Ukiegesha gari vibaya, faini kwa gari ndogo ni Tsh 200,000 na Tsh 10,000 ni gharama ya gari kulala yard kwa siku moja

Mama sio mpigaji ila kafungua nchi ili wapigaji waendelee na upigaji
Mkuu ni kweli kabisa, km jana nimeona jamaa wa OilCom wamechukua kijiwe chote, sijui ni mwenge kule eti na gari zote wamepelekwa Polisi kuzuiliwa
hao Waarabu enzi za Jiwe wasingetamba hata dakika
sasa mwenye nacho na hasa hawa walio ,...........
 
Iliwahi tokea morogoro alphard ili kuwa imepark wrong parking maeneo ya juwata, tarura hao wakajitia kiherehere wakatia ile triangle yao, ghafla hawajamalizia vizur, wakaona jamaa anakuja na mabaka afu mabegan amechafuka nyota za kutosha, ilibidi wawe wapole wakamwachia pasipo kuongea chochote
 
Hahaha ukawapa 60 yao tu! Dah ni noma kweli sema usawa huu bora sitembei na gari maana watakuwa wapo kila mahali
Ukija huku mbezi Stend, njoo nalo mzee, huku kuna hesabika nje kidogo ya Mji wa Dar, hivyo kuna baathi ya mambo hatupangiwi.
 
Unafanya mambo kwa kuzowea. Kama eneo halina maegesho rasmi, basi haliruhusiwi.
Sjui kama wewe ni mkazi wa Dar, aua la, kama ni mkazi wa Dar, Kwa mfano huku mbezi mwisho, maegesho rasmi yako wapi, yanayoendana mahitaji yanayopatikana huko. Ni Uonevu Watu wanakufidhia, ili wakunyang'anye fedha zako, Kama umesoma uderefa sehemu zote zisizoruhusiwa kupaki, huwekwa kibao, kinachokataza kupaki.
 
Miliki gari ukiwa na hela uache kupiga kelele

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijakuelewa hivyo ukiwa na hela, ndiyo unatakiwa kuziachia achia tu, Hivi kama kiasi walichotakiwa kulipa, we unawaambiaje hawana hela.
Ukiona mtu anamiliki kitu cha ml 10, ujue anauwezo kupata 10 nyingine, alafu gari kama gari, mtu ameweka mafuta ya hela ndogo ni Tsh. 10,000 sasa kwanini usimpe heshima huyu mtu, labda unamaanisha awe tajiri.
 
Wamekuja kasi sana hawa hata Mimi majuzi wamenikamata hapo Mbezi Louis... Karibu na roundabout ya kuja Malamba mawili...

Eti nitoe faini ya laki 2.... Uzuri niliwaeleza kuwa na mm ni kiongozi wa serikali na ukweli nilipaki pembeni ya vibanda kupokea simu muhimu iliyopigwa wakati nadrive... Wakaniachia...But walileta usumbufu kidogo...
 
Mimi ni kukamatwa tegeta kwa ndevu, wakaniomba rushwa tukakubaliana tuzunguke upande wa pili nikawatolee kwa wakala. Hilo lilikuwa kosa kwani gari nilishalitoa eneo la tukio na nilipoenda nachelewa maksudi waliogopa na kusepa
Uliwapatia kweli. Walikimbia maana walihisi unawaitia pccb
 
Anae takiwa kuwajibishwa ni mwenye mgahawa kwa kosa la kutoandika onyo au alama inayotahadharisha kuwa hilo eneo halina nafasi ya parking. Mimi ntaenda nikutane nao halafu niwafunze adabu. Najiandaa kwa shari kabisa. Pumbavu zao hao.
nenda tuu...
 
Ila huyo mwenye London Lounge sijui alifikiria nini kujenga baa nzuri kama ile halafu haina hata sehemu ya kuegeshea hata bajaj moja. Labda kama alikusudia iwe baa ya waende kwa miguu tu. Na siku hizi naona magari yamepungua sana pale labda huenda ni hii kadhia ya faini za "wrong parking" na magari mengi yanaonekana kwenye zile baa kule karibu na shule ya Makamba.
 
Faini iwe rafiki sh.5000 inatosha sambamba kupaki lory sehemu ya biashara kushusha na kupakia mzigo wanata laki 2 yaani wachawi wa biashara hawa.
 
Back
Top Bottom