Ukimya wa Lowassa kuna Siri nzito

Ukimya wa Lowassa kuna Siri nzito

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
408
Huwa nakaa na kufikiria sana ukimya wa Lowasa katika siasa za Tanzania huwa sipati majibu mpaka leo. Sijwahi kupata majibu ya ukimya wa Lowasa.
Pia,huwa nashindwa kumwelewa Lowasa kutumia nguvu nyingi kiasi hiki kutaka urais wa JMT. Lowasa akiwa Rais wa nchi hii hawezi kuwa Rais wa zaidi hata miaka 5 inawezekana hata mwaka mmoja kwake unatosha ila ana lengo lake alilolikusudia( kwa mtazamo wangu na muda niliokaa kufikiria juu ya ukimya wa EL)
ukimya huu wa EL sio wa bure hata kidogo,ametukanwa,amekashifiwameitwa kila aina ya majina,Fisadi,Richmond nk lakini yeye hajawahi kumtukana,kumkejeli mtu,kusema hadharani nk
tutafakari pamoja, sijwahi kuuelewa ukimya wa EL
 
Kuna ripoti ya Madaktari wanaomtibu ambayo inaonesha kuwa Lowasa hawezi hata kukimbia mita 10
 
ngoja laki ni pesa aje atolee ufafanuzi
 
Ukimya ndio dawa ya kila kitu,...kuna waziri moja (Nyalandu) kapigwa siku mbili tu ya tatu akafunguka kuhusu Aunt Ezekiel sasa lowassa tokea 1995 anapigwa tu na bado yuko imara, kwa kweli tanzania tunataka kiongozi anayeweza kuweka mambo makubwa na madogo katika vifua...
 
Kuna siku niliwaza juu ya Afya ya EL. na kujiuliza "Hivi EL angekuwa chama cha upinzani kama kina Dr. Slaa,Mboe au Lissu si tungekwisha msahau. Mana nikiangalia jinsi Makamanda wanavyopambanaga na polisiccm, na jinsi EL watu wanavyodai kuwa hawezi kukimbia ata mita10 sijui ingekuaje.
 
Kuna ripoti ya Madaktari wanaomtibu ambayo inaonesha kuwa Lowasa hawezi hata kukimbia mita 10
Hiyo ripoti unayo mkuu ili utusaidie? Mwenye kujua ripoti yake ni yeye mwenyewe au mke wake therefore kwa kuwa wewe sio mwenyewe basi inaonekana ni mke wake
 
Ukimya wa Lowasa unaashiria kukata tamaa na anaandamwa na maradhi yasiyotibika
 
Ukimya ndio dawa ya kila kitu,...kuna waziri moja (Nyalandu) kapigwa siku mbili tu ya tatu akafunguka kuhusu Aunt Ezekiel sasa lowassa tokea 1995 anapigwa tu na bado yuko imara, kwa kweli tanzania tunataka kiongozi anayeweza kuweka mambo makubwa na madogo katika vifua...
Silence miens yes.
Anaitwa fisadi- Kimya.
Hawezi kuzunguka uwanja wa taifa ata raundi moja- Kimya.
Afya mgogoro- Kimya.
 
Kuna siku niliwaza juu ya Afya ya EL. na kujiuliza "Hivi EL angekuwa chama cha upinzani kama kina Dr. Slaa,Mboe au Lissu si tungekwisha msahau. Mana nikiangalia jinsi Makamanda wanavyopambanaga na polisiccm, na jinsi EL watu wanavyodai kuwa hawezi kukimbia ata mita10 sijui ingekuaje.
Huko umeenda mbali. Chukulia Lowasa ni Rais wa nchi, huku anatakiwa kimataifa na ndani ya nchi ziara zinamngoja, na kuna hafla kibao za kitaifa. Nadhani tutakuwa na Rais kama Michael Satta wa Zambia
 
kukaa kimya ni jibu la mjinga,usione kobe kainama ujue anatunga sheria,vivile kimya kina mshindo mkubwa.big up muheshimiwa rais edward lowasa kwa ukimya wako.
 
kukaa kimya ni jibu la mjinga,usione kobe kainama ujue anatunga sheria,vivile kimya kina mshindo mkubwa.big up muheshimiwa rais edward lowasa kwa ukimya wako.
Fisadi Lowasa ni janga la taifa
 
Lowasa bora anyamaze tu hana cha kuongea amechafuka sana kichwani hadi miguu maovu yote yake akisema neno atakuwa anakwaza watu tu tena asituzoee kabisa hakuna wa kumpa urais kabisa ataibia watanzania tu.
 
Back
Top Bottom