Ukijua nchi inavyoharibiwa unaugua hulali

Ukijua nchi inavyoharibiwa unaugua hulali

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Moja ya masharti yaliyotolewa na Bodi ya Mikopo kwa waombaji wapya ni, ikiwa mzazi wako anamiliki LESENI YA BIASHARA huwezi kupatiwa mkopo.

Wengi wanadhani hilo linatokea kwa bahati mbaya, hapana, serikali yetu imeishiwa hela, kwa ujumla ni kama nchi yetu inafilisika.

Serikali imeshakopa kila mahali ndani na nje, na imekopa kweli kweli, imekopa hadi kuvuka viwango vya mkopo ulioidhinishwa na bunge kwenye bajeti ya 2017/18 kwa zaidi ya nusu trilioni.

Mashirika ya Hifadhi ya jamii yameshakopwa hadi hayajiwezi. Mabenki ya ndani yaliyopaswa kukopesha Raia yamekuwa "disturbed" na yametishwa na sasa yanaikopesha zaidi serikali kuliko raia (ni mkakati wa kuinusuru dola ya CCM).

Tunafahamu kuwa bajeti ya mwaka jana haikutekelezeka kwa zaidi ya asilimia 50 (chukulia tu mfano wa bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji ambayo ilipewa asilimia 22 tu ya fedha zilizopitishwa. Serikali haina pesa!

Makusanyo ya fedha za kigeni yameanguka kabisa, bei ya mazao ya biashara imeanguka vibaya, thamani ya shilingi inaporomoka, wastaafu wananyimwa hela zao zilizoko kwenye mifuko ya pensheni, wafanyakazi wamenyimwa ongezeko la mshahara hata lile la kila mwaka ambalo lipo kisheria (statutory annual increament).

Manispaa na halmashauri zimebanwa, mfano hivi sasa barabara nyingi za mitaani ni mashimo na mahandaki, fedha za ujenzi wa barabara zimechukuliwa na serikali kuu kutoka serikali za mitaa, zimewekwa TARURA...nina taarifa kwamba huko TARURA hazitoki kirahisi kurudi kutengeneza barabara, haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi.

Halmashauri na manispaa huko nyuma zilikuwa zinakusanya fedha kwenye majengo n.k. Serikali Kuu imepora vyanzo vyote hivyo, halmashauri zimebaki zinashangaa. Zenyewe ndizo hushughulika na masuala ya moja kwa moja ya wanachi na ndizo ziko karibu ma watu na kwa kiasi kikubwa husimamia maendeleo ya WATU siyo VITU - hazina hela.

Hela zote zinapelekwa serikali kuu, zinanunua Bombardier's na Boeing's na kujenga viwanja vya ndege maeneo kama CHATO na madudu mengine mengi. Zinashughulika na maendeleo ya VITU ambavyo kwa kiasi kikubwa vitu hivyo havitakuwa na tija kwa asilimia 90 ya wana taifa (wapo watakaoelewa hili baada ya miaka 5 au 10).

Sasa hivi kila senti tano inapelekwa Serikali kuu na Bwana Mkubwa ndiye anayeamua kila jambo....jenga makao makuu Dodoma, Jenga reli ya umeme, jenga bweni hapa, hamisha hela za kujenga bweni kule wapelekee wale, mpe huyu hela hizi...n.k.

Amri zote hizo kwa kiasi kikubwa siyo utekelezaji wa bajeti iliyopitishwa na bunge, ni bajeti za mkubwa. Mfano, Bunge kwenye bajeti ya 2017/18 halikutenga fedha za kujenga uwanja wa ndege Chato, lakini cha ajabu uwanja umejengwa kwa shilingi bilioni 38 na naambiwa mabilioni zaidi yanaendelea kupelekwa huko. Uwanja umejengwa mahali ambako hauwezi kuwa na tija yoyote.

Sekta za kukuza maendeleo ya WATU kama sekta ya Kilimo, zimetupwa. Kwa sasa kilimo kinategemewa na asilimia 75 ya watanzania wote. Nchi zote zilizokuza uchumi wake duniani ziliwekeza fedha nyingi zaidi kwenye sekta ambayo inategemewa na watu wengi zaidi.

Kwenye Bajeti ya Mwaka huu 2018/19 serikali imetenga Shilingi Bilioni 11 kukuza kilimo na Shilingi Bilioni 495 kununua ndege moja mpya ya Boeing! Ndege hii moja (na kwa biashara ya ndege ilivyo) ni ndege itakayotuletea hasara mpya kila mwaka (Rejea hasara ya Shilingi Bilioni 223 tuliyoipata kwa kusimamia uendeshaji wa Bombardier mbili kwa miaka miwili 2016 - 2017.)

Lakini leo tumekitupa kilimo ili tununue ndege ili tupate sifa kuwa tulinunua ndege. Tumekosa vipaumbele na hatujui tunataka nini, wakati gani.

Tuendako ni kubaya zaidi kuliko tunakotoka. Mpaka siku watanzania watajua mapambano ya kudai nchi yao halisi ni mapambano ya kila mmoja, tutakuwa tumeumizwa vibaya sana.

Haya ya bodi ya mikopo ni mfano tu wa namna nchi inavyohama kwenye mstari. Inavyong'ang'ana kushughulikia maendeleo ya vitu huku watu wakiendelea kuporomoka kabisa, hadi siku tutakapojua tumefilisika.
 
Naangalia uwezekano wa kufungua biashara Zambia. Nasikia kuna grace period ya miezi 3 ndo unakadiriwa kodi.
Yani wapo fair. Tukapige kwacha Zambia.
Halafu hapa tukiwa na Leseni za biashara watoto wetu hawapewi mikopo ya elimu ya chuo kikuu.

Twende nje ya nchi.
 
Mishahara jamaa kagoma kuongeza kwa madai kuwa mpaka amalize miradi mikubwa........

Tafsiri ya hiyo no kuwa alichotuambia in kuwa tutasubiri hadi mwisho wa dunia bila nyongeza ypyote ya mishahara!
 
Ili ufungue kiosk /duka la rejareja
1. Kujadili maombi yako serikali ya Kijiji / Kata - 50,000/=

2. Leseni ya biashara - 50,000/= nakuendelea

3. TRA - 150,000/=

Hapo bado TFDA kama utauza vinywaji Kama soda na juice ndogondogo kwa rejareja. Hukiuza mchele + maharage kwa rejareja unao.

Kweli miradi inatekelezwa na tunaona, ila mnatukamua Kweli Kweli.
 
Ni kweli hakuna fedha,ila wasitafu wanapewa haki yao
 
Naangalia uwezekano wa kufungua biashara Zambia. Nasikia kuna grace period ya miezi 3 ndo unakadiriwa kodi.
Yani wapo fair. Tukapige kwacha Zambia.
Halafu hapa tukiwa na Leseni za biashara watoto wetu hawapewi mikopo ya elimu ya chuo kikuu.

Twende nje ya nchi.
Zambia, Mozambique, Kenya, Uganda kunafaa mzunguko upo vizuri
 
Jiwe Penda Misifa ashajichanganya. Naye analijua hilo ameshaharibu sana. Alianza kwa nyodo sana, sasa ataomba poo!

Zitto aliwahi kusema Washamba na Malimbukeni ndiyo wameshika usukani wa nchi wenye akili wako pembeni wanatizama tu, maana wakitia neno wanaitwa wachochezi.
 
Back
Top Bottom