Ukipata watoto wenye afya shukuru Mungu

Kwann asingezaa akiwa Chuo mbona Chuo watu kibao wanapata mimba Na wanazaa
Alipata shule nchi nyingine walikuwa mbali mbali na mazingira ya kule aliona kuzaa itamsumbua. Pia kuna wanaongoja harusi ya gauni leupe kwanza ndio wazae.
 
Mmhh jamanii inaumaaa watoto wote wawili wawe na matatizo....... Mwambie abebe wa tatu ilà chini ya uangalzi Wa daktari na amuombe mungu sana pia awaponye watoto wake
 
Thanks God it's Friday,

Jana nilikuwa na shost tunapita madukani, shost alikutana na shost yake ambae mimi simfahamu, mdada mzuri na yeye ametoka madukani si mnafahamu Mlimani City panavyokuwa busy jioni. Nilifahamishwa kwa mdada huyu baadae walipiga story mbili tatu na kuagana.

Basi shost ananipa story baadae kuwa yule dada alikuwa anafanya kazi bank, alikuwa supervisor flani hivi. Imefika 35 ndiyo anapata mchumba, mipango ya ndoa inaanza dada amepata redundancy kazini. Wamekaa na mchumba walishauriana pesa aliyolipwa akafanye Masters, harusi iliahirishwa. Dada amekwenda huko, shughuli za huku na kule mpaka anakuja kuolewa yuko 42.

Hapo mume ameshagonga 50, baada ya mwaka mmoja tu wa ndoa harusi imejibu na baby boy. Kwakuwa alichelewa basi alikuwa na speed si ya kawaida, baby ana miezi sita alikuwa mjamzito tayari. Baby alikuwa slow kidogo, basi alijifariji kwasababu amebebewa mimba mapema, mpaka anajifungua, baby hajaanza kuongea.

Mtoto wa pili amezaliwa pia ana matatizo kama ya kaka yake. Sasa hivi wana watoto wawili wote wana severe autism. Mkubwa ana miaka 5 mdogo miaka 4 wote bado wanatumia nappy, hawawezi kuongea na wanahitaji matunzo ya karibu masaa 24.

Umri Mkubwa Chanzo cha Watoto Wanaozaliwa Kuwa na Matatizo ya Akili

Uzalishaji wa mbegu za kiume katika korodani ya mwanadamu wakati anapokuwa mzee huongeza hatari ya watoto wenye matatizo ya kimaumbile.

Mamilioni ya seli zinazotolewa wakati wa uzalishaji wa mbegu hizo hutoa mbegu nyingi za kiume katika korodani.

Lakini utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza unaonyesha kwamba mbegu hizo humea uvimbe na kusababisha mbegu nyingi za kiume kuwa na kasoro.

Wataalam wamesema kuwa wanandoa wanapaswa kupata watoto mapema katika maisha yao.

Magonjwa kadhaa ikiwemo ugonjwa wa akili wa watoto pamoja na dhiki hutokea sana miongoni mwa akina baba walio na umri mkubwa kutokana na Uzalishaji wa mbegu za kiume zilizo na kasoro.

Na hatari kuu ya ugonjwa huo huwaathiri watoto wanne kati ya 200 hadi watano kati ya 200 kwa pamoja wakati baba anapopitisha umri wa miaka 50.

Utafiti huo, uliochapishwa katika chuo cha kitaifa cha sayansi, ulichunguza korodani 14 kutoka kwa wanaume walio kati ya umri wa miaka 39 hadi 90.

Viungo hivyo vilikuwa havina matatizo ya kiafya lakini viliondolewa kwa matatizo mengine.

Watafiti walichunguza ndani ya korodani hizo ili kujua ni maeneo yapi yanayotoa mbegu hizo za kiume.

Wachanganuzi wa DNA katika maeneo hayo yenye kasoro walibaini kwamba kuna uzalishaji wa mbegu zilizo na kasoro zilizosababishwa taratibu mbalimbali mwilini.

Zilihusishwa na saratani, lakini pia zilikuwa na jukumu la ukuaji na uzazi katika korodani.

Matatizo hayo ambayo huathiri watoto husababisha uzalishaji wa mbegu zaidi ambazo huenea na hivyobasi kusababisha kiasi kikubwa cha mbegu zilizo na kasoro.

Chanzo: BBC
 
Asante Mungu baba uliyejuu mbinguni mwenye mamlaka juu yetu wanadamu. Nakushukuru kwa kunipa watoto wenye afya njema na akili, msaidie huyu mama kwa imani yake ili watoto wake wapone baba. Amen
 
Umri Mkubwa Chanzo cha Watoto Wanaozaliwa Kuwa na Matatizo ya Akili

Uzalishaji wa mbegu za kiume katika korodani ya mwanadamu wakati anapokuwa mzee huongeza hatari ya watoto wenye matatizo ya kimaumbile.

Mamilioni ya seli zinazotolewa wakati wa uzalishaji wa mbegu hizo hutoa mbegu nyingi za kiume katika korodani.

Lakini utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza unaonyesha kwamba mbegu hizo humea uvimbe na kusababisha mbegu nyingi za kiume kuwa na kasoro.

Wataalam wamesema kuwa wanandoa wanapaswa kupata watoto mapema katika maisha yao.

Magonjwa kadhaa ikiwemo ugonjwa wa akili wa watoto pamoja na dhiki hutokea sana miongoni mwa akina baba walio na umri mkubwa kutokana na Uzalishaji wa mbegu za kiume zilizo na kasoro.

Na hatari kuu ya ugonjwa huo huwaathiri watoto wanne kati ya 200 hadi watano kati ya 200 kwa pamoja wakati baba anapopitisha umri wa miaka 50.

Utafiti huo, uliochapishwa katika chuo cha kitaifa cha sayansi, ulichunguza korodani 14 kutoka kwa wanaume walio kati ya umri wa miaka 39 hadi 90.

Viungo hivyo vilikuwa havina matatizo ya kiafya lakini viliondolewa kwa matatizo mengine.

Watafiti walichunguza ndani ya korodani hizo ili kujua ni maeneo yapi yanayotoa mbegu hizo za kiume.

Wachanganuzi wa DNA katika maeneo hayo yenye kasoro walibaini kwamba kuna uzalishaji wa mbegu zilizo na kasoro zilizosababishwa taratibu mbalimbali mwilini.

Zilihusishwa na saratani, lakini pia zilikuwa na jukumu la ukuaji na uzazi katika korodani.

Matatizo hayo ambayo huathiri watoto husababisha uzalishaji wa mbegu zaidi ambazo huenea na hivyobasi kusababisha kiasi kikubwa cha mbegu zilizo na kasoro.

Chanzo: BBC
Shukrani mkuu, hili ni bonge la shule.
 
Back
Top Bottom