Ukilaza wangu uliniponza, sasa naomba msaada kwa ajuaye!

Huyo mlw wako alikufundisha kijuujuu sana. Je alikufundisha ukweli kuwa wajumbe wa legislature wa kiamua kumkimbia kiongozi wa mhimili wao, tena kwa akili timamu na hiari yao wenyewe kitakachotokea ni kukosa cha kuwa ambia wanao wawakilisha na kuishia kulalamika kila uchao?
Yiyu sheping umenipa raha sana. Naamini ukiwa wameelewa
Ha ha ha ha!
 
Darasani walikudangaya, so that you can pass your exams..!! Just like ulivyosoma mwanadamu ALIKUWA NYANI... kisha with time akageuka kuwa mwanadamu.. huo ni uongo mkuu pia..!!

Huku kwenye FIELD, hakuna cha mihimili, mambo yote ni RAIS.. full stop..!! umeelewa..!!?

Narudia, huku kwenye field, kuna mhimili mmoja tu, na ndie ALFA & OMEGA, nae ni Mh. Rais..!! FULL STOP..!!

Na ww au babu wa babu wa babu wa babu na mababu wako hawajawahi KUWA NYANI kama ulivyofundishwa na mwalimu wako...!! FIELD huku ww uliumbwa kama mwanadamu period... na NYANI ALIUMBWA KAMA NYANI PERIOD...!! Kima aliumbwa kama KIMA period..!!

Usimeze tu unavyopewa darasani, ukifika HUKU FIELD yafuate ya huku, huku FIELD ndiko vitendo vipo..!!

Na baada ya RAIS, mkubwa anaefuata ni MUNGU... period..!!
 
Walioweka misingi ya check and balance, walisahau kuweka wazi mamlaka za uwajibishaji na usimamizi wa mihimili iliyopo

Kilichopo sasa, kinadharia mahakama ndo anajiona boss wa wengine. Why? Mihimili mingine ikigombana huenda mahakamani kwa uamuzi, lkn mahakama humalizana wao kwa wao.

Lkn ki uhalisia mwenye pesa ndiye boss wa wote. Anaweza amua mihimili mingine isifanye kazi kwa decade na hakuna wa kupinga
 
mihimili hii ukitaka isikupe shida, ipange vizur usiipishanishe, unatakiwa uanze na LEGISLATURE, EXACUTIVE, JUDICIALY.

-LEGISLATURE :, Wanatunga sheria.
-EXACUTIVE :, Wanatanga kwa wananchi.
JUDICIALY:-wanaisimamia.
tatizo lipo kwa EXACUTIVE. (utawara) ambao ndio wenye kusibitisha sheria ili isimamiwe.
kimyumecha wanavuluga. wanafanya wanavyotaka.
 
Wakuu salamu!

Wakati nikiwa shuleni nilibahatika kusoma kidogo siasa. Katika jambo ambalo Mwalimu wangu alinifundisha ni kuwa Nchi za Kidemokrasia zinakuwa na Mihimi Mitatu ya Dola. Akaniambia mmoja unaitwa "Executive" mwingine "Legislature" na wa tatu ni "Judiciary". Akiwa amenikazia macho, huku akiongea kwa ukali kidogo na akionesha kusisitiza akaniambia "Mihimili hii ni kwa ajili ya Check and Balance! . Hakuna muhimili unaotakiwa kwa sababu au kwa namna yeyote kuingilia majukumu ya mwingine. Ni mwiko! kufanya hivyo ni kinyume na Katiba na sheria".

Uzembe ambao niliufanya ni kutokumuuliza kwamba ni nani sasa mwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa mihimili hii haiingiliani kimajukumu na kama muhimili mmoja kwa 'Makusudi' ukaamua kufanya kazi za mihimili mingine ni nani mwenye wajibu na nguvu ya kuzuilia hilo lisitokee!? . Au kwa lugha nyingine, kama muhimili mmoja kwa makusudi ukiamua kwenda kinyume na Katiba ni nini cha kufanya na ni nani mwenye wajibu na uwezo wa kufanya? ( tunaweza kutolea mifano nchi za Afrika Magharibi).

Kwa kuwa nilishafanya uzembe huo wakati nikiwa shuleni, labda sasa niombe mwenye ujuzi anisadie uelewa! maana nimejuuliza sijapata jibu kwa kweli.

Kinadharia mihimili yote inasimamiana.

Kwa mfano, muhimili wa executive, rais akikiuka kiapo chake au kuvunja katiba, muhimili wa legislature unaweza kuanzisha impeachment process itakayofika kwenye muhimili wa judiciary na rais akipatikana na makosa anaondolewa.

Vivyo hivyo rais anaweza kuanzisha process ndefu sana ya kikatiba ya kumtoa Jaji.

Pia Mahakama inaweza kumkuta mbunge na hatia nje ya kinga ya kibunge, hatia ambayo inaweza kumvua mbunge ubunge.

Zaidi ya hapo, rais anaweza kukataa kutia sahihi muswada uliopitishwa na bunge kuwa sheria. Bila sahihi ya rais muswada hauwi sheria.

Kuna mengi yanayohusika katika checks and balance, kimsingi ni kwamba hakuna aliye juu ya mwenzake, wote wanatakiwa kuangaliana.

Kinadharia.

Kiukweli Magufuli kashaingilia bunge tangu fedha za tafrija zilipopelekwa hospitalini. Kaingilia Mahakama na kuahidi kuipa hela ikitoa maamuzi fulani.

Magufuli hajui au hajali checks and balance.
 
Mkuu, sasa kwa kuwa kuna mihimili isiyo na vyombo vya kutumia nguvu na silaha yao ni kujieleza tu, sasa ikidhibitiwa itakuwa je? kwa mfano nilikuwa nafuatilia taarifa nikaona huko Kenya kuna Wakili kauawa pamoja na mteja wake! walichokifanya mawakili wanaandamana (wakiomboleza) lakini najiuliza pia kwa mfano kama wangezuiwa wangefanya je zaidi ya kutulia tu? nafikiri waliotengeneza, au wataalamu wa nadharia hizi hasa Wasomi wa Political Science kuna vitu wanatakiwa watusaidie kwamba ulinzi wa mihimili hii kweli unaweza kuwa "guaranteed" practically kweli! na kivipi? au angalau ni kinadharia zaidi tu na kama ni nadharia, basi kutumaini katika nadharia ambazo practically hazina uhakika nayo inakuwa je?.

Mkuu sasa wakili ana uhusiano gani na mihimili mingine?au tuseme ni Jaji... Hapo sasa muhimili mwingine wa executive unaingilia, polisi watafanya kazi yao, watapeleka watu mahakamani...mahakama itafanya kazi yake, ila ndio mpaka hapo katiba itakapokuwa na nguvu dhidi ya wale walioapa kuilinda katiba hiyo
 
Mwananchi alifungua kesi mahakamani ya kutotendewa haki na polisi wa Kenya , mwananchi (mteja) akatafuta wakili wakumtetea mahakamani. Wakati wakili na mteja wake wanatoka mahakamani (kufungua kesi husika ili haki ipatikane), wakauwa na polisi wakaatupwa mtoni. Nafikiri unaona huo mkanganyiko hapo.
 
Katika kilatini kuna msemo "abusus non tollit usum" maana yake misuse does not remove use, Just because something is misused doesn't mean it can't be used correctly.

Huu mfano umetoka kwenye scenario ambayo justice imekuwa abused. Hauna maana kwamba checks and balance haifai.

Kama vile mtu anayesema checks and balance haifai kwa sababu imekuwa abused na Magufuli.
 
Jiulizeni kwa nini ya msingi ya Warioba yalitupwa. Ili kuondoa hizi checks na balances. Tatizo sio democracy bali muktadha wake ni shida kwa wengine. Kuna level fulani ya ustarabu inatakiwa sasa ukiikosa ni matatizo. Wengi wetu bado tunapendelea "strongman mentality"-kamata vyombo vya dola na vitumie upendavyo.
 
Katika kilatini kuna msemo "abusus non tollit usum" maana yake misuse does not remove use, Just because something is misused doesn't mean it can't be used correctly.

Huu mfano umetoka kwenye scenario ambayo justice imekuwa abused. Hauna maana kwamba checks and balance haifai.
Mkuu, hakuna aliyesema haifai. Binafi ni miongoni mwa wanaoipendwa sana ila swali la msingi ni ikiwa ni nani mwenye jukumu na nguvu ya kuzuilia mhimili mmoja ambao kwa makusudi umeamua kiingilia shunguli za mwingine kwa namna moja ama nyingine?
 
Kinadharia mihimili yote inasimamiana.

Kwa mfano, muhimili wa executive, rais akikiuka kiapo chake au kuvunja katiba, muhimili wa legislature unaweza kuanzisha impeachment process itakayofika kwenye muhimili wa judiciary na rais akipatikana na makosa anaondolewa.

Vivyo hivyo rais anaweza kuanzisha process ndefu sana ya kikatiba ya kumtoa Jaji.

Pia Mahakama inaweza kumkuta mbunge na hatia nje ya kinga ya kibunge, hatia ambayo inaweza kumvua mbunge ubunge.

Zaidi ya hapo, rais anaweza kukataa kutia sahihi muswada uliopitishwa na bunge kuwa sheria. Bila sahihi ya rais muswada hauwi sheria.

Kuna mengi yanayohusika katika checks and balance, kimsingi ni kwamba hakuna aliye juu ya mwenzake, wote wanatakiwa kuangaliana.

Kinadharia.

Kiukweli Magufuli kashaingilia bunge tangu fedha za tafrija zilipopelekwa hospitalini. Kaingilia Mahakama na kuahidi kuipa hela ikitoa maamuzi fulani.

Magufuli hajui au hajali checks and balance.
Bravo..
 
Mwisho wa siku wananchi ndio mwamuzi wa mwisho. Wananchi mkikaa kimya kusubiri chadema ndio pekee ifanye basi mtasubiri mpaka kiama. Wananchi wakiwa wakali basi automatically hata mihimili ya dola hutimiza wajibu wake sawa sawa. Nikupe mfano. Kuna mtu alifungua kesi kupinga ccm kubaki na mali baada ya vyama vingi kuanzishwa, hoja yake ikiwa kuwa hizo mali zilitafutwa na watanzania wote enzi ya chama kimoja. Huyo jamaa iliitelekeza hiyo kesi. Kisheria mtu akitelekeza kesi huwa inafutwa bila kuijadili kiundani. Sasa mahakama ya juu kabisa ya Rufaa ikaendelea na kesi kuijadili kiundani na kutangaza maamuzi ya ajabu kuwa eti ccm inamiliki mali hizo kihalali. Lakini nadhani wote mmejua kuwa hata baadhi ya majaji na jaji mkuu waliohudumu hiyo nafasi wana kadi za ccm. Naamini wananchi wangekuwa wakali mihimili ya dola isingefanya upuuzi. Sasa maadamu wa tz tumezubaa kama kuku mwenye kideli, basi mihimili itaendelea hivyo kwa hovyo.
 
Mkuu, hakuna aliyesema haifai. Binafi ni miongoni mwa wanaoipendwa sana ila swali la msingi ni ikiwa ni nani mwenye jukumu na nguvu ya kuzuilia mhimili mmoja ambao kwa makusudi umeamua kiingilia shunguli za mwingine kwa namna moja ama nyingine?
Mihimili miwili mingine ina jukumu hilo.

Unatakiwa usiweze kupika mpaka uweke mafiga matatu. Ukiweka mawili sufuria litaanguuka.

In theory.
 
Back
Top Bottom