UKIMWI tu ama tupimwe magonjwa yote kabla ya kufunga ndoa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,892
16,413
UKIMWI tu ama tupimwe magonjwa yote kabla ya kufunga ndoa?

Kwanini huwa hawapini kisukari, figo, moyo, vidonda vya tumbo, matatizo ya ini, matatizo ya akili na mengineyo yote?

Kwanini wasifanye full medical checkup wao wanang'ang'ania kupima kama mtu yupo kwenye 'gridi ya taifa'? Kwanini UKIMWI tu? Kwanini ngwengwe tu?

Ninawasilisha mada
 
Nadhani kinachoangaliwa zaidi ni kupima magonjwa ya kuambukiza ambayo hayana tiba. Wote tunajua UKIMWI sio ugonjwa lakini ndo hivyo kwamba hauna tiba na unaambukizwa asilimia kubwa kwa njia ya sex.

Hayo magonjwa mengine kama vidonda vya tumbo au figo hayawezi kusababisha watu wasioane kama wanapendana kwa dhati.

Yote kwa yote, ni vizuri kujua afya yako kwa ujumla na sio kwenye "umeme" tu.
 
Unaijua hepatitis B mkuu? Inaambukizwa kwa ngono na haina tiba endelea kupima ukimwi tu
 
Back
Top Bottom