Ukimya wa viongozi wa dini, mtasema lini?

Ukimya wa viongozi wa dini, mtasema lini?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,290
Reaction score
96,515
Ukimya wenu unatia mashaka uumini wenu kwa Mungu mnayemtumikia wakati kondoo wanahitaji kauli yenu. Tutawasikia siku ikitangazwa kuwa Tanzania ni nchi ya kiislamu, au inajiunga OIC, hapo maaskofu mtalipuka , maana linahusu maslahi yenu. Hivyo hivyo Masheikh ikisemwa sheria ya ndoa ni mke mmoja mtalipuka kwa vile imegusa imani yenu.
Nyote Kuminywa kwa democrasia hakuwahusu, mko kimya

==============================

Hapa tupate majibu. Baraza LA maaskofu (TEC) na Jumuia ya Kikristo (CCT) ni makundi yanayoheshimika sana.

Kwenye mitandao kumekuwa na tuhuma kuwa pamoja na utawala wa awamu ya tano kuja na speed kubwa ya kusigina katiba na sheria kiasi cha kuhatarisha amani ya nchi kuliko kipindi chochote toka uhuru hawaja kemea hali hiyo kwa vile muhusika ni muumini wao tofauti na JK ambaye walikuwa wanamkomalia hata masuala madogo madogo.

Taarifa hizo binafsi zimenifedhehesha na kujiuliza jee kuna ukweli? Kama ni hivyo hamuoni mna tuondolea imani tuliyokuwa nayo na taasisi hizo?
 
wote hao waganga njaa niliwaamini sana ndugu zangu katoliki niliposikia tu serikali mbili nimechoka
 
Wanaifanya kazi yao. Hawapo kwa ajili ya kuhakikisha demokrasia ipo, wapo kutuongoza kiroho kwa ajili ya maisha yajayo ambayo hayapo bayana. Nisaidie andiko la kitabu chochote linalosema bila demokrasia hakuna kwenda mbinguni.
 
Viongozi wa dini ni wanasiasa pia kwa mtindo tofauti labda ungesema viongozi wa KIROHO.Sasa niambie ulitaka wasemee jambo gani hasa maana wao HUNENA rohoni na Mungu huwasikia na kuleta matokeo chanya lakini kwa hao uliowataja UTASUBIRI sana wanaangalia ujaaji wa KIBABA kwanza
 
Ukiona watu unaowategemea wakusaidie wako kimya kwa muda mrefu, lazima wewe ujiulize kama unachofanya kiko sahihi badala ya kuanza kuwalaumu.

Ukimya wao unatoa ujumbe kuwa hicho unachotakifanya hawakiafiki.
 
Wanaifanya kazi yao. Hawapo kwa ajili ya kuhakikisha demokrasia ipo, wapo kutuongoza kiroho kwa ajili ya maisha yajayo ambayo hayapo bayana. Nisaidie andiko la kitabu chochote linalosema bila demokrasia hakuna kwenda mbinguni.
Huwezi kuuona ufalme wa mbinguni pasipo kutenda haki.
 
Wenzako wanapiga ibada wapate uwokofu na daraja za juu kiimani unataka wasupport mambo yenu ya kushikishana UKUTA .. hell no Mashekh zangu na Maskofu baba pegine ibada na endeleeni ku-mute hadi Mungu awasikie maombi yenu ya kiroho.Amen
 
Wewe ulitaka waseme nini, demokrasia hipi unayoizungumzia wew. Wana Uhuru katika nchi yao kusali popote, kuhubiri popote.
 
Vyama vya wafanyakazi vimenyea sembuse wao!.Heri wakae kimya maana siasa si zao
 
Siku hizi kuna dini basi? wewe anzisha kanisa lako tuje kukuchangia sadaka maisha yaende.
 
Umeona TUCTA, CWT NA TUGHE wana payuka tena? HATA wao hawajui hii ngoma wataichezaje, mdundiko unapigwa, kwaya inapigwa, bongo fleva IPO, viduku vipo, rege IPO, Taarabu IPO, nachi zipo NA..... Sasa wafuate lipi? Kumbuka NJAA haina BAUNSA
 
Ukimya wenu unatia mashaka uumini wenu kwa Mungu mnayemtumikia wakati kondoo wanahitaji kauli yenu. Tutawasikia siku ikitangazwa kuwa Tanzania ni nchi ya kiislamu, au inajiunga OIC, hapo maaskofu mtalipuka , maana linahusu maslahi yenu. Hivyo hivyo Masheikh ikisemwa sheria ya ndoa ni mke mmoja mtalipuka kwa vile imegusa imani yenu.
Nyote Kuminywa kwa democrasia hakuwahusu, mko kimya
shiiiiiiiii.........
wanasali
 
Back
Top Bottom