Ukijua nchi inavyoharibiwa unaugua hulali

Ukijua nchi inavyoharibiwa unaugua hulali

Maombolezo ambayo mwisho wake haujulikani utakuwa lini. Nch ina huzuni kubwa sana furaha waliyokuwa nayo Watanzania wengi imetoweka kutokana na udhalimu uliokithiri nchini.

Nchi inaomboleza
 
Miaka 10 ya kilimo kwanza ilitufikisha wap? Nyuma ya kilimo kwanza kulikuwa na sera nyingi tu za kilimo ukizichanganya zote ni Miaka 35+ ya kilimo kupewa kipaumbele na bajeti za kumwaga tuambie kilimo hicho miaka yooote hiyo kimetufikisha wapi?

Kulima huku huna pa kupeleka mazao kwafaa nini kama hakuna viwanda vya kuchakata hayo mazao. Viwanda ndio hamasa ya kilimo na sio serikali.

Sio mambo ya kulima kisha unaililia serikali ikutafutie pa kuuza ulicholima.
 
Mungu yupo na anaona
Tunavyotembea kifua mbele
FB_IMG_1525601167817.jpg
 
ilinishangaza kwa kweli kwani. Kutoongeza mishahara kwa sababu. Ya kutoa elimu. Bure haina Tija kabisa kwani kusomesha kila mtu angepambana na. Hali yake
 
kuwanyima watoto wa wenye leseni za biashara mikopo ya elimu wakati watoto wa wafanyakazi wanapewa ni uendawazimu. kuwa na leseni si uthibitisho wa kipato cha kumudu gharama za elimu. hata kiosk kina leseni. kuna wakulima hawana leseni lakini wana mapato makubwa. hata wauza unga na mafisadi hawana leseni.
 
kila kitu ni....balaaa! mtanyooka mbona? barabara zimejaa tope kama zimemwagiwa urojo wa chocolate.
Hivi kwa nini mkuu. Barabara zina miinuko ya tope na zingine zimechimbika mashimo. Hivi huwezi jua ni za lami kweli?
 
Moja ya masharti yaliyotolewa na Bodi ya Mikopo kwa waombaji wapya ni, ikiwa mzazi wako anamiliki LESENI YA BIASHARA huwezi kupatiwa mkopo.

Wengi wanadhani hilo linatokea kwa bahati mbaya, hapana, serikali yetu imeishiwa hela, kwa ujumla ni kama nchi yetu inafilisika.

Serikali imeshakopa kila mahali ndani na nje, na imekopa kweli kweli, imekopa hadi kuvuka viwango vya mkopo ulioidhinishwa na bunge kwenye bajeti ya 2017/18 kwa zaidi ya nusu trilioni.

Mashirika ya Hifadhi ya jamii yameshakopwa hadi hayajiwezi. Mabenki ya ndani yaliyopaswa kukopesha Raia yamekuwa "disturbed" na yametishwa na sasa yanaikopesha zaidi serikali kuliko raia (ni mkakati wa kuinusuru dola ya CCM).

Tunafahamu kuwa bajeti ya mwaka jana haikutekelezeka kwa zaidi ya asilimia 50 (chukulia tu mfano wa bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji ambayo ilipewa asilimia 22 tu ya fedha zilizopitishwa. Serikali haina pesa!

Makusanyo ya fedha za kigeni yameanguka kabisa, bei ya mazao ya biashara imeanguka vibaya, thamani ya shilingi inaporomoka, wastaafu wananyimwa hela zao zilizoko kwenye mifuko ya pensheni, wafanyakazi wamenyimwa ongezeko la mshahara hata lile la kila mwaka ambalo lipo kisheria (statutory annual increament).

Manispaa na halmashauri zimebanwa, mfano hivi sasa barabara nyingi za mitaani ni mashimo na mahandaki, fedha za ujenzi wa barabara zimechukuliwa na serikali kuu kutoka serikali za mitaa, zimewekwa TARURA...nina taarifa kwamba huko TARURA hazitoki kirahisi kurudi kutengeneza barabara, haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi.

Halmashauri na manispaa huko nyuma zilikuwa zinakusanya fedha kwenye majengo n.k. Serikali Kuu imepora vyanzo vyote hivyo, halmashauri zimebaki zinashangaa. Zenyewe ndizo hushughulika na masuala ya moja kwa moja ya wanachi na ndizo ziko karibu ma watu na kwa kiasi kikubwa husimamia maendeleo ya WATU siyo VITU - hazina hela.

Hela zote zinapelekwa serikali kuu, zinanunua Bombardier's na Boeing's na kujenga viwanja vya ndege maeneo kama CHATO na madudu mengine mengi. Zinashughulika na maendeleo ya VITU ambavyo kwa kiasi kikubwa vitu hivyo havitakuwa na tija kwa asilimia 90 ya wana taifa (wapo watakaoelewa hili baada ya miaka 5 au 10).

Sasa hivi kila senti tano inapelekwa Serikali kuu na Bwana Mkubwa ndiye anayeamua kila jambo....jenga makao makuu Dodoma, Jenga reli ya umeme, jenga bweni hapa, hamisha hela za kujenga bweni kule wapelekee wale, mpe huyu hela hizi...n.k.

Amri zote hizo kwa kiasi kikubwa siyo utekelezaji wa bajeti iliyopitishwa na bunge, ni bajeti za mkubwa. Mfano, Bunge kwenye bajeti ya 2017/18 halikutenga fedha za kujenga uwanja wa ndege Chato, lakini cha ajabu uwanja umejengwa kwa shilingi bilioni 38 na naambiwa mabilioni zaidi yanaendelea kupelekwa huko. Uwanja umejengwa mahali ambako hauwezi kuwa na tija yoyote.

Sekta za kukuza maendeleo ya WATU kama sekta ya Kilimo, zimetupwa. Kwa sasa kilimo kinategemewa na asilimia 75 ya watanzania wote. Nchi zote zilizokuza uchumi wake duniani ziliwekeza fedha nyingi zaidi kwenye sekta ambayo inategemewa na watu wengi zaidi.

Kwenye Bajeti ya Mwaka huu 2018/19 serikali imetenga Shilingi Bilioni 11 kukuza kilimo na Shilingi Bilioni 495 kununua ndege moja mpya ya Boeing! Ndege hii moja (na kwa biashara ya ndege ilivyo) ni ndege itakayotuletea hasara mpya kila mwaka (Rejea hasara ya Shilingi Bilioni 223 tuliyoipata kwa kusimamia uendeshaji wa Bombardier mbili kwa miaka miwili 2016 - 2017.)

Lakini leo tumekitupa kilimo ili tununue ndege ili tupate sifa kuwa tulinunua ndege. Tumekosa vipaumbele na hatujui tunataka nini, wakati gani.

Tuendako ni kubaya zaidi kuliko tunakotoka. Mpaka siku watanzania watajua mapambano ya kudai nchi yao halisi ni mapambano ya kila mmoja, tutakuwa tumeumizwa vibaya sana.

Haya ya bodi ya mikopo ni mfano tu wa namna nchi inavyohama kwenye mstari. Inavyong'ang'ana kushughulikia maendeleo ya vitu huku watu wakiendelea kuporomoka kabisa, hadi siku tutakapojua tumefilisika.
Uongozi duni ndiyo hulka yetu
 
Miaka 10 ya kilimo kwanza ilitufikisha wap? Nyuma ya kilimo kwanza kulikuwa na sera nyingi tu za kilimo ukizichanganya zote ni Miaka 35+ ya kilimo kupewa kipaumbele na bajeti za kumwaga tuambie kilimo hicho miaka yooote hiyo kimetufikisha wapi?

Kulima huku huna pa kupeleka mazao kwafaa nini kama hakuna viwanda vya kuchakata hayo mazao. Viwanda ndio hamasa ya kilimo na sio serikali.

Sio mambo ya kulima kisha unaililia serikali ikutafutie pa kuuza ulicholima.
NduGu yangu sijui kiwango chako cha elimu lkn ktk hik ulchochangia ni wazi hujui vigezo vinavyotumika ili kiwanda kijengwe mahal fulan..! Moja ya kigezo kikubwa ni upatikanaji wa malighafi... Hivyo ni muhim kuwekeza ktk kilimo na viwanda vitajileta vyenyewe kufuata malighafi.

Wakati mwingine tuzungumze facts sio fictious kila siku. Ni mwekezaji gani atachukua mkopo wenye riba ajenge kiwanda cha nguo badala ya kuanza uzalshaji yeye aanze kuhamasisha watu kulima pamba..?

Mkoa wa Geita kuna maeneo kunalimwa nanasi nyingi sana. Kisiasa inatosha kuweka kiwanda cha Juice lakn tathmin iliyofanyika kibiashara inaonyesha nanasi zote zinaweza kuliwa na kiwanda kimoja cha kati kwa mwezi mmoja tu zikaisha zisipatikane kabsa kwa walaji wa kawaida.

Hivyo hakuna mwekezaji yeyote anayeweza kujenga kiwanda cha Juice nchini kwa kutegemea matunda yetu tunayozalisha Tanga na Geita bila kuagiza cyrup nje... bila kilimo kuimarika SGR ni White Elephant..!
 
Mmmmmmhhhh...😳🙁😱😱 vyuma vimekazaaa vibaya i can see
 
Miaka 10 ya kilimo kwanza ilitufikisha wap? Nyuma ya kilimo kwanza kulikuwa na sera nyingi tu za kilimo ukizichanganya zote ni Miaka 35+ ya kilimo kupewa kipaumbele na bajeti za kumwaga tuambie kilimo hicho miaka yooote hiyo kimetufikisha wapi?

Kulima huku huna pa kupeleka mazao kwafaa nini kama hakuna viwanda vya kuchakata hayo mazao. Viwanda ndio hamasa ya kilimo na sio serikali.

Sio mambo ya kulima kisha unaililia serikali ikutafutie pa kuuza ulicholima.

Mzee kiwanda bila kua na mazao ni sawa na kujenga nyumba bila kiwanja kwa dangote atengenezi cement kwann unajua viwanda vingi vimekufa kwann mahindi yanapigwa marufuku kuuzwa kenya na kwingineko coz uchache alafu uanzishe kiwanda cha unga wakati mahindi shida tunaimba viwanda alafu general tyre imetushinda kufufua tu viwanda vya nguo vimetushinda nadha tunafeli sio kisa mzungu ni tamaa ya wanaotuongoza wanataka waishi maisha mazur wenyewe
 
Back
Top Bottom