Tunafeli sana eneo la ujenzi wa familia bora

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,962
Katika jambo ambalo linarudisha nyuma sana maendeleo sio tu binafsi ya mtu , bali ya familia, jamii na taifa zima basi ni kukosekana kwa utaratibu mzuri wa kuishi ndani ya familia.

Familia ni taasisi ya kwanza na muhimu na NDOA imara ndio msingi wa familia bora ambayo ndio huleta matokeo mazuri katika swala la maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Leo naomba nijikite kuzungumzia familia na namna mifumo yake inatakiwa kuwa na si vinginevyo.

Familia ni muunganiko wa Mwanaume na mwanamke ambao wamependana ya dhati ya moyo na wamechagua kushirikiana na kuishi pamoja kama mwili m'moja bila kubaguana na kupeana kipaumbele katika umoja wao.

Sasa tujikite kwenye namna ya kuishi ndani ya familia. Familia inafanya kazi kwa namna ile ile taasisi zinafanya kazi. Taasisi zote unazoziona kwenye hii Dunia zimecopy mfumo wa familia yaani baba kiongozi, mama msaidizi na watoto na ndugu kama subordinates au watendaji wa taasisi katika vitengo mbali mbali.

Sasa inapotokea kitengo kimoja kinaleta uzembe aidha wa makusudi au kwa kusababishiwa then hii italeta hitilafu katika mfumo mzima wa familia na kusababisha utendaji wa hovyo na matokeo mabovu.

Tukianza ni wajibu wa mama wa familia kuhakikisha kunakuwapo na hifadhi ya chakula cha kutosha kwajiri ya familia yake bila kuwa na mapungufu. Sukari hununuliwa kiwango fulani ya jumla lets say kilo 35 then imebakia kilo 4 ,mama unatakiwa mapema sana kumjulisha baba huku ukibadili matumizi ya sukari kutoka ya kawaida kwenda ya dharula ili sukari hii iweze kusindikiza bajeti kwa muda mchache uliosalia hadi kikao kipya cha bajeti kitakapoketiwa na manunuzi mapya yatakapofanyika. Hii itaenda sambamba na kuwajulisha watoto kuacha uharibifu na ufujaji na kuweka adhabu kali na maonyo pale wanapokiuka hiyo amri.

The same goes kwa vitu kama umeme, mchele, matunda, vinywaji, na kadhalika ndani ya nyumba. Mama anapokuwa makini na rasilimali ndani ya familia na kujiepusha kwanza yeye mwenyewe kuwa mfujaji na kuwadhibiti watoto kuwa wafujaji hiyo itasaidia sana kuongeza mapato na kuimarisha mahusiano mazuri na mumewe ambaye anatafuta kwaajiri ya familia yake. Imagine, kila mwezi mwanaume kajiwekea matumizi ya familia ni laki 5. Lakini kutokana na control nzuri ya mkewe baadhi ya vitu vitavuka muda wa bajet na kukutana na bajeti mpya na matokeo yake badala ya kulipa 5 safari hii unakuta mahitaji ni laki 3, laki mbili inakuwa saved. Sasa katika mazingira hayo kwann mwanaume asione amekutana na mke jembe. Hiyo laki mbili itakaa kwenye akiba na kufanya mambo mengine ya familia na kupunguza mzigo wa kifedha.

Sasa kinyume chake, mke akiwa hazingatii usimamizi madhubuti wa bajeti ya familia na kushiriki ufujaji wa rasilimali za familia mfano anagawa vitu, jirani kaja amempa sukari nusu, mara chumvi pakti moja, mara kampa nyanya, mara kampa viberiti, mara amekuja ndugu kajichotea mchele store, yote hii in the name of roho nzuri, huu msalaba atakuja ubeba ni mume wako na wewe na watoto. Ewe mwanamke Usiruhusu ajizi ya mwingine ielemee familia yako na mume wako. WANAUME TUNACHUKIA SANA WANAWAKE WAFUJAJI WA RASILIMALI. Huwa hatusemi ila moyoni tunaanza kuwachukia na ndio unaanza ona tunapunguza kutoa matumizi mnasema tunabadilika ni ninyi ndio mnatubadilisha tabia.

Pesa ni ngumu sana kupatikana nyakati hizi sababu uhitaji wake unaongezeka kadiri gharama za maisha zinavyozidi kupanda kila uchao sasa inapotokea mwanaume anajitoa kutafuta kwaajiri ya familia , kufuja na kutompa ushirikiano eneo la bajeti ni sawa na kumtukana matusi ya dharau na ya nguoni.

Sasa tuwarejee watoto. Hawa jamaa usipokuwa nao makini ndio wanaoongoza kufilisi familia sababu wanamahitaji mengi sana ila hawalipii hata mia mbovu kuchangia. Sasa usipokuwa na usimamizi mzuri wa hawa viumbe maumivu yake yanazidi mara kumi ya kuwa na mke mpumbavu. Watoto ni baraka sana kwa wazazi kama watapitia malezi bora na kusimamia njia za utii na kuelewa. Ila ni nuksi kama hawatakaa kwenye mstari.

Tazamia mambo yafuatayo. Mtoto anatakiwa kujua anapiwasha vifaa vya umeme na kuacha vikitumika hovyo ikiwa yeye hayupo hapo mfano kawasha tv, feni, radio kwa wakati m'moja halafu yeye yupo chumbani huo ni uharibifu na wazazi ndio watabeba mzigo, hivyo akanywe na kukemewa hiyo tabia ikome na asichukulie mzaha mzaha. Hiyo tabia inachangia sana kuongeza gharama za bajeti ya famili.

Pia kuna mtumizi ya ufujaji mtoto anachukua unga wa ngano anachezea kufanya mazoezi ya kutengeneza keki, sijui cupcakes, sijui pancakes mwisho wa siku anaharibu unga na vitu vyenyewe haviliki vinatupwa kwenye Trashcan kama takataka. Sukari, unga wa ngano, maziwa, chumvi, gesi, umeme vimechezewa bila matokeo ya msingi. Hii ni tabia mbaya ya ufujaji na mtoto akemewe, kama anataka kujifunza kupika basi aombe mama yake amfundishe kipindi mama yupo jikoni anapika na sio muda wowote akijisikia yeye huku akiharibu stock ya vyakula.

Watoto wanawajibika kutunza mali za wazazi sababu zipo kwaajiri ya kuwasitiri wao pia. Kuna tabia za uharibifu wa vifaa vya ndani,kuvunja viombo, kuchora kuta za nyumba,kutoboa nyavu za dirisha. Hizi ni tabia mbaya za kukemea sababu zikichekewa huwa zinachangia uchakavu wa mali na kuleta gharama ya matengenezo ambayo haikutakuwa kuwapo. Watoto ni lazima watengenezewe mfumo wa kujitambua na kuwa makini na matendo yao.

Ni vema kutambua kuwa thamani ya familia ipo kwenye kushirikiana na kujitoa. Familia yoyote inayojengwa katika misingi hii huwa inajenga mfumo mzuri sana wa kuwa na mafanikio ya kila mwanafamilia siku za baadae watapoanza kujitegemea. Kinyume chake ni fedheha,mahangaiko na aibu katika maisha ya baadae.

Ushirikiano na mpangilio mzuri wa kimaamuzi ngazi ya familia hujenga maadili mazuri kwa raia kwasababu familia ndicho kiwanda cha kutengeneza raia wa sasa na wakesho. Tujitahidi na kujikita zaidi katika kuweka ufanisi mzuri katika malezi ya familia na watoto ili kujenga taifa zuri la raia wa kesho.

Siku njema.
 
Ugumu wa maisha unachangia mkuu , sasa inabidi mama na baba wote watoke kutafuta kijiko ,kurudi usiku unajengaje familia mkuu?
 
Change the heading to Matumizi ya rasilimali za familia.

Nimefungua nilifikiri ungeongelea familiy structure - extended family, single parent family, joint family etc
 
Tafuta hela ndugu, acha kujifanya mtaalam wa masuala ya familia. Walio na nafasi zao hawawazi habari kupunguza matumizi ya sukari. Na mawazo yako yamekaa kibinafsi. Nikushauri tu, tafuta hela ndugu uache kutupa mawazo yako ya kimasikini.
Leta mawazo namna gani tunapata pesa za kutosha kukidhi mahitaji ya familia zetu.
 
Ugumu wa maisha unachangia mkuu , sasa inabidi mama na baba wote watoke kutafuta kijiko ,kurudi usiku unajengaje familia mkuu?
Najua. Inabidi kutafuta namna ya kupambana na kuweka mkakati. Mbona wengine wanaweza na wanakuwa na amani sana.

Chunguza sana couples ambazo mwanaume anatafuta halafu mwanamke anasimamia say kabiashara ka duka, au genge. Utaona hawa watu wana maisha ya tofauti sana.

Less stress na kipato chao kinakuwa kwa kasi kidogo.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Change the heading to Matumizi ya rasilimali za familia.

Nimefungua nilifikiri ungeongelea familiy structure - extended family, single parent family, joint family etc
Mmmmmmhmn hiyo mbona uzi ungekuwa mrefu zaidi ya huu. But nimefocus na familia ya baba mama watoto. Hizo nyingine siku hizi kudeal nazo ni mitihani.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Tafuta hela ndugu, acha kujifanya mtaalam wa masuala ya familia. Walio na nafasi zao hawawazi habari kupunguza matumizi ya sukari. Na mawazo yako yamekaa kibinafsi. Nikushauri tu, tafuta hela ndugu uache kutupa mawazo yako ya kimasikini.
Leta mawazo namna gani tunapata pesa za kutosha kukidhi mahitaji ya familia zetu.
Ni watu kama wewe ndio hufa na tai shingoni kwa hofu ya kushindwa kujadili mambo madogo ambayo ndio chanzo cha kuharibu mshikamano ndani ya familia.

Sasa wewe mimi naongelea ufanisi wa familia wewe unaongelea kutafuta hela kwan mtu akiwa na ufanisi mbovu hizo hela zitakwenda kutibu nini Kwenye familia?

Yaani mkeo awe anagawa vitu, anachezea pesa, watoto wanavunja na kuharibu vitu ndani wewe unaita ni familia hiyo ?

Ukiendelea na hizi fikra potofu mwisho wake ndio unajikuta unalea matoto hayana adabu, ambayo hayataweza kuishi popote na yoyote. Hata yakiwa majitu mazima yanakuwa mafujaji maharibifu na yatashindwa ishi na wenzao sababu ya viburi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom