Ukimya wa Lowassa unaitesa CCM na UKAWA

Ukimya wa Lowassa unaitesa CCM na UKAWA

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,344
Reaction score
9,845
Wadau tukubali tu kwamba katika Mambo mageni tuliyoona kwenye wakati huu ni nguvu na ukubwa wa sauti ya Ukimya wa Lowasa.

Nimejaribu kupitia mabandiko mengi hapa JF na ninaona mengi ni malalamiko au matokeo ya wasiwasi wa ukimya wa Lowasa.

Magufuli ameanza kwa kasi ya ajabu bila kujali uelekeo ili kujaribu kuzima makali ya sauti ya ukimya wa Lowassa.Anatamaani sana Lowasa asahaulike mapema ili apate nafasi ya kujenga jina lake na labda umaarufu wake mwenyewe.
Kwa bahati mbaya kila anachofanya kinaongeza kumbukumbu na ukubwa wa sauti ya Ukimya wa Lowasa.

Wamejitokeza wana CCM humu wanaomshambulia Mbowe,wanamshambulia Mbatia,wanakishambulia CHADEMA na vyama vya ukawa,wanachokoa kwa kijiti wapate majibu.Watu kama Juliana Shonza na Faiza walioumizwa na Ukimya wa Lowasa.

Ni dhahiri sasa taifa limetega sikio,liko makini kiasi kwamba hata sindano ikianguka linasikia,lina kiu na sauti ya mtu mmoja tu, Linateseka kwa ukimya wake,linataka kumsikia Ndugu Edward Ngoyae Lowasa.

Mihemko ya kisiasa inayoongelewa na vyombo vya usalama ni mawimbi tu ya Ukubwa wa sauti ya ukimya, intelijensia inaumizwa na ukimya.Naanza kuipenda falsafa hii ya ukimya.

Ila kama mdau tu wa UKAWA na mwanachama wa kawaida kwenye chama changu nitumie fursa hii kumuomba Ndugu Edward Ngoyae Lowassa aongee kitu, Taifa linaumia.
 
Always ukimya ni jibu zuri, na hakuna haja ya yote hayo kama kuna pingamizi unaenda sehemu husika otherwise tujenge taifa
 
Sasa tutishwe na ukimya wake Kwasababu gani??
Na Magufuli hapigi kazi Kwasababu ya Lowasa!
Kwa taarifa yako huyo Mamvi wenu hana Dili tena, sio ndani ya CDM wala ndani ya Ukawa!
Ni sawa na kondomu ikishatumiwa hakuna anayetamani hata kuigusa!!!
Magufuli ndio habari ya mjini!!!
 
How can a dead case resurface?
 
unaumia ww na sio taifa, usiisemee mioyo yetu kama tumekutuma vile. ameshindwa aendelee kukaa kimya hivyo hivyo maana hana cha kusrma.
 
Muacheni mzee wa watu apumzike. . . . . uwezo wa kusema anao akiamua. . .
 
Mkuu hebu edit hiyo title na uondoe neno Taifa. Yaani mi niumizwe na ukimya wa lowassa. halafu unasema kabisa taifa linaumia eboo!!
Hiv nani kakupa mamlaka ya kuwasemea watu?? We unajuaje kama mi naumia au la? Yaani mie niache kufanya mambo yangu kwa amani nishughulishwe na mfanya maigizo yule!!
Kweli JF siku hizi kumejaa vilaza.
 
unaumia ww na sio taifa, usiisemee mioyo yetu kama tumekutuma vile. ameshindwa aendelee kukaa kimya hivyo hivyo maana hana cha kusrma.

...na wewe unausemea moyo wa nani?!
 
Wee jamaa, ebu muache mzee wa watu apumzike, acha kumtumia kwa maslahi yako binafsi!
 
Mie nishaanza kumuamini Magufuri. Ukimya wa Lowassa nimekuja kugundua sio sifa ila ni madhaifu makubwa sana aliyonayo. Alinyamaza kuhusu kashfa lkn Kikwete siku anafunga kampeni Mwanza akamchana live na matokeo tumeyaona. Mtu ambaye ninamkubari kwa sasa ni Maalimu Seifu na tamko lake kwa wakati muafaka katika uchaguzi huu. Tusijidaganye Lowassa tulimpenda sana na tulimpa kura nyingi sana lkn hakuwa amejipanga kuzilinda. Tupelekeni mawazo yetu Zanzibar kama matunda ya UKAWA. Shukrani zimwendee Mansour aliyetoka CCM na kuunda kamati ya kumpeleka Seif ikulu na kweli wamefanikisha kwa mpangilio ulionyoka.
 
Unaumia peke yako usichanganye wenzio,kama hulali ni wewe maisha yangu yanasonga with or without Lowassa....
 
Ni ajabu sana mnapolazimisha kila mtu afanane na mnavyotaka nyie. Kila mtu yuko tofauti, sio lazima awe unavyodhani. Naheshimu alivyo maana huyo ndiye Lowassa na hatakaa awe kasuku kama wewe uwazavyo. Waacheni wazee wapumzike, sio lazima kila kitu mkifahamu na mipango na anayoongea mjue. Eboo!
 
Mie karibu narest in peace kwa ukimya wao tena na huu mnyukano ya viti maalum umenimaliza nguvu kabisa.
 
ukimya wa lowassa unawatesa wafuasi wake hasa chadema....

Ccm hatuna na time na zeee hilo....
 
Mzee mshapiga hela zake sasa hivi anaugulia maumivu mnataka aseme aongee nini sasa kuwa amepata hasara asioitegemea?
 
Mafuriko ya kipindi kile si yalikua ya maigizo. unadhani saizi watu watadeki barabara na kuzimia. Atulie tu huko aliko asubiri kufilisiwa mali zote alizozipata kwa kutuibia Watanzania. Na makampuni yake yote yaliyokua yanafanya janja janja kukwepa kodi nk yatakiona cha mtema kuni
 
Mzee wenu alishachinjwa bila kuoneshwa kibla huko baharini na kuzamishwa kwa jiwe zito kama osama! Akumbukwe kwa lipi hasa?
 
Back
Top Bottom