Rekebisha heading yako haijakaa vema. Nilikuwa nakuamini sana hapo mwanzo ila kwa sasa uwezo wako wa kufikiri umeshuka kwa kiwango kkubwa. Ina maana kupingana na kiongozi wako ni kosa hata kama una hoja za msingi? Organization na leadership inayoruhusu challenge inapiga hatua kimaendeleo. Hata kwenye chama cha siasa, ikiwa kuna utamaduni wa kupingana kwa hoja na kuvumiliana, mambo yanaenda barabara. Najuamdhamira yako imelala wapi.mila nakushauri, think twice and thrice

Umemwelewa kweli,naamini hujamwelewa?
 
Back
Top Bottom