Ukinyang'anywa mtoto, unaweza kuchukua maamuzi kama haya?

Mh hivi jamani hamna yoyote anaye muonea huruma mke wa ndoa ambae ndiyo kasalitiwa?

mke amlaumu mumewe 100%, mie kila cku nasemaga mtoto chini ya mwanangu wa pili cmpokei kwenye familia yangu, nalea niliemkuta alienikuta inamuhusu na baba yake na mama yake na uzinifu wao, kila mtu abebe mzigo wake aise.
 
huwa sielewi una nguvu na huna shida yoyote unagawaje mtoto wako kama unagawa pipi halafu unakuwa na amani kwanini mama asipewe nafasi akatunza mtoto wake mwenyewe na kama kuna support yoyote ya baba ipelekwe.
kwangu mi hawa watoto sioni tatizo ntawalea kama wanangu lakini kama mama yupo ni vizuri akae nao na msaada wa baba upelekwe kama nishule wasome na waangaliwe kama wa kwangu wanavolelewa tusiwaumize hawa viumbe kwa makosa tunayofanya sisi wazazi ndo maana wimbi la watoto wa mitaani linaongezeka kila kukicha.

mke amlaumu mumewe 100%, mie kila cku nasemaga mtoto chini ya mwanangu wa pili cmpokei kwenye familia yangu, nalea niliemkuta alienikuta inamuhusu na baba yake na mama yake na uzinifu wao, kila mtu abebe mzigo wake aise.
 
nilimpeleka mtoto hosp for a check up maana alikuwa na ka-homa kidogo! Wakati nasubiri kuingia kwa daktari nikasikia kelele za kilio toka chumba kingine, mama/dada mmoja akawa analia "nataka mtoto wangu, nipe mtoto wangu"
kwa makadirio ya haraka mimi na wateja wengine wa pale hospitalini tukahisi kwamba yule dada/mama alikuja na mtoto mgonjwa na either amefariki au kuna kitu kibaya kimetokea!
Mara tukasikia tena kelele za kuomba msaada "ananiua, ananinyonga", ikabidi tukimbilie kwenda kuona nini kinatokea! Tukakuta doctor mwanaume ambaye tshirt yake imelowa damu anamkaba yule mama sakafuni, wakaachanishwa!
Sasa baada ya ile sakata kutulia, yule dr akaingia kufanyiwa dressing ya wounds za kisu nyuma ya kichwa na shingoni!
Ikabidi tutafute sababu ya yule mama kumjeruhi yule dr ambaye tulidhani ni mume wake, kumbe ni tofauti kidogo! Yule mama aliongea kwa uchungu sana, akatueleza kwamba yeye na yule dr walikuwa ni wapenzi,
huyo dr ana mke na watoto sita wa kike, sasa amezaa na yule nyumba ndogo mtoto wa kiume! Yule jamaa akakata mahusiano na yule dada, mtoto alipofikisha mwaka 1 na miezi mitatu yule dr akaja akamchukua mtoto on mother's absence
akaenda kumficha anakojua! Sasa ndo yule mama akaja kudai mtoto pale kazini kwa hawara yake/baba mtoto! Dr akam-provoke kuwa yeye hakuwa na shida na yule dada, alikuwa na shida na mtoto wa kiume, so achape lapa! Dada wa watu ndo akawa mbogo, dr akaanza kumdunda, dada akatoa bisu lake akampa za shingoni na utosini!
Je wapendwa wazazi wenzangu, ingekuwa wewe ungeweza kuchukua uamuzi kama huo?

ingawa biblia yangu inasema kisasi ni cha bwana ial kuna vingine inabidi vianzie dunian

binafsi amempendelea kwa nyie kumkuta nakuwaachanisha walahi angekutana na dadazangu wamachame hiyo shingo ingekuwa alali yetu na mie kaka ningeifunga nkaiweka kwenye boneti ya gari easy...huu upuuziunatoka kwa wengi sana ..wasipopewa adabu watachomeka mpaka kwa mama zao..sio kila ushi sehemu ya kujaribia saizi ya uume wako zininge zina miba jamani watch out ushauri wa bure
 
Ulianza kwa ku-generalize issue.... hebu tuendelee kujadili % ya watoto wanaozaliwa katika ndoa na kulelewa na baba na mama kisha wakawa na staha. Na je, mfano baba na mama wameoana mmoja wao au wote wakiwa na watoto tayari, wakawalea kwa pamoja, inakuwa staha au sio staha?

Unless wale watoto wa kabla ya ndoa walitokana na ajali (ubakaji), talaka halali au ujane, vinginevyo hakuna staha. Kuhusu % nakupa wewe hiyo assignment ulete data za upande wako. Upande nilioko mimi ni kwamba kulelewa katika familia rasmi ndiyo heshima, na ninapojikuta mtoto niko kwenye mazingira kinyume na hapo bila maelezo yanayokubalika nachukulia kwamba nimeonewa na kudhulumiwa haki yangu, na anayebeba lawama zote za dhuluma hiyo ni yule aliyechukua mimba huku akijua kabisa hayo ndiyo yatakayokuja kumpata mtoto.
 
Kwani umejitia mimba mwenyewe?? Baba yupo ndo maana mimba ikaingia na sio kwamba baba anazuiwa kuja kumuona mwanae...
Baba habebi mimba. Mmefanya ngono kwa starehe zenu (na kwa kupenda kwenu starehe mkaona inakuwa tamu zaidi bila condom), na wewe mama unaelewa uwezekano wa mimba, bado unataka kichapo cha live, sasa kama si kujibebesha mimba hapo ni kufanya je?
 
Mi nasema hivi, ni bora nilelewe na wazazi wawili mafukara kuliko mama pekee tajiri aliyedaka sperm kutoka kwa lifataki ambalo lina mkewe na watoto wengine huko, na hata ndugu zangu wa huko eti waitwe 'half brothers' na 'half sisters', access kwa babangu iwe ya tabu, ninyapaliwe tuuuu, nimekosa nini? Kinamama wafikirieni watoto wenu kabla hamjawaingiza kwenye makwazo haya.
 
Hiyo ni tofauti maana hata mtoto atakuelewa kuwa hukuwa na nia ovu, ni bahati mbaya ilitokea baada ya kuzaliwa. Si kama yule anayepanga kuzaa kwa kumkosesha mwanaye baba.

Sasa ulivyogeneralize kwamba wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi wakati kuna ambao wanazaa kisha wanaachana?
 
Nakubaliana na wewe kwa hili, mtoto ni mtoto especially ukiwa mama, lazima utamfeel mtoto yeyote...

Niliwahi kumzaba kibao mama mmoja pale saba saba... alikuwa na watoto wawili ambao wamepishana kama miezi tu au mwaka... ametoka nao ndani ya maonyesho, watoto wamechoka vibaya sana, it seems walikuwa na njaa pia, and it was late around 7pm, akawa amembeba yule mdogo na anamburuza yule mkubwa... kale katoto kakawa hakawezi ku-keep pace na mama yake, kakawa kanaumia na kanalia, yule mama akaanza kumfokea na kumpiga... aisee i felt a twinge, nikajikuta nimemzaba kibao... lakini kumbe wengi walikuwa wanamwangalia anavyofanya ndo wakaanza kumgombeza, kwanza kwa nini amekuja na watoto wadogo hivyo kwenye fair grounds wakati anajua hali halisi ya pale... kwa kweli niliumia...

So, sio wamama wote wako hivyo, if a mother can desert his/her child then hashindwi kumfanyia mtoto wa mwenzie... inategemeana na roho ya mtu!! Ndio maana kuna malaika na shetani

Jamani kuna maumivu fulani mtu huwa unayapata mtoto wako akilia, kuumwa au kitu chochote yaani hata siwezi kuyaelezea sidhani kama mtu unaweza kuyapata kwa mtu mwingine hata kama unampenda vipi? sio kwamba watu wanachukia watoto wengine ila kuna uchungu fulani hivi huwa unatokea, ingekua ni rahisi basi watu wasingezaa wangekua wanaadopt tu watoto halafu biashara inaisha. Kuna mbaba kwenye thread moja mkewe hazai kakataa kuadopt matokeo yake kaenda kuzaa na mdada anamsumbua. Kuna hali fulani huwa inamtokea mama kwa mtoto wake wa damu na ndio iyo inayomfanya aonee huruma watoto wengine, ila kwa wako inazidi jamani sio kwamba mtu unakua una roho mbaya.

Mfano mtoto wa jirani akiwa na tabia za ujambazi, umalaya na mambo mengine mengi tu maovu. Unaweza ukaanza kusema mtoto wa fulani jambazi sana bora alivyofungwa wala huumii moyoni. Ila wa kwako akiwa jambazi akafungwa hutoumia moyoni ingawa hiyo tabia ya ujambazi huipendi? tuweni wa kweli jamani kuna tofauti kubwa kati ya unavyomfeel mtoto wako wa kumzaa na wa mtu mwingine.
 
Sasa ulivyogeneralize kwamba wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi wakati kuna ambao wanazaa kisha wanaachana?

naona una matatizo ya uelewa. Wapi niliposema wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi? Nimesema na narudia tena, wanawake wanaozaa watoto na wanaume ambao hawana ndoa nao wanafanya tabia ambazo hazina tofauti na zile za mbuzi wanaokutana machungani au mbwa koko wanaokutana majalalani maana wale hawana maadili, wanajizalia tu. Sijasema wazazi wote, acha uzushi.
 
Mimi jamani nilivyonauchungu na watoto wangu nahisi kama ntaweza kufanya hilo.., wewe mtoto afichwe, hujui yuko na nani na anakula nini halafu mtu anakujibu hovyo hovyo aa chochote chaweza kutokea. Hivi hawa madokta si ndio huwa wanaita watu kwenye klinik zao kushauri watu jinsi ya kupata watoto wa jinsia fulani sasa kwanini yeye ameshindwa kushauriana na mkewe.
 
naona una matatizo ya uelewa. Wapi niliposema wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi? Nimesema na narudia tena, wanawake wanaozaa watoto na wanaume ambao hawana ndoa nao wanafanya tabia ambazo hazina tofauti na zile za mbuzi wanaokutana machungani au mbwa koko wanaokutana majalalani maana wale hawana maadili, wanajizalia tu. Sijasema wazazi wote, acha uzushi.[/QUOTE]


HE!!!!!!!!!!!!!!!!
 
msamehe huyu maty nafikiri ndo kwanza anaona jua likimpiga ataacha kubwabwaja

naona una matatizo ya uelewa. Wapi niliposema wazazi wote wanaozaa ni mbwa na mbuzi? Nimesema na narudia tena, wanawake wanaozaa watoto na wanaume ambao hawana ndoa nao wanafanya tabia ambazo hazina tofauti na zile za mbuzi wanaokutana machungani au mbwa koko wanaokutana majalalani maana wale hawana maadili, wanajizalia tu. Sijasema wazazi wote, acha uzushi.[/QUOTE]


HE!!!!!!!!!!!!!!!!
 
daaah uamuzi si mbaya maana huwezi jua kama alitaka mtt kweli au viungo vya binaadamu...hawa madaktari wana mambo ya ajabu ndio hawa hawa wanaoshiriki ktk kuuza mazeru zeru mhhh angemuua tu kabisa,,,,,,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom