Ukinyang'anywa mtoto, unaweza kuchukua maamuzi kama haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukinyang'anywa mtoto, unaweza kuchukua maamuzi kama haya?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Darlingtone, Jan 18, 2011.

 1. Darlingtone

  Darlingtone JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilimpeleka mtoto hosp for a check up maana alikuwa na ka-homa kidogo! Wakati nasubiri kuingia kwa daktari nikasikia kelele za kilio toka chumba kingine, mama/dada mmoja akawa analia "nataka mtoto wangu, nipe mtoto wangu"
  Kwa makadirio ya haraka mimi na wateja wengine wa pale hospitalini tukahisi kwamba yule dada/mama alikuja na mtoto mgonjwa na either amefariki au kuna kitu kibaya kimetokea!
  Mara tukasikia tena kelele za kuomba msaada "ananiua, ananinyonga", ikabidi tukimbilie kwenda kuona nini kinatokea! Tukakuta Doctor mwanaume ambaye Tshirt yake imelowa damu anamkaba yule mama sakafuni, wakaachanishwa!
  Sasa baada ya ile sakata kutulia, yule Dr akaingia kufanyiwa dressing ya wounds za kisu nyuma ya kichwa na shingoni!
  Ikabidi tutafute sababu ya yule mama kumjeruhi yule Dr ambaye tulidhani ni mume wake, kumbe ni tofauti kidogo! Yule mama aliongea kwa uchungu sana, akatueleza kwamba yeye na yule Dr walikuwa ni wapenzi,
  Huyo Dr ana mke na watoto sita wa kike, sasa amezaa na yule nyumba ndogo mtoto wa kiume! Yule jamaa akakata mahusiano na yule dada, mtoto alipofikisha mwaka 1 na miezi mitatu yule Dr akaja akamchukua mtoto on mother's absence
  Akaenda kumficha anakojua! Sasa ndo yule mama akaja kudai mtoto pale kazini kwa hawara yake/baba mtoto! Dr akam-provoke kuwa yeye hakuwa na shida na yule dada, alikuwa na shida na mtoto wa kiume, so achape lapa! Dada wa watu ndo akawa mbogo, Dr akaanza kumdunda, dada akatoa bisu lake akampa za shingoni na utosini!
  Je wapendwa wazazi wenzangu, ingekuwa wewe ungeweza kuchukua uamuzi kama huo?
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Ndio hapo sasa kuvamia wana ndoa. Huwa mambo hayakai kueleweka hata kidogo. Mama azae mtoto mwingine tu
   
 3. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  huo ni unyama unaofaa kukemewa
   
 4. LD

  LD JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmmm, pole yake huyu dada, jamani mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitatu huyu baba anampeleka wapi?? Anyway hebu ngoja nisubiri maoni ya watu wengine kwanza.

  Manake kama neema ya Mungu haijakushika, unaweza ukajikuta unaua mwanaume wa style hii kabisaa.
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Azae mtoto mwingine tu?We unadhani mtoto anaweza kua replaced??Binafsi niko upande wa huyo mama...huyo mzee mshenzi kweli!
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  huyu Dr. ni mwenda wazimu.....kwani anafikiri Mama atakaa na mtoto hadi lini?? Ningekuwa mimi wala sijui ningefanyaje pamoja na kuwa sheria na haki zote nilikuwa ninazifahamu fika (inauma jamani asikwambie mtu) Nakumbuka kuna siku junior wangu alikuja chukuliwa .............tena mbele yangu si in my absence...nilichanganyikiwaje...hata hizo sheria sikuzikumbuka) acheni kabisa bana........... yaani mara kumi na ngapi sijui achukuliwe akiwa ashakuwa na akili yake lakini mwaka mmoja na kitu ...........acha kabisa

  mimi nakumbuka T-shirt niliivalia chini kwenye ngazi....hapo ni saa nne usiku hata sijui nlikuwa naelekea wapi, ah acha kabisa bwana.
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Lizzy nahisi mi ningetokea ningemsaidia huyu mama kummaliza kabisa huyu mwanaume, halafu anasema eti alikuwa na shida na mtoto sio mama,fine lakini mbona hakujali wakati akiwa tumboni akasubiri akakua kidogo hivo??
   
 8. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mi ningemng'ata hadi ninyofoke na something kwanza,.afu sheria ichukue mkondo wake..yani mimba ulee mwenyewe then aje tu,jambaz kweli!alidhani mwanamke ni kama kuku?anatotoa tu..
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mj1 yani sipati picha, nahisi ningekuepo halafu nijue kinachoendelea ningejitolea mhanga tu, hapana ujinga kama huu. Mwaka mmoja na miezi mitatu, anampeleka wapi huyu.
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani kaniudhi kweli!Tatizo wanaume wanadhani mapenzi yao kwa watoto ni sawa na aliyonayo mama!Hamna comparison aisee...huyo anastahili kipigo cha mbwa mwizi!
   
 11. Atoti

  Atoti Senior Member

  #11
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Huyo mwanaume ni myama, baniani mbaya kiatu chake dawe eh? Hamtaki mama but mtoto anamtaka.. Bloody shwain.. hata sheria hairuhusu mtoto under 7yrs kulelewa na baba..
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  MJ1 pole mpendwa!Yani siwezi kuimagine!Mtu unaweza kujikuta unaua hivi hivi majuto baadae akili ikikaa sawa!
   
 13. LD

  LD JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uwiiiii, natamani tufanye maandamano tukamkomboe huyo mtoto, na huyo baba tumtundike juu ya mti ka yule HAMANI kwene kitabu cha Esta kwene biblia.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Hilo deal lao mpaka nijue pande zote zilikubaliana nini maana bwana dunia ya leo duuuh
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Madai yake ana mke wake ndo atamlea aisee hapana......mi nakwambia wangu ilikuwa ni dakika lakini nahisi nilikonda na kupunguza kilo kwa sababu by the time namalizia kuvaa t-shirt chini ya ngazi ndo nagundua kuwa skin jeans ninayovaaga mara kwa mara bila mkanda, inanipwaya.......mbona niliishikilia kwa mkono?,miguuni sina hata kandambili ah......................sitaki kuikumbuka ile siku.
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kumnyang'anya mama mtoto wake ni UNACCEPTABLE!Labda kama anamnyanyasa na hamjali...zaidi ya hapo hairuhusiwi kwenye kitabu changu!
   
 17. LD

  LD JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pole pole poleeee sana, sio rahisi aisee. Yani unajua wakati naisoma hio thread nilikuwa nasisimka, natamani labda huyo daktari angetokea nikammalizia tu mi mwenyewe, mke wake gani akamlee mtoto wa mwaka mmoja na miezi hiyo. Hebu ASHINDWE kabisa.
   
 18. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Plus viboko vilivyokwenda shule,.i can picture hz face kama ya kangaroo vile!
   
 19. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  :frusty::frusty::frusty: ninachukia watu wanaochagua jinsia za watoto......! ina maana angekuwa wa kike asingehangaika naye.:frusty:
   
 20. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #20
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante Lizzy hata hivyoninamshukuru Mungu na pia ninamshukuru huyo Ex- wangu alipata akili baada ya mimi kumpigia simu baba mkwe na kumweleza kuwa usiku huo mwanae atalala ndani ...akaongea naye bahati nzuri he was wise enough kunsikiza baba yake after half an hour akanirudishia darling wangu.................na tray ya mayai .....ilinibidi tu nicheke.

  Acha bana nusu saa lakini it was like a week I see. Mimi siujui uchungu wa kuzaa kwani sikubahatika kuusikia kipindi kile ila siku ile nahisi vile nlivyokuwa nasikia ilikuwa ni uchungu....ahaaaaaaaaaa hapana bana Lizzy.
   
Loading...