Ukichaa ni nafsi au akili?

Ukichaa ni nafsi au akili?

Kila siku tunaona watu wanakufa mkuu.
Sio lazima unachokiota uwe umekiexperience wewe hata kama uliona tu au una hio idea...huwezi kuota (never) kitu ambacho huna idea kabisa..

Mfano hata ukiota umekufa umeenda mbinguni basi mbingu itakuwa na watu unaowafahamu au mazingira yske yatakuwa ya kibinadamu mf kutakuwa na nyumba labda treni n.k

Lakini huwezi kupaota mbinguni halafu ukaanza kuona vitu ambavyo hujawahi kuviskia wala kuimagine ukiwa macho..hio ni impossible.

Sometimes ndotonk unaweza kuona sura mpya kabisa ya mtu..lkn jiulize ni watu wangapi ulishaona sura zao tangu unazaliwa?? Kwahio hio sura mpya ni moja ya sura ulizoziona lkn ukasahau but the brain has a place for such memories

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo langu mie lilikuwa kwenye kuexperience tu,kwa nilivyokuelewa ni kwamba ndoto zengine si katika vitu tulivyo experience bali ni fikra tu zetu hivyo ndoto za kufa na za huko mbinguni kila mtu ataota kadri vile alivyoimagine.
 
Au mkuu ulshawahi kuwaza kipofu tangu kuzaliwa huwa anaota nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au mkuu ulshawahi kuwaza kipofu tangu kuzaliwa huwa anaota nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi kuchunguza hilo na si ndoto tu kuna vitu vingi nahitaji kuvijua kuhusu hao vipofu wa kuzaliwa,ila kama wewe umeshawahi kufuatilia kuhusu ndoto za vipofu basi unaweza ukaeleza ndoto zao huwa kama sisi au vp?
 
Kipofu aliepufuka ukubwani anapata ndoto kama sisi sababu ya vitu alivyoexperience kabla hajawa kipofu..

Lakini hawa wa kuzaliwa anaota jinsi anavyofikilia jinsi vitu vilivyo (anavyo perceive) mfano kwenye ndoto yake akiota kugongwa na gari basi ataliona gari kama anavyofikiria yeye haliwezi kuwa gari la kawaida na most of the time wanaota audio tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sayansi imeprove uwepo wa akili kwa binadamu kwanini isiprove uwepo wa nafsi na roho, ikiwa vyote ni intangible
Huwezi kuprove kitu kisichokuwepo..
Labda unaposema nafsi unamaanisha hii akili inayotunza kumbukumbu ,inayotambua mema na mabaya ambayo ni part ya brain.

Zamani watu walikua wanaamini MOYO unaplay part kwenye tabia ya mtu mf huruma ,kupenda nk
Lakini ikaja kufahamika moyo kazi yake ni kupump damu tu...ndio maana watu wakifanya heart transplant mtu anabaki na personality yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika pitapita zangu nmekuja jua kuwa katika mtu kuna mambo makuu matatu, yaani nafsi, akili na mwili.
Nafsi ndio mtu mwenye kwa maana yu hai hata ukitoka mwili(kufa).
Leo nataka mwenye kujua anijuze; Ni ipi nafasi ya nafsi kwa kichaa katika maisha yake, baada ya akili kwenda mrama. Ni kweli kichaa ni akili au nafsi?.
Pia naomba kujua kichaa usingizini huota akiwa safi au huwa katika ukichaa uleule? Vipi akifa atabakia kuwa kichaa katika ulimwengu wa giza?.
Wajuvi wa mambo haya karibuni.

Ni nafsi, mwili Na roho sio akili
 
Kipofu aliepufuka ukubwani anapata ndoto kama sisi sababu ya vitu alivyoexperience kabla hajawa kipofu..

Lakini hawa wa kuzaliwa anaota jinsi anavyofikilia jinsi vitu vilivyo (anavyo perceive) mfano kwenye ndoto yake akiota kugongwa na gari basi ataliona gari kama anavyofikiria yeye haliwezi kuwa gari la kawaida na most of the time wanaota audio tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mfano mtu akikwambia ameota mnyama kama simba lakini hakuwa simba,je utaweka nafasi gani hicho alichokiota? Maana ni wazi hajawahi kumuona mnyama huyo wala hajawahi kuimagine uwepo wa mnyama huyo.
 
Au mkuu ulshawahi kuwaza kipofu tangu kuzaliwa huwa anaota nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ndipo uliponifanya niwaze kidogo...your thought has a content inside....ni ipi dhana ya kuwa kila unachoota ni lazima macho yawe yame experience katika hali ya mazingira ya kawaida ukiwa concious....??

...But how if somebody is born without eyes ( Anophthalmia) yani mtu anazaliwa hana jicho au hana macho kabisa japo ni rarely sana ila hali hizo zinatokea kwa baadhi ya maeneo duniani japo juhudi za kuwawekea reconstruction nyingine kwa njia ya ocular prostheses inafanya kazi lakini sasa tujiulize hao vipofu ambao pengine wanakuwa na umri mkubwa kabla ya kuja kupewa tiba ya kurudisha sight yao ,Je !wakilala usiku,.....what is their mental occular reflection inayokuja kwa njia ya ndoto....??

My take....

Ndiyo kuna ushahidi wa kisayansi kuwa kila unachokiota ni lazima macho yako yawe yamesha ki witness( Shuhudia) katika physical reality....Lakini je ni kweli ndoto ni reflection ya yote ambayk macho yameona katika concious reality....??

Kuna mazingira mtu anaota ili hali hajawahi kufika huko wala hajawahi kuwa na idea ya mazingira flani ila anota mazingira tofauti kabisa.. ....

Mara ngapi mtu anaota kakatika mguu lakini hajawahi kuwa na imagination ya namna hiyo...!!??

Dream covers a wide range of reflection ,kuna physical reflection na mental reflection ,inategemeana zaidi ni wapi akili yako inasimamia zaidi...ukiwa unaconcentrate zaidi kuona vitu na kuviweka akilini nayo akili yako itafanya back up reflection katika memory centre ,mtu anaota kile ambacho macho yamekuwa yakikiona mara kwa mara lakini memory yako inakuwa inakipa nafasi sana thus why intensity zake zinakuwa nyingi( overcapacity) na kufanya memory centre kuwa inatema data kwenye subconcious kuikumbusha kuwa hiki kitu nishakihifadhi but kinadisturb snaa...

Lakini pia mtu anaweza pata mental reflection kama kuna kitu anakifikilia kwa muda mrefu ( Mental ideation for a long time) bila kukiiona kwa macho hence memory inahifadhi kwa staili ile ile ,nayo ikiwa kubwa inampa taarifa bwana subconcious kuwa hicho kitu kimechukua nafasi sana kwenye sehemu yangu vipi hakuna namna ya kukiondoa ....!!

So dreaming is what your mind concentrates together with your eyes witnessing the moments ever....

Back to question.........

Kichaa ni mtu kama wewe ambaye una percieve mambo kulingana na concious awareness yako..

Kila mtu ana eneo au capacity flani katika ku percieve mambo...kila mtu ana range yake ya kuona na kuhisi mambo katika interaction range flani....

Mtu ambaye kawa kichaaa hawezi jijua kama amekuwa kichaaa kwani ukichaa ni hali ambayo mental inahamia katika level zingine za awareness na anapokuwa kwenye mazingira hayo anakuwa normal ( kwake) ila nyie ambao majority mpo kwenye level moja ya awareness mnamuona kama nati zimelegea na yeye anakuwa anawaona kama nati zenu zimewalegea.....

Mpaka pale atakapopewa dawa ya kuirudisha conciousness yake katika range ya kawaida ndo anaweza feel kama yupo sawa na nyie...

Mwili wa binadamu ni kama computer....

Computer ilitengenezwa kuportray jinsi mwanadamu anavyofanya kazi....unavyoiona computer ilivyo ndivyo hata wewe ulivyo...jinsi inavyofanya kazi ndivyo wewe pia ulivyo...jinsi ilivyoundwa ndani ndivyo hata wewe ulivyo...jinsi inavyotumia umeme ili ifanye kazi ndivyo hata wewe unahitaji chakula ili uwe concious muda wote...jinsi ilivyo na keyboard ili iweze kutoa comand ndivyo ulivyo hata wewe , una vidole na miguu ili utembee na kufika mahala husika....

kama ambavyo inaweza ikacease ( Off) au on na kutoa informations kuhusu ilichokihifadhi ndivyo hata wewe unaweza ukafa na kupoteza kila kitu kichwani mwako...

computer ni kama mwanadamu...ina HD( hard disc in GB ili kuhifadhi materiols au documents,)ndivyo ulivyo ubongo wa mwanadamu ,bila hard disc computer haiwezi hifadhi chochote,bila ubongo ,mwanadamu hawezi hifadhi chochote..

Computer ina Processor na RAM ambavyo vina ifanya computer iwe inasoma kwa haraka nyaraka zilizohifadhiwa kwenye hard dis ,so peocessor kubwa na RAM kubwa hufanya computer kuwa nyepesi katika duveliver unachokihitaji kwa haraka zaidi..

Ukiwa na processor ndogo au RAM ndogo ndivyo uwezo wa kufungua document na mafaili kwenye hard disc unakuwa shida...

Ndivyo ilivyo kwenye ubongo...mtu anahitaji akili zaidi ambayo itakuwa inasoma na kupembua mambo ambayo ubongo umeyahifadhi..ukiwa ana akili zaidi ndivyo uwezo wa kuhifadhi na kukumbuka mambo unakuwa mwepesi and vice versa...

Computer ina transistors na capacitors nying sana ,ndivyo ulivyo mwili wa mwanadamu umeundwa kwa cell na organi nyingi ambazo zinafanya kazi kwa pamoja..kimoja kikifeli kingine kinaathirika kwa namna moja au nyingi (indirectly)...

Hivyo basi,the way unavyoiona computer ndivyo miili yetu inafanya kazi...

So ukichomoa kifaa mimoja kidogo kwenye computer ,japo computer inaweza izioneshe dalili za kushindwa kufanya kazi ila ipo siku itazima gafla na utashindwa kujua shida ni nini kumbe kuna kitu kilitolewa sehemu ...na ndo mwisho wa computer yako kufanya kazi ndivyo yalivyo maisha wa mwanadamu...

Hata miili yetu nayo ni hivyo hivyo..ikifeli figo,basi ipo siku Ini nalo litafeli...ukifeli ubongo ipo siku Ini litafeli nalo..everything interact in such away that ni multisystem dependant...miili yetu ni multisystem dependant.....mfumo mmoja unategemea mfumo mwingine ili mwili wote uwe hai..so ni lazima mifumo yote iwe hai ndipo mwili utakuwa okeyyyyyyy...

Kwa hiyo swala la kuwa kichaaa anaota nini au anajiona ni wa hali gani ni kwamba kila hali huwa inaji define ikiwa kwenye hali flani ya concious awareness....

Wenye uelewa mdogo wa akili huwa wanajiona wapo sawa kuliko wengine ,hali kadhalika kwa wenye akili nyingi nao huwa wanajiona ni bora kuliko wengine...kwa hiyo kila level ilipo conciousness yako inaipa akili yako ufahamu kuwa upo kawaida tu na huwezi kujijua mpaka utoke level ulipo...

So the shifted mental status ya mwanadamu yoyote haiwezi jigundua mpaka pale itakaporudishwa kwenye deviated condition.....

Sent using Nokia 8 Plus
 
*Kifuatacho*

Kwa yule ambae hafahamu jina sahihi la mlemavu sasa naomba afahamu hivi

Kipofu............ *asiyeona*

Zeruzeru, mlemavu wa ngozi........ *albino*

Asiyesikia........... *kiziwi*

Kichaa............. *mwenye ugonjwa wa akili*

Zezeta,taahira............................... *mwenye ulemavu wa akili*

Kifafa................ *mwenye kifafa*

Mbilikimo......... *mwenye umbile fupi*

Kilema............ *mlemavu*
Kiwete.......... *mlemavu wa viungo*

Tukumbushane kutumia majina sahihi
Mkuu akili inatafsiri kila k2, lakin hicho k2 kinatoka wapi,. Ama taarifa inapindishwa na akili au akili inapokea taarifa ilipinda kabisa
 
Nafsi:

Mwanzo 2:7 inaonesha jinsi ambavyo Nafsi ya mtu iliumbwa. Nafsi husimamia mambo 3. (1) Hisia (kuchukia, kufurahi, kusikitika, kupenda n.k.); (2) Nia (namna tunavyofikiri); (3) Utashi (namna tunavyoamua). ......................

Hata hivyo, nafsi ndiyo mfasiri (interpreter) wa yaliyopo rohoni kwenda kwenye mwili au ya mwilini kwenda rohoni. Nafsi inaweza kufa.
Haya ni madini safi sana... kwamba akili ndiyo nafsi... Barikiwa.
 
Ni kweli mtu yupo katika hali tatu, lakini natofautiana na wewe katika kuzitambua hizi hali. Binadamu ni Roho, Nafsi na Mwili.

Roho:

Mwanzo 1:26-27 (na tufanye mtu kwa mfano wetu...), andiko hili linaonesha jinsi ambavyo Roho iliumbwa, ndiyo maana imeandikwa kuwa wote, mwanamume na mwanamke waliumba siku moja, hii kwa sababu uumbaji wa roho ulifanywa siku moja. Wengi wamekuwa wakipotosha kuhusu andiko hili wakidai kuwa huyu mwanamke aliyeumbwa hapa si Hawa ila kulikuwa na mwanamke mwingine jambo ambalo si kweli. Kwa mwanadamu, Roho (au ulimwengu wa roho) ni sawa na soft copy (Roho), ambayo huandaliwa kabla ya priting (kuumbwa kwa mwili), ambapo ndipo utapata hard copy (Mwili).

Roho husimamia mambo yote ya ndani ya mtu kama ya ibada iwe za Kimungu au kishetani, mapokeo ya karama na vipaji mbalimbali, kuandaa mawazo, ndoto, udadisi, ufahamu, tafsiri mbalimbali n.k. Roho haiwezi kufa, kwani ndiyo nguvu na mfano wa Mungu (Uungu) na hurudi kwa Mungu baada ya mwili huu kufa.

Nafsi:

Mwanzo 2:7 inaonesha jinsi ambavyo Nafsi ya mtu iliumbwa. Nafsi husimamia mambo 3. (1) Hisia (kuchukia, kufurahi, kusikitika, kupenda n.k.); (2) Nia (namna tunavyofikiri); (3) Utashi (namna tunavyoamua).

Mwanadamu mmoja anahusiana na mwingine kwa nafsi yake, unapokuwa kwenye uhusiano na mtu hisia zako, nia yako na utashi wako huunganishwa na mtu huyo. Ndiyo maana ukishaingia kwenye uhusiano basi hata kufikiri au kuamua kwako hubadilika... Ndiyo maana ukiingia kwenhe uhusiano usio sahihi basi hata kufikiri kwako, kuhisi na kuamua kwako kunavurugwa, wakati mwingine utatamani usifikiri au usiamue namna unavyoenenda lakini unakuwa hujui utajinasuaje.

Hata hivyo, nafsi ndiyo mfasiri (interpreter) wa yaliyopo rohoni kwenda kwenye mwili au ya mwilini kwenda rohoni. Nafsi inaweza kufa.

Hoja zako ziko na mashiko sana Bishop, M niko naswali hapa je kuna uhusiano wowote ule kati ya nafsi pamoja moyo?
 
M

Mwili:

Mwanzo 2:7 (Mungu akamuumba mtu kwa mavumbi). Mwili huhusisha mambo yote ya nje (ya ulimwengu). Mwili pia husimamia mambo 3: (1) Utambuzi (hali ya kibinadamu ya kupokea habari kwa njia ya ufahamu); (2) Urejeshi "reaction" (hali ya kutenda kutokana na kutendewa, iwe kwa maneno au matendo; (3) Udhihirisho (hali ya mwili kutoa habari za ulimwengu kwa mawazo, kujisikia au maamuzi ya nafsi. Mwili unakufa na kurudi mavumbini ulikotoka.

Sasa swali la kujiuliza, mtu anapopata matatizo ya kiakili (ukichaa, msongo wa mawazo n.k.) ni nini kinachokuwa kimepata shida? Kwa maelezo yangu nadhani jibu lipo wazi kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu lako linaweza kuponya hadi machizi
 
Haya ni madini safi sana... kwamba akili ndiyo nafsi... Barikiwa.
Mwal
Fuatilieni semina ya Mwl Mwakasege kuhusu somo la kutumia akili. Yuko Moshi kuanzia 25/2/2019 hadi 3/3/20019. Fuatilia YouTube, Radio Sauti injili kuanzia 11.00 jioni na kurudiwa usiku SAA 5.00. Pia www.mwakasege.org utajifunza mengi kuhusu kutumia akili ktk mpango wa Mungu ili ufanikiwe ktk maisha yako
 
Hoja zako ziko na mashiko sana Bishop, M niko naswali hapa je kuna uhusiano wowote ule kati ya nafsi pamoja moyo?
Ndiyo mkuu, uhusiano upo mkubwa sana... Nafsi inahusika kwa asilimia 100 na ufahamu wa mtu mwenyewe na pia ni kiini cha ubinafsi, ikiwa na kazi tatu za kuhisi, kufikiri na kuamua, hali kadhalika hizo ndizo kazi za moyo...
 
Mtu anapokua kichaa manake kwenye nafsi kumepata shida ila haimaanishi kwamba hana akili,kila mtu ana akili ila inategemea nafsi imeshibishwa nini ndani yake ndiyo hupelekea mtu kutafsiriwa vile anavoonekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo mkuu, uhusiano upo mkubwa sana... Nafsi inahusika kwa asilimia 100 na ufahamu wa mtu mwenyewe na pia ni kiini cha ubinafsi, ikiwa na kazi tatu za kuhisi, kufikiri na kuamua, hali kadhalika hizo ndizo kazi za moyo...

Ahsante sana Bishop Hiluka
 
Back
Top Bottom