Ukiona mtu ananunua papai ujue hana nyumba

Ukiona mtu ananunua papai ujue hana nyumba

Vitu kama papai,embe,parachichi,passion in short matunda yote yenye mbegu haihitajiki kupanda wala kununua miche yake,yale yale unayonunua mbegu zake tenga sehemu kwenye ardhi yako zirushe.

Juzi jumapili nilikuwa nakagua home nina mapapai itabidi nipunguze miche,nina maembe miche sita (hii nitahamishia baadhi sehemu nyengine) nina miparachichi mitatu na passion nimeona moja,pia ipo miche sijajua kama ni ya limao au chungwa.
 
Anashamba la mipapai na kapanga
Kupanga hakukuzuii kuwa na bustani kama eneo lipo

Nakumbuka kuna nyumba moja niliwahi kupanga 2014 nilipanda bustani na miche mbali mbali ya matunda bila kujali ni kwangu ama nimepanga

Nashukuru yule mzee alivitunza mwaka juzi nilibahatika kutembelea ule mkoa na nikakuta baadhi ya Miti ikiwa bado ina uhai wake....
 
Wachache watakuelewa... Kila binadamu anastahili kuishi mazingira kama hayo na kushi mjini isiwe kisingizio
Mkuu,

Acha maisha ya kutaka kumpangia kila mtu.

Wale watu wanaopenda kuishi kwenye ma apartment katikati mjini ghorofa ya kumi nao unataka wapande mipapai ghorofani kule?
 
Kwa hivi viwanja vya 20x15 tunavyonunua hapa Mjini sio rahisi kupata space ya kupanda miti ya matunda

Ndiyo maana kama una nafasi inashauriwa ununue eneo kubwa hata kama ni ekari 3 nje ya Mji huko na kisha kuweza kujenga nyumba nzuri na kupata space ya kupanda miti ya matunda na kivuli

Shukrani sana Kwa kutushauri Mkuu 🙏🙏
 
Hakuna raha kama kukaa kwako ,matunda ya Kila aina yamejaa ndani ,mbogamboga na nk
Ni kweli ni raha sana , utatuaje mtu kapanga ila anazo nyumba kadhaa , na zina kila kitu , ila yupo kapanga sehemu fulani kwa sababu zake maalumu na papai ananunua tu?
 
Ni kweli ni raha sana , utatuaje mtu kapanga ila anazo nyumba kadhaa , na zina kila kitu , ila yupo kapanga sehemu fulani kwa sababu zake maalumu na papai ananunua tu?
Dhaumuni la mtoa hoja sio kazodoa watu wanaopanga ila kaonesha jinsi gani tunavyotakiwa kufanya tukiwa nyumbani Ili kuepuka manunuzi ya vitu rahisi ambavyo Tunaweza kufanya home.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom