Ukionewa ni sahihi kushika bunduki na kuingia mtaani kuua watu?

sijawahi kuonewa.... ila nikionewa... mamaaake nakuwa zaid ya hamza....!"(nawaza tu kwa sauti")
 
Hamza mwenyewe kabla ya kutandikwa risasi kasema anauwa kwasababu ya jihad na kajitoa muhanga kwaajili ya siro anauwa waislam Sasa sijui ni waislam gan wameuliwa na siro
Hamza ni mtoto wa hovyo sana
 
I am not afraid of standing up in what I believe in even if I am standing alone!! Hamza alichokifanya sio sawa. Kilicho wakosha watu ni vile amesema anawaua polisi na kwakuwa watu wengi mna hasira na matendo ya polisi basi mioyo yenu imesuuzika lakini hamjui mnaandaa balaa gani lijalo.

Siku Atatokea mtu atalipua kadamnasi atasema pale palikua na polisi wawili alikua anawalenga. Ila kwakuwa mmesikia neno polisi mtaendelea kufurahia.
Na mnao sema watu wote wanamuongelea vizuri Hamza sijakataa sio mtu mwema. Lakini moyo wa mtu ni kichaka! Kwani hizi nchi wanazopigana wenyewe kwa wenyewe hao watu hawana upendo huko wanapoishi?? Watu wanaishi miaka hata 40 kwenye jamii zao na kuwa watu wema na siku akifanya jambo wote mnashangaa!! Hakuna cha kumsifu hamza.

Tukisema watu wote walioonewa na polisi walipize nyie ni mashahidi mnajua nani ataanza. Kuna mtu amebomolewa majengo yake, akaunti zake zimefungwa, lakini hatujaskia ameua polisi. Endeleeni kuwapa kichwa wauaji. Siku watakuja na tukio walipue nyumba za ibada au city malls kwa kisingizio kuwa mlikua na mapolisi humo ndani na ndo waliokua wanalengwa. Endeleeni kusifia.

Alafu mtu mwenye hasira na ambae sio gaidi zile silaha alijifunzia wapi? AK 47 tukupe saizi hapo utaikoki vizuri na kuirusha rusha vile confidently. Watanzania hatujui camouflage mi nasema endeleeni kuwapa vichwa wauaji. Watawafurahisha.

There is no Justification in this situation.
 
Usitudanganye wewe. Mimi nimepita JKT. Huyo mtoto wa miaka 29 au 30 alikwenda JKT lini? JKT ilishafutwa kipindi hicho. Aliirudisha tu JPM enzi zake. Huyo ni Gaidi, huo ndio ukweli. Nimetumia sana SMG na AK47 nikiwa Mafinga Mkuu. Enzi zile za kujibu wa sheria.
 
Chifu,ukifika kwenye point of no return, huwezi ogopa chochote,liwalo na liwe, ogopa Sana hasira.
Sawa, ni hasira, lakini hasira haziwezi kukufanya ujue kutumia silaha ambayo haujui kutumia. Yule ni mtu aliekuwa amefundishwa kutumia hizo silaha. Kutumia pistol ni sawa, lakini kwa SMG, hiyo haifundishwi kwa watu wa kawaida.
 
UZI hauna uzito, labda ungeuweka hivi." Ni nini Hamza kaonewa mpaka kubeba bunduki"?
 
Akili itakavyokutuma baada ya kuonewa ndo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…