Ukilaza wangu uliniponza, sasa naomba msaada kwa ajuaye!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Wakuu salamu!

Wakati nikiwa shuleni nilibahatika kusoma kidogo siasa. Katika jambo ambalo Mwalimu wangu alinifundisha ni kuwa Nchi za Kidemokrasia zinakuwa na Mihimi Mitatu ya Dola. Akaniambia mmoja unaitwa "Executive" mwingine "Legislature" na wa tatu ni "Judiciary". Akiwa amenikazia macho, huku akiongea kwa ukali kidogo na akionesha kusisitiza akaniambia "Mihimili hii ni kwa ajili ya Check and Balance! . Hakuna muhimili unaotakiwa kwa sababu au kwa namna yeyote kuingilia majukumu ya mwingine. Ni mwiko! kufanya hivyo ni kinyume na Katiba na sheria".

Uzembe ambao niliufanya ni kutokumuuliza kwamba ni nani sasa mwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa mihimili hii haiingiliani kimajukumu na kama muhimili mmoja kwa 'Makusudi' ukaamua kufanya kazi za mihimili mingine ni nani mwenye wajibu na nguvu ya kuzuilia hilo lisitokee!? . Au kwa lugha nyingine, kama muhimili mmoja kwa makusudi ukiamua kwenda kinyume na Katiba ni nini cha kufanya na ni nani mwenye wajibu na uwezo wa kufanya? ( tunaweza kutolea mifano nchi za Afrika Magharibi).

Kwa kuwa nilishafanya uzembe huo wakati nikiwa shuleni, labda sasa niombe mwenye ujuzi anisadie uelewa! maana nimejuuliza sijapata jibu kwa kweli.
 
Mkuu mi naona hapo kuna ka unafiki kiasi.... Judiciary inajengwa na mkuu wa Executive.... na
hamna ane weza muuliza ni kwa nini umemteu huyu kuwa jaji, kuwa jaji mkuu, kuwa jaji kiongozi kuwa kuwa kuwa.... sasa hapo check and balance iko wapi??
 
Muhimili wenyewe unatakiwa kujipigania na kujitetea kutokuingiliwa kwake, ni kama ubakaji tuu, ukikubali kuingiliwa imekula kwako

Kuna kanuni na taratibu za kufuata, katiba ndio kila kitu, katiba ikiheshimiwa mihimili itaheshimiana, ikishindikana Hapo hamna tena check and balance ila check and fire/hire
 
Muhimili wenyewe unatakiwa kujipigania na kujitetea
Mkuu, sasa kwa kuwa kuna mihimili isiyo na vyombo vya kutumia nguvu na silaha yao ni kujieleza tu, sasa ikidhibitiwa itakuwa je? kwa mfano nilikuwa nafuatilia taarifa nikaona huko Kenya kuna Wakili kauawa pamoja na mteja wake! walichokifanya mawakili wanaandamana (wakiomboleza) lakini najiuliza pia kwa mfano kama wangezuiwa wangefanya je zaidi ya kutulia tu? nafikiri waliotengeneza, au wataalamu wa nadharia hizi hasa Wasomi wa Political Science kuna vitu wanatakiwa watusaidie kwamba ulinzi wa mihimili hii kweli unaweza kuwa "guaranteed" practically kweli! na kivipi? au angalau ni kinadharia zaidi tu na kama ni nadharia, basi kutumaini katika nadharia ambazo practically hazina uhakika nayo inakuwa je?.
 
Wakuu salamu!

Wakati nikiwa shuleni nilibahatika kusoma kidogo siasa. Katika jambo ambalo Mwalimu wangu alinifundisha ni kuwa Nchi za Kidemokrasia zinakuwa na Mihimi Mitatu ya Dola. Akaniambia mmoja unaitwa "Executive" mwingine "Legislature" na wa tatu ni "Judiciary". Akiwa amenikazia macho, huku akiongea kwa ukali kidogo na akionesha kusisitiza akaniambia "Mihimili hii ni kwa ajili ya Check and Balance! . Hakuna muhimili unaotakiwa kwa sababu au kwa namna yeyote kuingilia majukumu ya mwingine. Ni mwiko! kufanya hivyo ni kinyume na Katiba na sheria".

Uzembe ambao niliufanya ni kutokumuuliza kwamba ni nani sasa mwenye wajibu wa kuhakikisha kuwa mihimili hii haiingiliani kimajukumu na kama muhimili mmoja kwa 'Makusudi' ukaamua kufanya kazi za mihimili mingine ni nani mwenye wajibu na nguvu ya kuzuilia hilo lisitokee!? . Au kwa lugha nyingine, kama muhimili mmoja kwa makusudi ukiamua kwenda kinyume na Katiba ni nini cha kufanya na ni nani mwenye wajibu na uwezo wa kufanya? ( tunaweza kutolea mifano nchi za Afrika Magharibi).

Kwa kuwa nilishafanya uzembe huo wakati nikiwa shuleni, labda sasa niombe mwenye ujuzi anisadie uelewa! maana nimejuuliza sijapata jibu kwa kweli.
Pamoja na kuwa mie ni kilaza zaidi ya wote mwenye wajibu wa kuhakikisha hii mihimili haiingiliani ni yule anayetoa PESA. Kama muhimili X unategemea fedha toka Muhimili Y lazima Muhimili X uratibiwe na Muhimili Y. Mengine ni siasa tu
 
Huyo mlw wako alikufundisha kijuujuu sana. Je alikufundisha ukweli kuwa wajumbe wa legislature wa kiamua kumkimbia kiongozi wa mhimili wao, tena kwa akili timamu na hiari yao wenyewe kitakachotokea ni kukosa cha kuwa ambia wanao wawakilisha na kuishia kulalamika kila uchao?
 
Yi Yu She-pig, hapo ndio utaona msingi wa swali la muanzisha mada...ni vile akili zako pia ni made in Hu Ha!

Ikiwa kiongozi wa Legislature katokana na 'Executioners' na anakiuka misingi ya Legislative Council je nani anamuwajibisha nani kuangalia kila mhimili unafanya kazi zake?
 
Back
Top Bottom