Ukikaa na binti aliwahi kuwa mchawi

Ukikaa na binti aliwahi kuwa mchawi

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
783
Msaada kuna binti wa kazi amekuja home katika maelezo yake alikotoka aliwahi kuwa mchawi na Bibi yake lakini aliweka agano la kuacha.

Sisi kama familia tumepiga maombi sana na kuchoma moto vitu vyote na kumnunulia vitu vingine vipya.

Mnashaurije wakubwa nimrudishe kwao au tuendelee na maombi

I am worried sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nae pia mchomeni moto halafu mkanunue beki 3 mpya.
 
Endeeleni na maombi mkuu,msiache na kama inawezekana washirikishe waliojuu kiroho km mchungaji wako nk,maana uchawi haukai kwenye vitu,uko rohoni zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endapo itatokea kila mkiamka asubuhi mnakuta keshamaliza kazi zake zote kabla nyie hamjaamka, basi atakuwa hajaacha mambo yake. Chunguza hilo.
 
Msaada kuna binti wa kazi amekuja home ktk maelezo yake alikotoka aliwah kuwa mchawi na bibi yake lakini aliweka agano la kuacha. Sisi kama familia tumepiga maombi sana na kuchoma moto vitu vyote na kumnunulia vitu vingine vipya. Mnashaurije wakubwa nimrudishe kqao au tuendelee na maombi....i am worried sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unatakiwa kuwa na Imani kwa Mungu wako. Pia usiwe na waswas maana Mungu ndio Kinga yako. Ukimrudisha kwao akiamua kukufanyia mabaya yanaweza kukupata kama ww haupo karibu na Mungu kwa Njia ya Sala.
 
Kama unamwogopa mchawi unahitaji mafundisho zaidi.
Hakuna nguvu kubwa inayoshinda uchawi na majini kama imani ya kuokoka. Wala hakuna hata shida ya kumweka chini ya darubini 24hrs. Akianza uchawi atakimbia yeye. Akiiendelea ataumia.
Inategemea na wewe umejielimisha nini katika Biblia na uaminifu wako katika kuishi sawa na imani yako. Sababu mchaei snajua mlokole feki
 
Kama hajatubu na kubadilishwa kwa nguvu ya Yesu Kristo hakika bado yupo tayari kufanya chochote manake maagano na vifungo vya kichawi bado vinamuandama.

Hakikisheni mnamaliza kabisa kumtoa kwenye uchawi amasivyo anaweza kuwasumbua sana na kama hampo vizuri kiroho atawavuruga vibaya.

Kumfukuza bila kumsafisha nayo yaweza kumpa hasira na akaamua kutumia chochote alicho nacho.

Kwa upendo wa Kristo Yesu msaidieni akomboke kabisa kwani uchawi ni utumwa mbaya sana na wengi waliopo huko wanashindwa kutoka kutokana na maagano na wanateseka sana kama walivyo watumwa.
 
Mkuu! Hata siku moja usiinue majeshi yako kupeleka kwenye vita isiyokuhusu, au vita isiyo na faida.

Na Jemedali bora ni yule anayeingia vitani kwa kuwa ameona kuna uwezekano wa kushinda.

Uyo dogo ni mchawi, hata kama amekwambia aliacha, ipo siku atajikumbushia na wewe na familia ndio mtakuwa victims.

Vinginevyo, bas jiandae kupambana na bibi zake ambao wanakuona wewe ni kauzibe kwa mtu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom