Ukimya wa Lowassa wakitia homa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Ukimya wa Lowassa wakitia homa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

watu wasiotaka kushindwa lazima watafute porojo ili wawe midomoni mwa watu! tafadhali hizi ngonjera kawasimulie watoto yatima zitawafariji zadi kwa kufanya muda uende na wewe kukuondelea msongo wa mawazo.:glasses-nerdy:
 
NA IWE HIVYO TUMECHOKA MATUSI DHARAU / USHINDI ASB NA MAPEMA KWA SEIF ZNZ NA ..........BARA./ii
 
Na ni UKAWA hao hao waliomshutumu sana Lowasa kuwa fisadi wa Richmond......wao hujipambanua kama wasafi, iweje waamue kuingia katika viatu vya Lowasa fisadi?

kinachotakiwa ni kuitoa ccm madarakani kwanza mengine ni baadae hata Lowasa anaweza kujirudi baada ya kuona kumbe ccm walikuwa wanamtumia tu,bila kujali kwamba uwepo wake kuwa ccm ndio salama ya ccm
 
kinachotakiwa ni kuitoa ccm madarakani kwanza mengine ni baadae hata Lowasa anaweza kujirudi baada ya kuona kumbe ccm walikuwa wanamtumia tu,bila kujali kwamba uwepo wake kuwa ccm ndio salama ya ccm

siyo kwa Lowasa huyu....
 
Baada ya mchakato mzima wa Chama Cha Mapinduzi kumtafuta mgombea wake wa urais kwa mwaka 2015 kumalizika, huku ukigubwika na sintofahamu nyingi kutokana na rafu za waziwazi kuchezeka kwa moja ya mgombea wake ambaye ni Mhe Edward Lowassa bado ameendelea kuwa kimya na kutosema chochote na kuzidi kukipa maswali mengi chama chake.

Nguvu nyingi zilitumika ikiwa ni pamoja na kuvunja Kanuni, taratibu na sheria zilizojiwekea tangu kuundwa kwa chama hicho nia ikiwa ni kuhakikisha kinazima ndoto ya mgombea huyo. Nguvu hiyo ya ziada ilibidi kutumika baada ya kugundua nguvu kubwa aliyonayo mgombea huyo ndani ya chama hicho na kwamba hakuna hoja ya msingi ya kuweza kukata jina lake ndani ya Kamati Kuu.

Kama ilivyo ada miaka yote ya uchaguzi ndani ya chama hicho kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho, Kamati ya Maadili haina mamlaka ya kukata jina la mgombea awaye yoyote yule kwa kuwa kikanuni kazi hiyo hufanywa na Kamati Kuu tena kwa hoja za msingi.

Mwanasiasa Mkongwe wa chama hicho Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru ametanabaisha vyema katika press aliyoifanya hivi juzi nyumbani kwake masaki na kuita waandishi wa habari kwa kuwaeleza kuwa kilichofanywa na CCM safari hii ni Uhuni, batili na si haki.

Kwa kuonyesha kutoridhishwa na kile kilichofanyika ndani ya Chama hicho, mamia ya Wanaccm wameanza kurudisha kadi za Chama hicho na kuhamia katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Tangu kuisha kwa mchakato huo wa kuteuliwa mgombea huyo wa CCM ni takribani wiki moja sasa ila Mhe Lowassa ameendelea kuwa kimya na kutozungumza lolote, ingawa aliita waandishi wa habari hivi majuzi nyumbani kwake jijini Dar es salaam na ghafla akaghairisha mkutano ule.

Habari za ndani zinasema kughairishwa kwa mkutano ule ghafla ni baada ya kuitwa na chama chake kuombwa wazungumze kwani inasemekana ana mpango wa kukihama chama hicho, ambapo inasemekana Mhe Lowassa hakuitikia wito huo.

Habari hizo ambazo zimekuwa zikitiliwa mashaka kuwa ni za kweli baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kushindwa kutangaza mgombea wake wiki iliyopita, ikisemekana bado wanafanya mazungumzo na Lowassa zimekuwa zikikichanganya CCM na kutumia kila namna kumfanya Mhe Lowassa kuachana na maamuzi hayo.

Baada ya jitihada za CCM kumwita wapate kuzungumza kufeli, wamekuwa wakitumiwa watu wa karibu wa Lowassa kumshawishi na kumshauri kama kweli ana mawazo hayo ayatupilie mbali kwani kitendo hicho kitamuondolea heshima yake kwa jamii au kumsababishia matatizo.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ukiendelea kuwa na kigugumizi juu ya nani atakaepeperusha bendera ya umoja huo, hivi juzi akihojiwa na waandishi wa habari ndani ya Colloseum Hotel Mhe James Mbatia amesema tayari wamempata mgombea ambaye ndio chaguo la watanzania na watakuwa tayari kumtangaza baada ya wiki moja.

Kila mtanzania macho yake na masikio vikisubiri kwa hamu zote kufahamu kama yanayovuma ni kweli ama lah. Kama ni kweli, ina maana Slaa na Lipumba wamekubali kumpisha Lowassa, nA kama sio kweli, ina maana Lowassa amekubali kushindwa kirahisi hivyo.

Ni jumatatu ama jumanne ya wiki ijayo tutapata kujua kama yaliyomo yamo, tuvute subira.

Nyie wanafiki sana. Na pesa alizokuwa anagawa waziwazi hamkuziona? Acheni ujinga wenu
 
Tukumbuke hata MUNGU alimtumia sauli aliyekuwa mtesaji na muuaji kuwa mtetezi wa watu.Lowasa aje Ukawa ili kwa nguvu ya pamoja ya mafuriko Tuuondoe rasmi mfumo CCM unaotesa watu ktk Taifa hili
 
tuache utani,lowasa ana nguvu huyu mzee aisee.
 
CCM Lazima wapinge Lowasa kwenda ukawa hv walichomfanyia Kule Dodoma ndio kimempa heshima lowasa na kitamjenga?CCM ni wakinga sana,na lowasa akiwasikiliza hawa manyang'au wa CCM amekwisha kwa sababu mipango ya CCM imekamilika baada ya kumkata jina,sasa Lowasa kazi kwake kama ni aibu CCM wameshamtwika sasa sijui akijiunga UKAWA atajikosesha Heshima ipi.
 
Acheni hadithi za kitoto,kama lowasa angekuwa muhimu kwa ccm asingekatwa,kwa sababu ni fisadi ndiyo maana kakatwa,iweje tena hao hao ccm waanze kumuomba asiende ukawa,fuatilieni siasa vizuri siyo kukurupuka tu na story za mtaani ni aibu,hayo mambo waongee wale ambao hawakubahatika kukanyaga shule
 
Acheni hadithi za kitoto,kama lowasa angekuwa muhimu kwa ccm asingekatwa,kwa sababu ni fisadi ndiyo maana kakatwa,iweje tena hao hao ccm waanze kumuomba asiende ukawa,fuatilieni siasa vizuri siyo kukurupuka tu na story za mtaani ni aibu,hayo mambo waongee wale ambao hawakubahatika kukanyaga shule
Unaweza kukanyaga shule na ukawa na akili mbaya kama zako. Huna sababu yoyote ya maana ya kuita wenzio watoto. Shule yako inakusaidia wewe na mama yako. Hapa kila mmoja ana nafasi ya kutoa hoja/maoni yake. Haijarishi umekwenda shule au umebaki nyumbani kama mimi.
 
Acheni hadithi za kitoto,kama lowasa angekuwa muhimu kwa ccm asingekatwa,kwa sababu ni fisadi ndiyo maana kakatwa,iweje tena hao hao ccm waanze kumuomba asiende ukawa,fuatilieni siasa vizuri siyo kukurupuka tu na story za mtaani ni aibu,hayo mambo waongee wale ambao hawakubahatika kukanyaga shule
thibitisha ufisadi wake
 
Muulize kama anahamu na siasa za nchi hii. Yeye sio zaidi ya chama! Wamekatwa wengi katika kugombea uraisi katika stage hiyo! Amuulize mzee Malecela, Mwandosya, Ahmed Salumu, Sumaye na Kikwete!!' Maamuzi ya chama ni ya maslahi kwa wananchi na si ya masilahi ya mtu mmoja!
 
lowasa huwa sio muongeaji sana,ni mtendaji sana...
 
Kwani Lowassa ana tofauti gani na vigogo wengine waliokatwa mbona wanaendelea na shughuli zao. Magufuli atosha.
 
amesusa kama alivyosusa uwaziri mkuu. anyway ni kawaida yake kukaa kimya hata suala la Richmond alikaa kimyaaa
 
Back
Top Bottom