Ukipata ajali na basi la abiria lazima ulipwe na Bima kama ni majeruhi

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Abiria anapaswa kuandika barua kwenda kampuni husika ya bima iliyokatiwa hilo Bus. Katika barua hiyo aambatanishe vifuatavyo

1.TIKETI YA SAFARI.
2.CHETI CHA MATIBABU YA HOSPITALI.
3. FOMU YA POLISI (PF 3).
4. MCHANGANUO WA GARAMA ALIZOINGIA.
5. PF 90.
6. PF115

7. TIKETI YAKE kama bado anayo (kama imepotea kutokana na mazingira ya ajali itaeleweka haina shida sana).
Cha muhimu ni kwamba kama hakuzidiwa sana basi ahakikishe yeye mwenywe kuwa jina lake lipo kwenye orodha ya majina ya polisi ya majeruhi kwa kutaja majina yake yote kamili.
8. Cheti cha kifo, ikiwa unadai kwa niaba ya ndugu aliyefariki katika ajali.
9. Hakikisha unaziwasilisha nyaraka hizi kwenye ofisi ya bima husika.

KUMBUKA: Utalipwa tu iwapo,ulipanda magari ambayo yaliyoruhusiwa kubeba abiria tu ndiyo (PSV) yaani Passenger Service Vehicles kama vile mabasi ya abiria,daladala, na taxi zilizosajiliwa.

Pamoja na hayo tarajia kupigwa danadana na kuzungushwa sana na wadau husika, cha msingi komaaa kupigania hakiyako. Ulkiona hakuna msaada panda ngazi ya aliyeko juu yake anayekupiga chenga na kukuzunguka.
Kumbuka kujenga confidence na kujifanya unajua sheria na haki yako

NB: Kampuni ya bima ikikataa kulipa madai unayoona ni halali, wasilisha mgogoro wako katika ofisi za Msuluhishi wa Migoigoro ya Bima zilizopo PPF Tower Dar es salaam au ofisi ya Mamlaka ya Bima(TIRA) zilizpo nchi nzima
 
Hii ndio jf ninayoisikiaga na hawa ndio the real members wake, akina kiduku lilo ni wanafacebook walioivamia jamiiforums.

Screenshot_20200414-124757~2.jpg
 
Watu wengi hawajui umuhimu wa tiketi mbali na kulipwa ukipata ajali.inaweza kuokoa kwenye janga la kusingiziwa
 
Back
Top Bottom