Habari Wadau!
Wiki hii katika harakati zangu nimekumbana na kadhia ambayo ikanisikitisha sana. Ilikuwa majira ya mchana niliposimamisha harakati zangu na kuelekea sehemu ya kupata chakula cha mchana.
Nilipofika pale kama ilivyo siku nyingine zote ambazo huwa naenda kula mahali hapo, nikaegesha gari pembezoni mwa barabara kwani kijiwe hicho kama ilivyo vijiwe vingine vingi tu vya hapa DSM hakina maegesho maalumu ya magari ya wateja.
Baada ya kuegesha gari nikaingia ndani na kuagiza chakula na maji ya kukata kiu nikisubiri chakula. Ghafla nikashtuliwa na mtu akiniambia kuwa angalia gari yako inafungwa kule. Kuangalia kweli nawaona vijana na suti zao nyeusi wanaendelea kufunga nyororo na chuma kwenye gurudumu la mbele.
Nikahamaki nikaenda kwa haraka na kuwasha gari ili niliweke pembeni kuepuka usumbufu na hasara zisizo za lazima ambazo niliona zinafata wakati bado jamaa anaendelea na zoezi lake la kufunga. Lakini nikashtuka kuwa nitaharibu gari kwani alishazungusha chuma kwenye gurudumu.
Majibizano yalifata kila pande ikionesha iko sahihi bila mafanikio yoyote kwani niliona ni dhahili kuwa hawa jamaa wanachokifanya ni kuvidhia na kufunga magari ya watu ili wajipatie pesa tu. Baada ya kuona wameanza niletea habari za faini ya hili kosa ni Tsh 210,000.00 na ukiendelea kuleta ubishi tunaita break down tunavuta gari na gharama itakuwa yangu. Na mimi wakati huo hiyo pesa sina nikaona ni bora niendeshe hadi huko ofisini kwao (wenyewe wanaita yard) zilizopo Ubungo Mawasiliano Stendi labda kama ni faini nitapewa muda nitalipa au pengine nitakutana na mtu ambaye tunaweza ongea kwa kusikilizana na kuheshimiana bila kutishana tishana.
Kufika ofisini kwao wakajaza fomu zao pale wakanikabidhi kwa mwenzao. Nikaanza kwa kumuuliza kwanini mnakamata gari imeegeshwa pembezoni mwa barabara bila ata kuathili watumiaji wengine na ni sehemu ya biashara inayoonekana kabisa? Pia kwa muda mrefu tu nimekuwa nikipaki pale pale walipoikuta gari na kula chakula hadi namaliza naondoka bila shida yoyote?
Majibu yake ndio yalinifanya nimkumbuke Hayati Rais Magufuli.
Alisema enzi za Magufuli haya mambo ya mawakala wa halmashauri hayakuwepo. Aliyakataa. Ila kwa sasa yamerudi. So jitahidi kuwa makini unapoegesha gari lako kama yule mtoza ushuru wa maegesho ya magari hatakuwepo.
Akanieleza kuwa ni kweli faini kwa gari ndogo ni Tsh 200,000 na Tsh 10,000 ni gharama ya gari kupaki yard kwa siku moja.
Nikamuuliza tena hamuoni kuwa mnaua Biashara London Lounge?
Akajibu ni kweli mwenyewe inatakiwa aende kuomba kibali cha maegesho na ataletwa mtu wa Ushuru pale. Hili likifanyika, ata gari zipaki hadi zifunge njia hazitakamatwa.
Nikashangaa sana. Kwahiyo mimi nalipishwa Tsh 210,000 kwa sababu mtu wa kutoza Tsh 500 kwa saa hayupo ila nyie wa kutoza Tsh 210,000 mpo????
Nikamuuliza kwa hiyo hiyo faini nikiandikiwa nitailipa kwa muda gani?
Akajibu akasema siku yoyote ila gari utachukua utakapo kamilisha malipo ila hii Tsh 10,000 kwa siku itaendelea kukua.
Wacha niishie hapo na maelezo yangu.
Swali langu. Je, serikali ya sasa imeona hii ni njia sahihi kweli?? Baada ya malalamiko yote iliyojinasibu kuyafanyia kazi kuhusu watu kufunga biashara zao.
Sababu mimi binafsi sitakanyaga tena London Lounge kwa hichi kilichonipata leo na rafiki yangu yoyote atakayependekeza twende mahali hapo nitamueleza haya na tutaelekea sehemu nyingine. Serikali ya sasa katika hili nanyi pia mtaaua biashara za watu.