Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,504
- 51,099
Hili ni jambo la ajabu sana. Yaani ukiongea na wana CCM tena wale wazito ndani ya chama, wanakwambia huu mkataba ni wa kipuuzi na kuwa sisi kama nchi tumepigwa.
Ila wakiwa public kwenye majukwaa wanapongeza mkataba, wanampongeza Samia.
Ukiwauliza kwanini, wanakujibu wazi, wanakwambia kuwa hata Rais Samia mwenyewe na Spika Tulia wanajua kuwa huu mkataba ni mbovu na tumepigwa. Ila wanakomaa tu kulinda nafasi zao za kisiasa wasije kuumbuka baada ya kulikoroga.
Wanasema sasa kama Rais Samia mwenyewe na Spika wanajua kuwa huu mkataba ni famba kwa nini sisi tujitie kimbelembele kuupinga waziwazi wakati hata wakubwa ukweli wanaujua?
Hapa ndipo tulipofika ndugu zangu. CCM inachokifanya kwa sasa ni kulinda chama chao kisianguke. Yaani kwao ni bora bandari ikaenda kwa mwarabu kwa mkataba mbovu kama huu na sovereignity ya nchi ikawa matatani ilimradi tu kulinda chama na rais wasianguke. Kwao madaraka ni muhimu zaidi kuliko nchi!.