Naunga mkono hojaNaangalia uwezekano wa kufungua biashara Zambia. Nasikia kuna grace period ya miezi 3 ndo unakadiriwa kodi.
Yani wapo fair. Tukapige kwacha Zambia.
Halafu hapa tukiwa na Leseni za biashara watoto wetu hawapewi mikopo ya elimu ya chuo kikuu.
Twende nje ya nchi.
freebasics ni bure! labda anatumia hiyo!mambo mabaya ila hukosi hela ya bandle!
Miaka 10 ya kilimo kwanza ilitufikisha wap? Nyuma ya kilimo kwanza kulikuwa na sera nyingi tu za kilimo ukizichanganya zote ni Miaka 35+ ya kilimo kupewa kipaumbele na bajeti za kumwaga tuambie kilimo hicho miaka yooote hiyo kimetufikisha wapi?
Kulima huku huna pa kupeleka mazao kwafaa nini kama hakuna viwanda vya kuchakata hayo mazao. Viwanda ndio hamasa ya kilimo na sio serikali.
Sio mambo ya kulima kisha unaililia serikali ikutafutie pa kuuza ulicholima.[/QUOTE
Sio kosa Lako
Umeeleza utumbo utumbo utumbo...hivi unajua Principle za Uchumi.. daaaa.. hivi huwa mnakaa chini na kutunga uozo kama huu ili usaidie nini...hivi unajua Tanzania ina foreign reserve ya kiasi gani.. hivi unajua Operating capital iliyopo kwa sasa ukilinganisha na awamu za serikali zilizopita.. kwanza umefanya research ili kuweza kufanya majumuisho uliyoyatoa..? Mama nakuruhusu nenda kafanye tafiti kwanza kabla hujatuletea huu uharo..ni hayo tu mama.Moja ya masharti yaliyotolewa na Bodi ya Mikopo kwa waombaji wapya ni, ikiwa mzazi wako anamiliki LESENI YA BIASHARA huwezi kupatiwa mkopo.
Wengi wanadhani hilo linatokea kwa bahati mbaya, hapana, serikali yetu imeishiwa hela, kwa ujumla ni kama nchi yetu inafilisika.
Serikali imeshakopa kila mahali ndani na nje, na imekopa kweli kweli, imekopa hadi kuvuka viwango vya mkopo ulioidhinishwa na bunge kwenye bajeti ya 2017/18 kwa zaidi ya nusu trilioni.
Mashirika ya Hifadhi ya jamii yameshakopwa hadi hayajiwezi. Mabenki ya ndani yaliyopaswa kukopesha Raia yamekuwa "disturbed" na yametishwa na sasa yanaikopesha zaidi serikali kuliko raia (ni mkakati wa kuinusuru dola ya CCM).
Tunafahamu kuwa bajeti ya mwaka jana haikutekelezeka kwa zaidi ya asilimia 50 (chukulia tu mfano wa bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji ambayo ilipewa asilimia 22 tu ya fedha zilizopitishwa. Serikali haina pesa!
Makusanyo ya fedha za kigeni yameanguka kabisa, bei ya mazao ya biashara imeanguka vibaya, thamani ya shilingi inaporomoka, wastaafu wananyimwa hela zao zilizoko kwenye mifuko ya pensheni, wafanyakazi wamenyimwa ongezeko la mshahara hata lile la kila mwaka ambalo lipo kisheria (statutory annual increament).
Manispaa na halmashauri zimebanwa, mfano hivi sasa barabara nyingi za mitaani ni mashimo na mahandaki, fedha za ujenzi wa barabara zimechukuliwa na serikali kuu kutoka serikali za mitaa, zimewekwa TARURA...nina taarifa kwamba huko TARURA hazitoki kirahisi kurudi kutengeneza barabara, haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi.
Halmashauri na manispaa huko nyuma zilikuwa zinakusanya fedha kwenye majengo n.k. Serikali Kuu imepora vyanzo vyote hivyo, halmashauri zimebaki zinashangaa. Zenyewe ndizo hushughulika na masuala ya moja kwa moja ya wanachi na ndizo ziko karibu ma watu na kwa kiasi kikubwa husimamia maendeleo ya WATU siyo VITU - hazina hela.
Hela zote zinapelekwa serikali kuu, zinanunua Bombardier's na Boeing's na kujenga viwanja vya ndege maeneo kama CHATO na madudu mengine mengi. Zinashughulika na maendeleo ya VITU ambavyo kwa kiasi kikubwa vitu hivyo havitakuwa na tija kwa asilimia 90 ya wana taifa (wapo watakaoelewa hili baada ya miaka 5 au 10).
Sasa hivi kila senti tano inapelekwa Serikali kuu na Bwana Mkubwa ndiye anayeamua kila jambo....jenga makao makuu Dodoma, Jenga reli ya umeme, jenga bweni hapa, hamisha hela za kujenga bweni kule wapelekee wale, mpe huyu hela hizi...n.k.
Amri zote hizo kwa kiasi kikubwa siyo utekelezaji wa bajeti iliyopitishwa na bunge, ni bajeti za mkubwa. Mfano, Bunge kwenye bajeti ya 2017/18 halikutenga fedha za kujenga uwanja wa ndege Chato, lakini cha ajabu uwanja umejengwa kwa shilingi bilioni 38 na naambiwa mabilioni zaidi yanaendelea kupelekwa huko. Uwanja umejengwa mahali ambako hauwezi kuwa na tija yoyote.
Sekta za kukuza maendeleo ya WATU kama sekta ya Kilimo, zimetupwa. Kwa sasa kilimo kinategemewa na asilimia 75 ya watanzania wote. Nchi zote zilizokuza uchumi wake duniani ziliwekeza fedha nyingi zaidi kwenye sekta ambayo inategemewa na watu wengi zaidi.
Kwenye Bajeti ya Mwaka huu 2018/19 serikali imetenga Shilingi Bilioni 11 kukuza kilimo na Shilingi Bilioni 495 kununua ndege moja mpya ya Boeing! Ndege hii moja (na kwa biashara ya ndege ilivyo) ni ndege itakayotuletea hasara mpya kila mwaka (Rejea hasara ya Shilingi Bilioni 223 tuliyoipata kwa kusimamia uendeshaji wa Bombardier mbili kwa miaka miwili 2016 - 2017.)
Lakini leo tumekitupa kilimo ili tununue ndege ili tupate sifa kuwa tulinunua ndege. Tumekosa vipaumbele na hatujui tunataka nini, wakati gani.
Tuendako ni kubaya zaidi kuliko tunakotoka. Mpaka siku watanzania watajua mapambano ya kudai nchi yao halisi ni mapambano ya kila mmoja, tutakuwa tumeumizwa vibaya sana.
Haya ya bodi ya mikopo ni mfano tu wa namna nchi inavyohama kwenye mstari. Inavyong'ang'ana kushughulikia maendeleo ya vitu huku watu wakiendelea kuporomoka kabisa, hadi siku tutakapojua tumefilisika.
Zitto alimaanisha yale yenye akili yaliyokaa pembeni ndio yale mafisadi papa yanayoitafuna nchi hii..shwain..wacha yaendelee kukaa pembeni, wacha hao wajinga wanaipambana na mafisadi waendelee kushika usukani hata milele na milele..tutavumilia tuu..tupo tayari...msikae mkategemea kuna nafasi ya kufisadi tena na kupiga mahela...hahahah..hao wenye akili wengine ndio wale waliofisadi mabilioni ya pesa ndani ya vyama vyetu hivihivi vya upinzani...na refer ripoti ya CAG. Eti ukiwa unajua kupiga hela ya wizi ndio unaitwa mwenye akili...hhahahah endeleeni tu..lakini nafurahi mwisho wenu unafika taratibu..mmoja baada ya mwingine..mtanyooka tuu..shwainnJiwe Penda Misifa ashajichanganya. Naye analijua hilo ameshaharibu sana. Alianza kwa nyodo sana, sasa ataomba poo!
Zitto aliwahi kusema Washamba na Malimbukeni ndiyo wameshika usukani wa nchi wenye akili wako pembeni wanatizama tu, maana wakitia neno wanaitwa wachochezi.
Cha Pombe alipomwona mwenzie Kagame ana midege akadhani ni kwa mtindo huo, hajui Rwanda baada ya Kagame kuingia, alianza kilimo kama kipa umbele. Kahawa ya Rwanda ina thamani kubwa ulimwenguni kulinganisha na ya Tanzania hata Uganda. Chai ya Rwanda kila stores Ulaya na USA hukosi kuiona kwenye shelves sijawahi ona chai ya Tanzania ila siku moja niliona Chocolate toka Tanzania kwenye sehemu ya Agoa. Rwanda iligawa ng'ombe mmoja kwa kila kaya maskini, sisi tunategemea wafadhiri wainject pesa kwenye tasaf ndo watu wasaidiwe tena pesa badala ya kuinvest kwenye kitu kitakachowasaidia. SNV ilikuwa imeanzisha mpango wa kuwapa wakulima mifugo ili wanapozalisha inarotate. Watu walinufaika ingawa nao haukudumu. That was in late 90s.
Rwanda, Kenya, Uganda ndio wasafirishaji wakubwa wa mazao ya kilimo hapa East Afrika. Nenda Leads market unakutana na matoke, yarms mpaka kisamvu toka Uganda na Rwanda. Je sisi kwa nini hatujaribu? Wawakilishi wetu meaning mabalozi hawana time ya kutembea kuona kipi tunaweza kutrade na wenzetu kazi ni kuchunguza watanzania wanaoandika mitandaoni. Ndizi za Rwanda za kuexport zinaandaliwa zikianza kuzaa, zinavalishwa plastic lenye dawa ili wadudu wasiziingilie mpaka zinakuwa tayari kusafirishwa. Sisi huko Bukoba ndizi mpaka zimeisha mashambani serikali haina mpango wa kutibu mnyauko. Pesa ambazo tungewekeza kutibu wadudu ili tupate hata chakula cha kutututosha zinaenda kwenye Bombadia. Wanaoumia ni wengi kuliko wanaosifia. Hata hao siyo kwamba koo zao zote zinafaidi kwa kuzipanda na kula pesa za Bombadia ila huko vijijini ni shida ila wamebaki na kofia, khanga na tshirts. Kidumu.
Hujui nimetumia kifaa gani kupost. Anyway umeshasema sasa kimya kimya ya nini. Siyo kila mtu asome. Wenye akili kama zangu watasoma wewe genius pita tu.Jifunze kutumia paragraphs jombaa.
Binafsi nimeshindwa kuisoma japo inawezekana post yako imejaa madini. Usinishambulie kwa mitusi - ichukulie tu kama ushauri na ilifanyie kazi kimya kimya.
yani hadi naogopa kulala peke yangu.Moja ya masharti yaliyotolewa na Bodi ya Mikopo kwa waombaji wapya ni, ikiwa mzazi wako anamiliki LESENI YA BIASHARA huwezi kupatiwa mkopo.