JacobMushi
Member
- Sep 18, 2018
- 22
- 30
Tatizo la watu wengi ni hili, wanapokataliwa kwenye maombi ya kazi au watu waliowapenda wanakosa kujiamini wanafikiri hawatapata tena kazi nyingine au mtu mwingine.
Nikwambie, Anza kujitengenezea mtazamo ambao utakufanya uone bado kuna nafasi tena. Ukikataliwa huku uone kuna nafasi nyingine tena kesho mahali Pengine.
Kama yalivyo maisha siku ikiisha inakuja nyingine ndivyo ilivyo katika vitu vingine. Haijalishi siku yako imekwendaje vibaya kiasi gani leo haiwagi kila siku.
Unapokosa jambo ulilokuwa unalitaka sana, au mtu uliekuwa unampenda sana jisemeshe kesho nitakutana na wengine kumi zaidi. Kesho nitakwenda kwenye interviews nyingine kumi tena.
Usikubali Kukata tamaa. Iwe ni biashara, Mahusiano, Kazini, na kila mahali. Kile unachokipenda usikubli kukikatia tamaa.
Endelea Kujaribu ipo siku utakutana na matokeo makubwa.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
#usiishienjiani
#jacobmushi
Sent using Jamii Forums mobile app