Ukipata watoto wenye afya shukuru Mungu

Ukipata watoto wenye afya shukuru Mungu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Thanks God it's Friday,

Jana nilikuwa na shost tunapita madukani, shost alikutana na shost yake ambae mimi simfahamu, mdada mzuri na yeye ametoka madukani si mnafahamu Mlimani City panavyokuwa busy jioni. Nilifahamishwa kwa mdada huyu baadae walipiga story mbili tatu na kuagana.

Basi shost ananipa story baadae kuwa yule dada alikuwa anafanya kazi bank, alikuwa supervisor flani hivi. Imefika 35 ndiyo anapata mchumba, mipango ya ndoa inaanza dada amepata redundancy kazini. Wamekaa na mchumba walishauriana pesa aliyolipwa akafanye Masters, harusi iliahirishwa. Dada amekwenda huko, shughuli za huku na kule mpaka anakuja kuolewa yuko 42.

Hapo mume ameshagonga 50, baada ya mwaka mmoja tu wa ndoa harusi imejibu na baby boy. Kwakuwa alichelewa basi alikuwa na speed si ya kawaida, baby ana miezi sita alikuwa mjamzito tayari. Baby alikuwa slow kidogo, basi alijifariji kwasababu amebebewa mimba mapema, mpaka anajifungua, baby hajaanza kuongea.

Mtoto wa pili amezaliwa pia ana matatizo kama ya kaka yake. Sasa hivi wana watoto wawili wote wana severe autism. Mkubwa ana miaka 5 mdogo miaka 4 wote bado wanatumia nappy, hawawezi kuongea na wanahitaji matunzo ya karibu masaa 24.
 
Sky bwana, nimependa heading. Nashangaa contents haziendani, itakuwa umeenda msa..l..ni. Tunasubiri urudi.
 
Ngoja tusubiri Season 2 .[emoji32]
 
umri wa kuzaa unajulikana kabisa ukiahirirsha mambo ndo kama hayo
 
hivi sarah wa kwenye biblia alizaa mtoto akiwa na umri miaka mingapi vile!!???

ngojam kidogo ntarudi...............
 
Kama alipata ujauzito wakati mtoto wa kwanza ana miezi sita, basi haiwezekani wakapishana miaka mitano kwa mitatu
 
Thanks God it's Friday,

Jana nilikuwa na shost tunapita madukani, shost alikutana na shost yake ambae mimi simfahamu, mdada mzuri na yeye ametoka madukani si mnafahamu Mlimani City panavyokuwa busy jioni. Nilifahamishwa kwa mdada huyu baadae walipiga story mbili tatu na kuagana.

Basi shost ananipa story baadae kuwa yule dada alikuwa anafanya kazi bank, alikuwa supervisor flani hivi. Imefika 35 ndiyo anapata mchumba, mipango ya ndoa inaanza dada amepata redundancy kazini. Wamekaa na mchumba walishauriana pesa aliyolipwa akafanye Masters, harusi iliahirishwa. Dada amekwenda huko, shughuli za huku na kule mpaka anakuja kuolewa yuko 42.

Hapo mume ameshagonga 50, baada ya mwaka mmoja tu wa ndoa harusi imejibu na baby boy. Kwakuwa alichelewa basi alikuwa na speed si ya kawaida, baby ana miezi sita alikuwa mjamzito tayari. Baby alikuwa slow kidogo, basi alijifariji kwasababu amebebewa mimba mapema, mpaka anajifungua, baby hajaanza kuongea.

Mtoto wa pili amezaliwa pia ana matatizo kama ya kaka yake. Sasa hivi wana watoto wawili wote wana severe autism. Mkubwa ana miaka 5 mdogo miaka 4 wote bado wanatumia nappy, hawawezi kuongea na wanahitaji matunzo ya karibu masaa 24.
Autism ndio tatizo gani kiafya??
 
Nakumbuka mtoto wa dada yangu mmoja alikuwa hawezi kutembea. Mpaka kafika miaka minne akafanyiwa dawa (sijui dawa gani). Lakini nakumbuka akipigwa mfagio wa miguu kila wakati hio ndio ilikuwa sharti la dawa. Kufika miaka sita akaanza kutembea hivi sasa yupo mid 20s anatembea vizuri tu. Na maisha yake yapo safi kabisa, Ushauri wangu hao watoto wanahitaji kufanyiwa dawa.
 
Back
Top Bottom