Ukiona Dalili hizi Kwenye Simu Yako, Jua Kuwa Uko "hacked"

Hapo mbona kuna icon ya "on going call" kwamba wakati unapiga hii screenshot kuna simu ulikuwa unaongea nayo au unapiga, kama ni hivyo basi hiyo ndio sababu ya kuonekana kwa hiyo icon ya kijani
Ukisoma maelekezo aliyotoa kwenye kipengele cha pili ndicho kinaelezea hivyo.... Unless kuwa sijamwelewa vizuri kwa alichomaanisha.
 
Habari mwanajamvi, najua umekuwa na siku ndefu sana ya kikazi maofisini au biasharani, ama mwingine unasoma uzi huu ukiwa kazini, piga kazi, kazi ni kipimo cha utu.

Kabla sijaendelea mbali naomba nisema kwamba mimi ni fundi simu, kazi hii imefanya nijifunze mambo mengi kupitia changamoto za watumiaji wa simu. Ni kweli kwamba teknolojia imekua sana, na katika kukua huko kuna faida na hasara zake. Ukiachilia mbali kukua huko na faida na hasara zake, pia kuna watu wasaka taarifa za watu wengine kupitia teknolojia. Baada ya kuona changamoto kadhaa kwa watu leo nimeamua nisemezane na wewe kidogo juu ya UDUKUZI na utajuaje kama UMEDUKULIWA. Twende sawa

Mdukuaji mara zote kuna vitu anakuwa anavilenga ili aweze kupata anachokitaka toka kwako. Kuna aina nyingi za udukuzi lakini hapa sitaongelea aina hizo bali nitaongelea "namna ya kujua kama simu yako imedukuliwa".
Mdukuzi anadukua simu yako kwa kuweka spy app kwenye simu yako bila wewe kujua, anaweza kukushawishi kwa kukutumia link flani yenye maelezo fulani kwamba kuna offer na ili upate offer hiyo uinstall app flani, au uguse link flani, ndugu yangu kuwa makini, mdukuzi anaweza chukua udhibiti wa simu yako sekunde tu kama ni mtu wa tamaa na kushawishika. Watu wa android wapo kwenye risk zaidi maana zinaruhusu kudownload apps toka nje ya google playstore, iOS nao hawako salama lakini angalau huko kuna process ndefu mpaka mtu kumdukua.

Njia ya pili ni watu wetu wa karibu ambao wana access na simu zetu, mke au mume akitaka kukudukua basi ataweka hiyo app kisha ataweza pata taarifa zako zoteee.

Ni Taarifa Gani Mdukuzi Anazipata Ukidukuliwa?
  1. Sms zako zote
  2. simu zinazotoka na kuingia
  3. location yako
  4. contacts zako
  5. picha na files zako
  6. anaweza kupiga picha bila wewe kujua
  7. anaweza kurekodi maongezi yako ya simu au live bila wewe kujua
  8. anaweza futa vitu vyako
  9. anaweza kubadilishia password ya simu yako
  10. anaweza kudhibiti baadhi ya vitu, kwa mfano anaweza kukuzuia settings za location usiweze kuzima n.k
Sasa katika yote hayo utajuaje kama simu yako imedukuliwa?
Kila simu ina mfumo wa ulinzi ambao unazuia kuinstall apps ambazo hazijatoka google apps store, na ikitokea spy apps imekuwa installed maanake ulinzi ulitolewa ili apps husika iwekwe. Kwenye simu ambayo nimetumia kama mfano neno "Installation Sources" limetumika lakini kwenye simu zingine wanatumia nene "Install From Unknown Source". Ukiangalia kwenye picha uataona kwamba mimi nimeruhusa kuinstall apps toka chrome na xender, nje ya hapo apps haziwezi kuingia, simu itakutaka ufungue ulinzi wake ili apps iweze kuingia. so, hapa angalia kwenye settings>Passwords and security>Installation sources(mpangilio wa settings unatofautiana ila concept ni moja) kisha angalia sehemu zinazopitisha hizo apps.
View attachment 2551635

2. Kwa simu kuanzia android ya 9, ukifungua camera au recorder kwa mfano, kwa juu kulia itakuletea kadoti kadogo ka kijani ambako kanakuonesha kuwa kuna kitu kinaendelea. Kwa hiyo kama hutumia kama kamera, location au recorder wakati huo na kadoti ka kijani kakaonekana weka wasiwasi kwamba huenda umedukuliwa na mtu ana access location yako au kamera yako au recorder ya kwenye simu yako. Na uzuri ni kwamba ukiswip kuja chini utaona ni kitu gani kinatumia camera, recorder au location yako.
Kama mtu ana access camera ukiswip utaona kitufe kwenye kijani kama ianavyonekana kwenye picha hapa chini.
View attachment 2551657

Kama mtu anakurecord utaona kitufe cha mic kwenye kijani kama inavyoonekana hapa kwenye picha
View attachment 2551664
Halikadhalika, kama mtu ana access location yako yako utaona location ina blink juu kwenye status bar yako kuonesha kuwa "you are being tracked"
Ndugu mwanajamvi, kujua hivyo vyote unatakiwa kuwa makini, maana mdukuzi anaweza akawa anafanya kazi yake wakati ambao wewe hutumii simu yako.

3. Kuscan apps zako kwa kutumia ant virus. Jiwekee utaratibu wa kuscan apss zako mara kwa mara. ant virus itakwamia na kukuonesha application ambayo ni suspicious na kama huitambui application hiyo itoe haraka, kama huwezi omba usaidizi maana wadukuzi wengine wanaenda mbali zaidi kwa kuzuia usiweze kutoa apps husika aidha kwa password au kukunyima access za administrator kwenye simu upande wa security, yote hayo yanafanywa automatic na apps maana apps inakuwa na kirusi kiiba taarifa.

4. Kagua apps zako unazo zitumia. Wote tunajua kuwa kuna apps ambazo huja na simu na hata hatuzitumii laikin kuna apps ambazo sisi tunaziweka, lakini ukiona apps ambayo haikuja na simu na wewe haukuiweka, washa full huenda umedukuliwa.

Baada ya kuandika dalili hizo nne, nitoe mapendekezo yangu hapa chini.
  1. download apps zako toka google playstore au app store tu
  2. achana na mods app kama vile GBwhatsapp, una hatarisha usalama wako. Tumia apps official tu.
  3. Usiguse link yoyote ambayo umetumiwa na hujui kazi kazi yake, kabla ya kugusa hakikisha umepewa maelezo ya kina na jiridhishe pia, na usiwe na tamaa, wengi wamedakwa kwa tamaa zao.
  4. kuduka simu ya mtu ni makosa kwa sheria ya Tanzania, hivyo jiepushe na kudukua simu ya mwenza wako wako maana inaweza pelekea ukapata kesi ya makosa ya kimtandao
  5. nunua simu official kila inapobidi (hasa samsung) zipo simu nyingi mtaani ziko "uchi" hazina ulinzi wowote kiasi kwamba mtu anaweza ingia kwenye simu yako na kufanya chochote.
  6. jiepushe na wi-fi za bure zingine ni mitego, ukiunga mtu anaweza pata access ya simu yako, pale juu nimekwambia kuna aina nyingi za udukuzi.
Ndugu zangu, hayo ndo maoni yangu, kama kuna uanchojua zaidi ya hayo tujuzane hapa ili tusaidie na wengine taarifa zao zibaki salama.

Naomba kuwasilisha.
Well
 
Back
Top Bottom