Ukioa kwenye familia yenye wazazi wenye maadili mabovu binti yao anaweza kuwa tofauti?

kilamba lamba

JF-Expert Member
May 27, 2020
367
679
Natumai ni wazima kabisa, nina jambo moja ningependa kushauriwa hapa, naamin kuna watu wenye uzoefu na hili na kujua ufumbuzi wake kiujumla. Nakuomba usipite bila kutoa ushauri wako.

Je, kuna mtu yoyote ambaye katika maamuzi ya kuoa aliamua kuoa mwanamke ambaye ilionekana kwenye familia yake kama pana maadili mabovu (mama) na akaamua kuoa na huyo mwanamke asiwe amefata tabia za mama yake kwa kipindi walichoishi wote? Kwa mfano kama mama aliolewa zaidi ya mara moja inaweza ikamuathiri na watoto wake wa kike?

Je, sifa za mama zinaweza zisiwe kipaumbele kwenye maisha ya watoto zake wakike (wasiige lifrstyle ya mama yao)?

Wenye uzoefu na hili usipite bila kutoa ushauri wowote.
 
Kila mtu na tabia yake

Mimi mke wangu tabia zake hafanani na mama yake wala familia yake (eg wadogo zake na dada zake)

Tabia ni ya mtu binafsi (ingawa mazingira na malezi.wazazi yanachangia) but usimjudge mwanamke kumuangalia mama yake au familia yake. Muangalie yeye kama yeye.

Ukiangalia wazazi unakua na bias, kuna watoto wa wachungaji ila hovyo kabisa
 
Mkuu na kuambia tuu mtoto wa nyoka ni nyoka ,

Haijalishi lini ataanza kujifunza kukung'ata kisigino ila ipo siku atakung'ata tuu.

Tabia ya mama yake aliyoishi na mumewe (baba yake) ndiyo tabia halisi ya mtoto wake wakike utakaekuja kuishi nae,

Ukijumuisha na tabia zako ndiyo utapata mtazamo wa maisha yako ya ndoa yatakavyo kua pamoja na huyo bidada.

KWA ULICHOKIELEZA HAPO JUU HAKIKISHA UNA MOYO MGUMU SANA
 
Kuna mchungaji aliwahi kusema, "ukitaka kumuoa binti, muone mama yake" Mara nyingi vile binti atakavyokuwa ni kutokana na kile anachokiona baina ya wazazi wake. Tukubali au tukatae, tabia za watoto wengi ni urithi kutoka kwa wazazi. Kama mama anaamini kwenye ushirikina, halafu ukaoa binti yake, basi jua tu ipo siku na wewe utakuwa victim.

Hapa nilipo nimesitisha ndoa na binti wa Kichagga, hivi karibuni nimefuma mawasiliano yake na mganga wa kienyeji akiwashughulikia wenzie kazini, sasa nikasema nikimuoa huyu si hata mimi ipo siku nitarogwa!?
 
Natumai ni wazima kabisa, nina jambo moja ningependa kushauriwa hapa, naamin kuna watu wenye uzoefu na hili na kujua ufumbuzi wake kiujumla. Nakuomba usipite bila kutoa ushauri wako.

Je, kuna mtu yoyote ambaye katika maamuzi ya kuoa aliamua kuoa mwanamke ambaye ilionekana kwenye familia yake kama pana maadili mabovu (mama) na akaamua kuoa na huyo mwanamke asiwe amefata tabia za mama yake kwa kipindi walichoishi wote? Kwa mfano kama mama aliolewa zaidi ya mara moja inaweza ikamuathiri na watoto wake wa kike?

Je, sifa za mama zinaweza zisiwe kipaumbele kwenye maisha ya watoto zake wakike (wasiige lifrstyle ya mama yao)?

Wenye uzoefu na hili usipite bila kutoa ushauri wowote.
Ndio familia hasa mama huathiri kwa kiasi kikubwa. Ushauri wangu kwanza angalia muhusika mwenyewe mambo yake na misimamo yake ilivyo maana unawezakuta mfano mama ni muasherati ila bintiye akawa tofauti kabisa, au familia/mama inajihusisha na kuamini katika mambo ya kishirikina/uchawi nk ila bintiye akawa tofauti kabisa na imani kama izo au kumbe binti ilimbidi kushiriki hayo mambo kwa shinikizo tu la wazazi/mama au fimilia, pia kuna external factors nyingi tuu hivyo kumuhukumu binti 100% kwa kumtumia mama yake ni sawa na kumuonea tuu. cha msingi fanya udadisi na maswali ya hapa na pale kujua misimamo yake yeye kama yeye na mambo yake.

Kumbuka pia kuna NEEMA YA MUNGU
kwani hujawahi sikia mpagani kamzaa padre 😂
 
Tabia ya mtu ni kama ngozi... Hata ukijichubua, itafika kipindi hiyo itarejea kwenye rangi yake halisi.

Mtu akipenda hutaona makucha yake. Mkichokana sasa, utaona naye ni walewale.

Kwanza kila mtu ana tabia mbaya, angalia utazoweza kumudu baada ya honeymoon.
 
Hanii...☹️
Tafrani...😑
Huonekani...😊
Hannniiiiiii.......😝
 
Back
Top Bottom