Peace be upon ya' all,
Hili swala limezua mjadala wa mda mrefu sana baina ya madaktari wao kwa wao wakivutana kwa hoja kuntu kabisa.
Je ni kweli UKIMWI hausababishwi na HIV kwamba agenda nzima ni scam na kuwa hakuna kipimo cha kupima HIV bali vilivyopo hupima tu kushuka kwa kinga?
Hili swala limezua mjadala wa mda mrefu sana baina ya madaktari wao kwa wao wakivutana kwa hoja kuntu kabisa.
Je ni kweli UKIMWI hausababishwi na HIV kwamba agenda nzima ni scam na kuwa hakuna kipimo cha kupima HIV bali vilivyopo hupima tu kushuka kwa kinga?
- Tunachokijua
- HIV ama Human Immunodeficiency Virus ni kirusi kinachoshambulia mfumo wa kinga mwili, ambacho baada kuishi mwilini kwa kipindi fulani kinaweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI)
Sio kila mwenye HIV hupata UKIMWI kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupata matibabu ya mapema. Pia, UKIMWI ni hatua ya mwisho kabisa anayopata mtu aliyeshambuliwa na HIV ambayo huonesha kuwa mfumo wa kinga umeshambuliwa vya kutosha, kiasi cha kuwa dhaifu na kuishiwa uwezo wa kutoa kinga kwa mwili.
Ili mtu mwenye HIV aweze kuchukuliwa kama tayari kapata UKIMWI anapaswa kuwa na nakala za seli hai nyeupe aina ya CD4 chini ya 200 kwa kila millimeter cubic ya damu (200 cells/mm3).
Pia, anaweza kuwa na hali hii ikiwa mwili wake tayari utaanza kushambuliwa na magonjwa mengine nyemelezi yanayoendana na maambukizi haya. Pamoja na machapisho mengine, Unaweza kutumia What Are HIV and AIDS? Kama rejea.
Hivyo, kujibu sehemu ya kwanza ya swali, JamiiForums inathibitisha kuwa ni kweli kuwa HIV husababisha UKIMWI. Tunapaswa kufahamu kuwa UKIMWI sio kitu cha ajabu, isipokuwa ni Upungufu wa Kinga Mwilini, jambo ambalo husababishwa na kudhoofika kwa mfumo wa kinga za mwili.
Sehemu ya pili ya swali inahoji juu ya uwepo wa kipimo kinachoweza kupima HIV, kuwa kwa sasa hakuna kipimo cha HIV, kinachopimwa ni uthabiti wa kinga pekee na siyo virusi wenyewe.
Ndugu msomaji, ni muhimu kukufahamisha kuwa hadi sasa kuna walau vipimo vitatu vya kuutambua ugonjwa huu.
- Antibody tests
- Antigen/antibody tests
- Nucleic acid tests (NAT)
Kipimo cha mwisho ambacho ni Nucleic Acid Test (NAT) huangalia na kuthibitisha uwepo wa HIV, pamoja na kubaini idadi ya nakala zake halisi kwenye damu. Unaweza kutumia CDC kama rejea.
JamiiForms imezungumza wa wataalam wa afya, na kwa kurejea taarifa hizi inasisitiza kuwa madai ya kutokuwepo kwa kipimo kinachoweza kugundua uwepo wa virusi kwenye damu pamoja na idadi ya nakala zake sio ya kweli.
Pia, sio sahihi kusema kuwa harakati zote zilizo nyuma ya gonjwa hili ni “Scam” kwa kuwa tunashuhudia watu wengi wakiugua na kupoteza maisha kila mwaka.