Ukiegesha gari vibaya, faini kwa gari ndogo ni Tsh 200,000 na Tsh 10,000 ni gharama ya gari kulala yard kwa siku moja

Hawa jamaa walishawahi niotea pale Sinza Mugabe, tena hii barabara mpya muwe makini sana kuna vibao kabisa vya parking kwa gari ndogo kubwa etc.. sasa mm nilisimama kweli kwenye kituo cha daladala nanunua kitu fasta dukani, ghafla wakavamia gari nilivyoenda tukaanza kubishana bishana pale mwisho tukaenda kwenye yard yao pale magomeni usalama hapo hata sijui kama fine yao ni laki mbili, mara baada ya kuanza kujaza kale kaform ndiyo nikaona hiyo figure nikasema hapa siwezi lipa hii hela yote. Ikabidi na mm sasa nitumie nguvu yangu zikapigwa simu pale nikaona ghafla wanaanza kuniita kiongozi , mwisho wa siku nikaishia kuwaachia elfu kumi tu hiyo ya parking sijui nayo waliomba nikaona siyo case. All in all wamerudi kwa kishindo sana hawa jamaa especially hii manispaa ya Ubungo, kama umepark sehemu siyo washa double hazard...ikiwezekana weka na triangle kabisa
Inasaidia ondoa wrong parking ila inabidi watoe hata dakika 5
 
Back
Top Bottom