Mom Fay
JF-Expert Member
- Feb 21, 2014
- 1,059
- 316
Habari za mda huu wanaJF, ni matumaini yangu mu wazima. Natumai ni usiku tulivu kwenu hasa kwa wale wapendanao mliopo pamoja mda huu hata mliotenganishwa na umbali tu!! Wote ni wapenzi na mapenzi ni hisia zilizopo ndani yenu.
Leo ningependa kuongelea kitu kuridhika ndani ya mahusiano yenu. Napoongelea kuridhika nagusa sehemu nyingi na mbalimbali. Lakini muhimu ni hapa.
Tunapoamua kuingia na kutulia katika mahusiano flani ni vyema kuridhika na mpenzi wako. Kuwa mke na mme ni hatua kubwa sana kimahusiano.
Ewe Mwanamke ridhika na mmeo, uwezo wake sio wa kuleta nyama kila siku, mboga saba saba kila mchana na usiku, kila style ya nywele, nguo, viatu usipitwe!!
Kisa fulani anatembelea verrosa basi na we unataka!! na ilhali yeye mwenyewe hata baiskeli hana! Jamani wapenzi, kumbuka huyo ni mmeo au ni mwanaume ulie na malengo nae jitahidi kumuelewa mazingira yake na msome vizuri.
Mwanaume haitaji kukwazwa kwa vitu vidogo vidogo,hata wakati mwingine kuwa mpole kupisha jambajamba lipite, hata kama unakwazika zuia hasira kwani wote ni binadamu, badala ya kupoteza mda mkibishana na kuumizana vichwa kwa ugomvi usio na maana ni bora ukasimama nyuma yake ukamsaidia unapohisi amekwama!!
Pesa zinatafitwa mkishirikiana na mkaelewana mtafika mbali. Mwanaume pia ,nyinyi ni watu muhimu sana kwetu mnapoamua kuwa na sisi sio siri mnafanya uamuzi wa busara sana hadi hatua ya kutuweka ndani!!
Kwenu ntakugusia swala la ukweli na uwazi!! Wengine mnayakaribisha mazito wenyewe kwa kuwaonyesha wenzi wenu mna uwezo wa kuwafanyia makubwa wakati ukweli mnapumulia mipira.
Swala la ukweli zuri sana kukiwa na uelewa pia.
MME: mmh mke wangu leo sio siri hali ya mfuko wangu mbaya!! Hela iliyopo ni ya mkate tu!!
MKE: usijali baba watoto wangu, ntachemsha chai tu na mkate tutakula tutalala..
Kwa upendo na tabasamu...maisha yanakuwa mazuri,upendo,uaminifu,ukweli na uwazi,uvumilivu na mengine mengi. Hakika hata mungu atawabariki.
Nawapenda wote na nawatakia mahusiano mema