Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Wakuu salamu!
Wakati nikiwa shuleni nilibahatika kusoma kidogo siasa. Katika jambo ambalo Mwalimu wangu alinifundisha ni kuwa Nchi za Kidemokrasia zinakuwa na Mihimi Mitatu ya Dola. Akaniambia mmoja unaitwa "Executive" mwingine "Legislature" na wa tatu ni "Judiciary". Akiwa amenikazia macho, huku akiongea kwa ukali kidogo na akionesha kusisitiza akaniambia "Mihimili hii ni kwa ajili ya Check and Balance! . Hakuna muhimili unaotakiwa kwa sababu au kwa namna yeyote kuingilia majukumu ya mwingine. Ni mwiko! kufanya hivyo ni kinyume na Katiba na sheria".
Uzembe ambao niliufanya ni kutokumuuliza kwamba ni nani sasa mwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa mihimili hii haiingiliani kimajukumu na kama muhimili mmoja kwa 'Makusudi' ukaamua kufanya kazi za mihimili mingine ni nani mwenye wajibu na nguvu ya kuzuilia hilo lisitokee!? . Au kwa lugha nyingine, kama muhimili mmoja kwa makusudi ukiamua kwenda kinyume na Katiba ni nini cha kufanya na ni nani mwenye wajibu na uwezo wa kufanya? ( tunaweza kutolea mifano nchi za Afrika Magharibi).
Kwa kuwa nilishafanya uzembe huo wakati nikiwa shuleni, labda sasa niombe mwenye ujuzi anisadie uelewa! maana nimejuuliza sijapata jibu kwa kweli.