ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,543
- 21,551
Hiyo ilikuwa ni kauli ya mwamba mmoja ambaye nimekutana nae asubuhi hii Kwa mama lishe.
Kwa kawaida mwandishi yoyote Yule huwa anaandika kutokana na mambo anayokutana nayo kila siku, mwengine huandika kutokana na uzoefu wa Maisha yake na mwengine huandika story za kutunga kama hadthi, Ila Mimi mara nyingi huandika kutokana na matukio ambayo huwa nakutana nayo katika Maisha.
Sasa Leo asubuhi nikiwa napata chai Kwa mama lishe, mara paap kuna mwamba akaja kukaa katika meza niliyo kaa Mimi, baada ya kuagiza chai yake na chapati kama tano na maharage, akaambiwa na mama lishe maji ya kunawa yapo pale, mwamba akasema haina haja ya kunawa kwani anajiamini yupo Safi.
Ndio nami ikabidi nishiriki Yale mazungumzo, nikamwambia mwamba " lakini unajua kunawa ni muhimu Sana kwani mikono yetu inashika mambo mengi Sana" mwamba akasema "ukijiamini haupati Maradhi"
Nikiwa katika Hali ya kupatwa na mshangao juu ya kauli ya jamaa, ikabidi nimuulize tena Yule mwamba "ulipokuja hapa vipi umepanda daladala?" Akajibu ndio, nikaendelea kumwambia mkuu umeshika viti na bomba katika daladala kila mtu anashika pale uwezekano WA kuacha bacteria wanao sababisha maradhi mbali mbali ni Mkubwa mno hivyo kunawa ni Jambo la msingi Sana.
Mwamba huku akianza kukuta chapati yake Bila kunawa akasisitiza kwakusema Sisi ngozi nyeusi tupo imara Sana ni wazungu Tu wanatudanganya na Mimi najiamini Sana na unajua ukijiamini haupati Maradhi kabisa.
Huyu mwamba nilimkubali Kwa kujiamini na kusimamia misimamo yake ingawa Kwa upande mwengine sikumkubali Kwa kulichukulia Jambo la afya kimchezo mchezo, sijui alipata wapi hiyo elimu ya afya ambayo inamwambia akijiamini basi hapati maradhi.
Je, ni huenda kwa kuwa na watu kama hawa ndio kumefanya COVID 19 isituchape Sana wabongo coz ilijua hatuiogopi hivyo ikaamua kupunguza makali yake? Au ni kweli Sisi waafrika tuna ngozi ngumu?
Baada ya kumaliza kifungua kinywa changu nikaondoka na kumwacha Yule mcuba akiendelea kupata chai yake taratibu Bila wasi wasi wowote ule.
Ni hayo Tu!