Ukijifanya kujua sana ipo siku utaaibika kama huyu jamaa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukijifanya kujua sana ipo siku utaaibika kama huyu jamaa!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by suleym, Jul 6, 2011.

 1. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  kuna watu wakiwa ndani ya vyombo vya usafiri ni watu wanaopenda kujionyesha wanajua kila kitu kwa huongea kwa sauti ya juu sana hadi kuwakera jirani zao. kuna jamaa mmoja alikuwa akisafiri kutokea jjijini dsm kwenda arusha bwana huyu alikuwa ni aina ya wale watu wanaopenda sifa sana mara atoe simu na akiongea ni kwa sauti ya juu sana.

  akiwa ndani ya basi alianza kumtolea maneno makali kondakta wa basi lile akimwambia amwambie dereva aongeze mwendo wa gari kwani aliona mwendo ulikuwa wa taratibu sana (ilikuwa kama km 80 au 100/hr), kondakta alionekana kupuuza ombii la yule bwana, jamaaa akaendelea kumsisistiza amwambie dereva aongeze mwendo kuna mambo muhimu anawahi huku anakokwenda (arusha).

  baada ya kuuona kondakta anayapuuza maombi yake akaanza kupaza sauti kwa dereva akimtaka aongeze mwendo aachane na mwendo wa kinyonga yaani km 80/hr! dereva nae akaweka pamba masikioni jamaa akaaza kulaani kwa nn kapanda basi bovu kama lile linakwenda kama linapeleka msiba akaapa safari nyingine halipandi. gari linaingia mombo abiria wanashuka kupatA chakula na kujisaidia, jamaa nae akashuka akiwa amenuna! akanunua chips na vipande vya kuku akala safari ikaendelea mara jamaa tumbo likaanza kumchafuka akahisi kutaka kwenda haja kubwa akamwita konda amwambie dereva asimamishe akajisaidie lahaula! konda akamjibu watachelewa safari akamuuliza wewe si ndo uliilkuwa ukisisitiza mwendo uongezwe unachelewa kufika sasa tukisimsimama si ndo tutachelewa zaidi na akamalizia kwa kumwambia tulia utajisaidia ukifika tunataka tukuwahishe safari yako!

  Alipoona konda amekataa kumwambia dereva akaamua kusimama yeye mwenyewe akamwambie dereva asimamishe gari, mpaka kufikia hatua hiyo "mzigo" ulikuwa karibu kushuka akapiga hatua kadhaa kuelekea kwa dereva akaanza kumuomba asimame, konda akamwambie dereva huyu ndo mheshimiwa alikuwa akkikwambia unakwenda mwendo wa konokono, sasa dereva akaanza kulichochea gari na akisisitiza wanataka kumwahisha arusha jamaa kwa hasira akaanza kufoka akajisahau kuwa MZIGO uko karibu mara harufu ikajaa ndani ya gari jamaa kashusha mzigo abiria wakaanza kulalamika wamshushe jamaa akashushwa akiwa na begi lake mkononi akiwa amefadhaika sana, akawa anakwenda uelekeo usioeleweka na akaapa kutorudi kwenye lile basi akatokomea vichakani akamaliza mambo yake na akabadili na nguo akawa safi tena.

  sasa akawaza arudi barabarani akasimamishe basi jengine maraakatokea barabarani Mungu shukuru hakutumia muda mrefu akaona basi linakuja kwa mbele yake alikotokea barabarani akalisimamisha likasimama, kuingia ndani kumbe ni basi lilellie alikuwa amepanda mwanzo na alipokelewa kwa maneno makali na shutuma nzito kutoka kwa abiria waliotumia muda mwingi kumsubiri barabarani, kwa aibu aliyokuwa nayo alipofika same akashuka akijidai ndo mwisho wa safari yake ilihali alikuwa anakwenda arusha. kisa hiki ni cha kweli kabisa na jamaa aliepatwa na kisa hiki aliapa kutokuwa msema hovyo wala kulakula hovyo.
   
 2. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  Hadithi...uongo...kolea!
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Haki za Binadamu zimekiukwa na watumishi wa hilo Basi, hata kama Jamaa alikuwa anawatukana lakini hawakupaswa kumfanya adhalilike kiasi hicho.. Wote wamekosa Busara!!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aaaah,jamani misos na safari........
   
 5. M

  Malk Mush Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh hiyo ni hadithi au kweli
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Nisingesoma hii post yako ningeandika hivyo hivyo. Kuna mama mmoja alilipwa M1 kwa kosa kama hili yeye basi lake lilikuwa linaelekea Mbeya kamwambia dreva simamisha nijisaidie tumbo limechafuka wakakataa akajisaidia kumbe ndani kulikuwa na mwanasheria na polisi wewe kulizuka balaa walimlipa kwa kukiuka haki za binadamu ni kosa kubwa sana
   
 7. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hao nao wamekosa utu yaani wamfanyie hivyo abiria eti kisa kawatukana. Jamaa kweli aliwakosea lakini walichomfanyia sio issue kabisa. Hata hao abiria nao wana tabia mbaya, wangemsaidia kwanza mwenzao halaf baadae ndo wakamkemea kuliko kuwaacha huyo konda na dereva wake wamdhalilishe mwenzao.
   
 8. serio

  serio JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  atakua mkali wa kuleeee, kagera..!!
   
 9. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haa haaaa, una visa weweee!
   
Loading...