Ukiegesha gari vibaya, faini kwa gari ndogo ni Tsh 200,000 na Tsh 10,000 ni gharama ya gari kulala yard kwa siku moja

Ukiwasha hazard hawatakiwi kukuletea zengwe!
Mie pamoja na kuwasha hazard nikashuka nikavuka barabara nikaenda ubalozi wa Japan kukabidhi documents getini, narudi nakuta wamezunguka gari.

Wanadai dereva akishuka akaacha gari hata kama kawasha hazard inahesabika amepaki.

Q*uma wale walikula 60,000 yangu maana ilibaki hatua chache waniingize kwenye yard yao kule Kurasini.
 
Mie pamoja na kuwasha hazard nikashuka nikavuka barabara nikaenda ubalozi wa Japan kukabidhi documents getini, narudi nakuta wamezunguka gari.

Wanadai dereva akishuka akaacha gari hata kama kawasha hazard inahesabika amepaki.

Q*uma wale walikula 60,000 yangu maana ilibaki hatua chache waniingize kwenye yard yao kule Kurasini.
Hahaha ukawapa 60 yao tu! Dah ni noma kweli sema usawa huu bora sitembei na gari maana watakuwa wapo kila mahali
 
Hao jamaa tangu enzi za Hayati walikuwepo wengi wanazunguka na Noah.
Mimi ni kukamatwa tegeta kwa ndevu, wakaniomba rushwa tukakubaliana tuzunguke upande wa pili nikawatolee kwa wakala. Hilo lilikuwa kosa kwani gari nilishalitoa eneo la tukio na nilipoenda nachelewa maksudi waliogopa na kusepa
 
Mie pamoja na kuwasha hazard nikashuka nikavuka barabara nikaenda ubalozi wa Japan kukabidhi documents getini, narudi nakuta wamezunguka gari.

Wanadai dereva akishuka akaacha gari hata kama kawasha hazard inahesabika amepaki.

Q*uma wale walikula 60,000 yangu maana ilibaki hatua chache waniingize kwenye yard yao kule Kurasini.
Ukiwasha hazard haitakiwi izidi dk 5 nadhani unatakiwa uwe umeshaondoa gari, so itakuwa walikuhesabia
 
Mimi ni kukamatwa tegeta kwa ndevu, wakaniomba rushwa tukakubaliana tuzunguke upande wa pili nikawatolee kwa wakala. Hilo lilikuwa kosa kwani gari nilishalitoa eneo la tukio na nilipoenda nachelewa maksudi waliogopa na kusepa
Walikuacha ukazunguka peke yako? Yaani hawakwenda na wewe?
 
Laki mbili mbona kubwa sana .... Me walishawai nikamata msasani .. nkaenda nao yard ya mwananyamala nkawapa 70000...Au labda imepanda sahv
 
Magomeni usalama
20210520_172941.jpeg
 
Pole sana brother kwa yaliyokukuta. Lakini pia nikutoe shaka kuwa wewe si mkosaji. Mkosaji ni yule anaevunja sheria akijua wazi kuwa ni kosa kufanya hivyo. Hapo kilichokukuta ni uonevu wa wazi.

Okay, hii nitakuelekeza ufanye next time yakikukuta madhira kama haya. Wewe ni raia huru na mlipa kodi katika taifa letu. Mamlaka zote zinatakiwa kukuheshimu na kukuhudumia kwa mujibu wa sheria zinazosimamia watendaji wao maeneo ya kazi.

Swali la kwanza ulitakiwa kuwauliza na ni lazima wakupe jibu ama sivyo wasiendelee kukusemesha, ulitakiwa uwaulize kwann wanagusa mali yako au gari lako bila ruhusa yako. Jibu lipo wazi, wangekwambia umepaki sehemu isiyoruhusiwa kupaki.

Then ungewauliza tena, swali, hapa nilipopaki mbona sikuona alama au maandishi ya onyo au katazo la kutoruhusu mtu kupaki?! Hili swali, jibu lake, litategemea na kama kweli kuna tangazo au alama ya katazo ambayo wewe haukuona au umeipuuza.

Then waambie wewe umepaki gari yako kwa maelekezo ya wahudumu wa mgahawa hivyo kuligusa gari lako bila ruhusa yako na kuzungumza na wewe ni kinyume na utaratibu.

Pia waambie kama kuna sheria imevunjwa wakwambie ni ipi na umeivunja kwa namna gani na kama wanataka kukuletea ubabe waambie wasubirie kuongea na mwanasheria wako ambaye unamwita muda huo huo anakuja kuongea nao ili yeye awape taratibu za kisheria.

Pia kama watang'ang'ania kuchukua gari waambie wakupe vitambulisho vyao vya kazi na National ID's upige picha uje uvitumie baadae kuwafungulia kesi ya upotevu wa mali zako kwenye gari na kukuharibia gari kwa namna walivyoiburuta.

Utawashitaki individually na sio kampuni iliyowatuma ili wawe na adabu na mali za watu siku nyingine. Wakigoma kukupatia ID zao usikubali waisogelee gari wala kuigusa kwa namna yoyote.

Hao mbwa waulize nilichowafanya pale mtaa wa fire road (ukiwa unaingia barabara ya United Nation, kabla haujaimaliza fensi ya shule ya jangwani ukiifuata shule ya azania, kuna barabara inaingia kulia inayoelekea upande ilipo hospital ya regency)

Walikuja na Kopo lao (Noah nyeupe)kunizingua kuwa nimepaki gari na sijawasha hazard na mtu nipo ndani ya gari. Nikawasha hazards lights, nikapandisha kioo nikaendelea kujilaza jamaa akagonga tena kumaanisha hatujamalizana. Nikashusha kioo, maana nilikipandisha kusudi ili wasiniongeleshe. Huku kuna takataka mwingine yupo upande wa mlango wa abiria wa mbele anavuta kitasa kutaka kufungua na nimelock milango.

Nikashusha kioo nakumtazama yale macho ya "unasemaje"! Ananambia, nakuomba ushuke, tuendelee na majukumu is yetu, umevunja sheria, nikamuuliza sheria gani, akasema wewe si umepaki na haujawasha hazards?! Nikamwambia ina maana hizo zinazowaka sio hazards?! Akasema si umewasha baada ya kutuona. Nikamwambia kijana katafute kazi ya kufanya usinipotezee muda, kichwa changu hakipo sawa. Nikapandisha kioo. Akagonga tena.

Nikamwambia sikiliza kama kuna kosa unalolijua wewe limevunjwa niambie ni kwa sheria ipi.... Jamaa akanambia hayo utayajua ukishalipa fine, utaratibu upo na utaelekezwa, fungua mlango tuelekee kituoni. Na kama hautaki gari tutaipeleka kwa kuikokota utaifuata kwa wakati wako. Tumeshaita gari ya kuvuta inakuja. Nikamwambia ngoja niongee na mtu. Nikampigia simu rafiki yangu ni wakili anapenda sana kubishana, akasema nipe nipe haraka hao ndio nawataka. Nikampa simu yule fala, akawa anagoma nikamwambia kama unajua kazi yako ongea na huyu muhusika.

Akagoma nikamwambia jamaa yangu, akasema weka loudspeaker. Akaaanza kuwaongelesha maneno kadhaa jamaa akachukua simu, akaanza ongea ikiwa loudspeaker. Jamaa yangu akawaambia naomba kama mnataka kugusa gari ya mteja wangu mjue mnatekeleza kosa la uvamizi na dhamira yenu inaweza kuwa ni kudhuru. Kama ninyi ni watu wa mamlaka husika nawaagiza mtoe vitambulisho vyenu vya taifa na vya kazi mteja wangu apige picha anitumie, kisha mnisubirie hapo, na mpige simu polisi kama kuna jinai imetendeka nje ya hapo kama ni kavunja sheria za jiji au halimashauri basi mnatakiwa kunisubiri nije hapo msifanye chochote na kama mnaharaka basi pelekeni kesi mahakamani tukutane huko ila nawashauri mjiandae pesa ya mashtaka kesi yenu ikikosa uhalali kisheria.

Jamaa wakaanza kujiuma uma pale wakasema wanamsubiria aje, nikawaambia haya naombeni ID zenu wote, wakagoma kutoa. Nikawaambia nadhani mlimsikia mwanasheria, mkigusa hii gari mnakesi ya uvamizi na kudhamiria kudhuru raia na mali yake.

Nikapandisha kioo nikalaza kiti nikatulia. Mwenyeji wangu akarudi muda huo huo. Nikawasha gari nikaanza kusepa jamaa wakaanza nizuia nisiondoke nikarudisha reverse nikachomoa gari taratibu, walipojaribu tena sikusima niliendelea kujanyaga mafuta. Wakajua huyo anaweza kutuua huyu nikasepa. Mwenyeji wangu kapigwa butwaa asijue nini kinaendelea.
 
kwa pale London mkamatwe tuu....mnapaki vibaya sana...na mwenye ile biashara hana akili.....alipaswa kuhakikisha wateja wana mahali salama kwa kupaki..........
Anae takiwa kuwajibishwa ni mwenye mgahawa kwa kosa la kutoandika onyo au alama inayotahadharisha kuwa hilo eneo halina nafasi ya parking. Mimi ntaenda nikutane nao halafu niwafunze adabu. Najiandaa kwa shari kabisa. Pumbavu zao hao.
 
Huo unaonekana kama uonevu, anayetakiwa kukamata makosa ya usalama barabarani ikiwemo na hiyo wrong parking ni askari wa usalama barabarani, na sidhani kama faini yake ni laki 2..
Mmmmmmhmn sio bongo hii.....
 
Hawa jamaa walishawahi niotea pale Sinza Mugabe, tena hii barabara mpya muwe makini sana kuna vibao kabisa vya parking kwa gari ndogo kubwa etc.. sasa mm nilisimama kweli kwenye kituo cha daladala nanunua kitu fasta dukani, ghafla wakavamia gari nilivyoenda tukaanza kubishana bishana pale mwisho tukaenda kwenye yard yao pale magomeni usalama hapo hata sijui kama fine yao ni laki mbili, mara baada ya kuanza kujaza kale kaform ndiyo nikaona hiyo figure nikasema hapa siwezi lipa hii hela yote. Ikabidi na mm sasa nitumie nguvu yangu zikapigwa simu pale nikaona ghafla wanaanza kuniita kiongozi , mwisho wa siku nikaishia kuwaachia elfu kumi tu hiyo ya parking sijui nayo waliomba nikaona siyo case. All in all wamerudi kwa kishindo sana hawa jamaa especially hii manispaa ya Ubungo, kama umepark sehemu siyo washa double hazard...ikiwezekana weka na triangle kabisa
Akiingia kwenye gari anza kumpiga kama mwizi.
 
Mimi ni kukamatwa tegeta kwa ndevu, wakaniomba rushwa tukakubaliana tuzunguke upande wa pili nikawatolee kwa wakala. Hilo lilikuwa kosa kwani gari nilishalitoa eneo la tukio na nilipoenda nachelewa maksudi waliogopa na kusepa
Hii pia ni smart move..... Unawaambia twende mkachukue hapa sina kitu. Kisha unawapeleka eneo lingine unawawashia moto.
 
Habari Wadau!

Wiki hii katika harakati zangu nimekumbana na kadhia ambayo ikanisikitisha sana. Ilikuwa majira ya mchana niliposimamisha harakati zangu na kuelekea sehemu ya kupata chakula cha mchana.

Nilipofika pale kama ilivyo siku nyingine zote ambazo huwa naenda kula mahali hapo, nikaegesha gari pembezoni mwa barabara kwani kijiwe hicho kama ilivyo vijiwe vingine vingi tu vya hapa DSM hakina maegesho maalumu ya magari ya wateja.

Baada ya kuegesha gari nikaingia ndani na kuagiza chakula na maji ya kukata kiu nikisubiri chakula. Ghafla nikashtuliwa na mtu akiniambia kuwa angalia gari yako inafungwa kule. Kuangalia kweli nawaona vijana na suti zao nyeusi wanaendelea kufunga nyororo na chuma kwenye gurudumu la mbele.

Nikahamaki nikaenda kwa haraka na kuwasha gari ili niliweke pembeni kuepuka usumbufu na hasara zisizo za lazima ambazo niliona zinafata wakati bado jamaa anaendelea na zoezi lake la kufunga. Lakini nikashtuka kuwa nitaharibu gari kwani alishazungusha chuma kwenye gurudumu.

Majibizano yalifata kila pande ikionesha iko sahihi bila mafanikio yoyote kwani niliona ni dhahili kuwa hawa jamaa wanachokifanya ni kuvidhia na kufunga magari ya watu ili wajipatie pesa tu. Baada ya kuona wameanza niletea habari za faini ya hili kosa ni Tsh 210,000.00 na ukiendelea kuleta ubishi tunaita break down tunavuta gari na gharama itakuwa yangu. Na mimi wakati huo hiyo pesa sina nikaona ni bora niendeshe hadi huko ofisini kwao (wenyewe wanaita yard) zilizopo Ubungo Mawasiliano Stendi labda kama ni faini nitapewa muda nitalipa au pengine nitakutana na mtu ambaye tunaweza ongea kwa kusikilizana na kuheshimiana bila kutishana tishana.

Kufika ofisini kwao wakajaza fomu zao pale wakanikabidhi kwa mwenzao. Nikaanza kwa kumuuliza kwanini mnakamata gari imeegeshwa pembezoni mwa barabara bila ata kuathili watumiaji wengine na ni sehemu ya biashara inayoonekana kabisa? Pia kwa muda mrefu tu nimekuwa nikipaki pale pale walipoikuta gari na kula chakula hadi namaliza naondoka bila shida yoyote?

Majibu yake ndio yalinifanya nimkumbuke Hayati Rais Magufuli.

Alisema enzi za Magufuli haya mambo ya mawakala wa halmashauri hayakuwepo. Aliyakataa. Ila kwa sasa yamerudi. So jitahidi kuwa makini unapoegesha gari lako kama yule mtoza ushuru wa maegesho ya magari hatakuwepo.

Akanieleza kuwa ni kweli faini kwa gari ndogo ni Tsh 200,000 na Tsh 10,000 ni gharama ya gari kupaki yard kwa siku moja.
Nikamuuliza tena hamuoni kuwa mnaua Biashara London Lounge?

Akajibu ni kweli mwenyewe inatakiwa aende kuomba kibali cha maegesho na ataletwa mtu wa Ushuru pale. Hili likifanyika, ata gari zipaki hadi zifunge njia hazitakamatwa.

Nikashangaa sana. Kwahiyo mimi nalipishwa Tsh 210,000 kwa sababu mtu wa kutoza Tsh 500 kwa saa hayupo ila nyie wa kutoza Tsh 210,000 mpo????

Nikamuuliza kwa hiyo hiyo faini nikiandikiwa nitailipa kwa muda gani?

Akajibu akasema siku yoyote ila gari utachukua utakapo kamilisha malipo ila hii Tsh 10,000 kwa siku itaendelea kukua.

Wacha niishie hapo na maelezo yangu.

Swali langu. Je, serikali ya sasa imeona hii ni njia sahihi kweli?? Baada ya malalamiko yote iliyojinasibu kuyafanyia kazi kuhusu watu kufunga biashara zao.

Sababu mimi binafsi sitakanyaga tena London Lounge kwa hichi kilichonipata leo na rafiki yangu yoyote atakayependekeza twende mahali hapo nitamueleza haya na tutaelekea sehemu nyingine. Serikali ya sasa katika hili nanyi pia mtaaua biashara za watu.
Unafanya mambo kwa kuzowea. Kama eneo halina maegesho rasmi, basi haliruhusiwi.
 
Back
Top Bottom