Ukikutana naye........UTAMUULIZA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukikutana naye........UTAMUULIZA?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Asprin, Aug 23, 2011.

 1. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Wapendwa marafiki salamu,

  Jana nlimpigia simu rafiki yangu. Alipokea akiwa na simanzi kubwa. Kumbe ndio alikuwa kapokea habari ya msiba wa kaka yake. Alikuwa analia na kuongea kwa shida. Nilihuzunika kwa niaba yake..........kama si nguvu ya Tusker Malt labda nami ningemwaga chozi. Mnywaji mwenzangu akashangaa kwanini nimepata simanzi ya ghafla, nikamsimulia.

  Huyu mtu akaniambia neno ambalo limenifanya nitafakari kwa kina usiku kucha......... Namnukuu: "Ndugu yangu, Mwache Mungu aitwe Mungu na aendelee kukaa hukohuko aliko maana ningepata nafasi ya kukutana naye sasa hivi ningemuuliza KWANINI ULIMCHUKUA BABA YANGU nikiwa bado mdogo nikataabika namna ile?"........ Nilichoka na mpaka sasa nimechoka.....Jamaa alivyonisimulia maisha yake, jinsi mama yake alivyohangaika.......Kweli kila mtu ana swali lake.....Dah!

  Nami najiuliza.... Hivi ningepata nafasi ya kukutana na Mungu akanipa nafasi ya kumuuliza au kumwambia chochote ningemwambia na kumuuliza nini?.....

  Kwanza ningeanza na shukrani:
  Ahsante kwa kuniumba Mwanaume..... manake angeniumba mwanamke ningemuuliza kwanini ameniumba mwanamke.
  Ahsante kwa kunipa mke mzuri (japo kwa ubinadamu wangu huwa natelezaga) na mabinti wawili wazuri.
  Ahsante kwa kunipa wazazi wanaonipenda na kunijali sana
  Ahsante kwa kunipa ndugu, marafiki, majirani tunaoheshimiana na kupendana sana.

  Then lazima ningemuuliza;

  Kwanini tatizo hili limetokea kwenye familia yetu?..... Kwanini kwetu?......... Ningemuuliza mbona kila siku tunakuomba kwenye maombi/sala utuondolee hili tatizo lakini huliondoi?........Lazima ningemuuliza...Niape?

  Kuna mtu mwingine huku angekuwa na Swali kama angekutana na Mungu na kupewa nafasi ya kumuuliza?

  Kama alivyonambia ndugu yangu, mwacheni Mungu aitwe Mungu......... Na aendelee kukaa huko aliko.
  AMINA.

  Leo ODM yuko kimajonzi zaidi.
  Harudi kitandani wala nini. Anajiuliza tu.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  ahhhhh.....ngoja kwanza nitarudi.......
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi nitamuuliza kwa nini watu wengine ni matajiri yaani mtu mwingine toka tumboni mwa mama yake ni full raha na mwingine toka tumboni ni full mahangaiko why?
   
 4. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Babu pole kwa majonzi...........kazi ya Mungu haina makosa
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mhhhh ngoja kwanza nitafakari na nitarudi baadae
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mimi ningemuuliza Mungu una moyo wa namna gani wa kumuacha Asprin aendelee kuwa hai ilihali umempa mke na anateleza na mabinti wengine?
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Angenipa muda zaidi ningemuuliza: Kwanini alikubali nikazaliwa Tanzania?

  Kwanini hakumfanya baba yangu awe Rais wa nchi hii?

  Hakutaka mama yangu awe Firstlady?
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Dah...kweli aisee.... Kwanini aniache nahangaika wakati ana uwezo wa kuilaza baioloji yangu pale naposaula boxer mbele ya binti asiye mke wangu?............Hilo la kuniua ningemuuliza kwanini unamuacha Ezan hai wakati anataka uniue?
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ningemuuliza Mungu je, ana lengo gani na Tanzania? na je Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania ina mzidi nguvu?
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ningemuuliza mengi kwa nini Tanzania ina viongozi legelege na wasiojali maisha ya wananchi wao
  Kwa nini kuna umaskini wa kutisha miongoni wa mwa watanzania
  Kwa nini kuna ugonjwa wa ukimwi na haupati dawa ya uhakika utuache tunajilia tunda kiulaini bila kula na maganda yake
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Kwenye hiyo bold hapo, nadhani angekunasa kibao.... hahahahah

  At least angalau nimefanikiwa kucheka LOL
   
 12. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  ingekuwa kama hapo nilipobold........mimi kalagabaho singekuwa rafiki yako.......
   
 13. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dah! tafakari inahitajika zaidi ngoja nitarudi baada ya muda kidogo.
   
 14. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Mbona una urafiki na Riziwani? Unahisi mi ni katili kihivyo? Ntake radhi.....
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Halafu ningemwambia kwa nini alitufanya tuwe tunavaa nguo angetuacha tuwe tunatembea uchi tukikutana ni kuangushana na kula tunda tuu hakuna kuvuana nguo wala nini
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahaah!! Kwani hii mada ina nini? Mbona wengi mnasema mtarejea!
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mmmh!! Kama kuku??
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Watu wanamwogopa Mungu, lakini hawaogopi kutenda dhambi....Hhahaha....
   
 19. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mhhhh!!!!! Pole sana kwa majonzi babu....kweli kabisa tumwache Mungu aitwe Mungu....
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa....
   
Loading...