Ni kweli mtu yupo katika hali tatu, lakini natofautiana na wewe katika kuzitambua hizi hali. Binadamu ni Roho, Nafsi na Mwili.
Roho:
Mwanzo 1:26-27 (na tufanye mtu kwa mfano wetu...), andiko hili linaonesha jinsi ambavyo Roho iliumbwa, ndiyo maana imeandikwa kuwa wote, mwanamume na mwanamke waliumba siku moja, hii kwa sababu uumbaji wa roho ulifanywa siku moja. Wengi wamekuwa wakipotosha kuhusu andiko hili wakidai kuwa huyu mwanamke aliyeumbwa hapa si Hawa ila kulikuwa na mwanamke mwingine jambo ambalo si kweli. Kwa mwanadamu, Roho (au ulimwengu wa roho) ni sawa na soft copy (Roho), ambayo huandaliwa kabla ya priting (kuumbwa kwa mwili), ambapo ndipo utapata hard copy (Mwili).
Roho husimamia mambo yote ya ndani ya mtu kama ya ibada iwe za Kimungu au kishetani, mapokeo ya karama na vipaji mbalimbali, kuandaa mawazo, ndoto, udadisi, ufahamu, tafsiri mbalimbali n.k. Roho haiwezi kufa, kwani ndiyo nguvu na mfano wa Mungu (Uungu) na hurudi kwa Mungu baada ya mwili huu kufa.
Nafsi:
Mwanzo 2:7 inaonesha jinsi ambavyo Nafsi ya mtu iliumbwa. Nafsi husimamia mambo 3. (1) Hisia (kuchukia, kufurahi, kusikitika, kupenda n.k.); (2) Nia (namna tunavyofikiri); (3) Utashi (namna tunavyoamua).
Mwanadamu mmoja anahusiana na mwingine kwa nafsi yake, unapokuwa kwenye uhusiano na mtu hisia zako, nia yako na utashi wako huunganishwa na mtu huyo. Ndiyo maana ukishaingia kwenye uhusiano basi hata kufikiri au kuamua kwako hubadilika... Ndiyo maana ukiingia kwenhe uhusiano usio sahihi basi hata kufikiri kwako, kuhisi na kuamua kwako kunavurugwa, wakati mwingine utatamani usifikiri au usiamue namna unavyoenenda lakini unakuwa hujui utajinasuaje.
Hata hivyo, nafsi ndiyo mfasiri (interpreter) wa yaliyopo rohoni kwenda kwenye mwili au ya mwilini kwenda rohoni. Nafsi inaweza kufa.
Mwili:
Mwanzo 2:7 (Mungu akamuumba mtu kwa mavumbi). Mwili huhusisha mambo yote ya nje (ya ulimwengu). Mwili pia husimamia mambo 3: (1) Utambuzi (hali ya kibinadamu ya kupokea habari kwa njia ya ufahamu); (2) Urejeshi "reaction" (hali ya kutenda kutokana na kutendewa, iwe kwa maneno au matendo; (3) Udhihirisho (hali ya mwili kutoa habari za ulimwengu kwa mawazo, kujisikia au maamuzi ya nafsi. Mwili unakufa na kurudi mavumbini ulikotoka.
Sasa swali la kujiuliza, mtu anapopata matatizo ya kiakili (ukichaa, msongo wa mawazo n.k.) ni nini kinachokuwa kimepata shida? Kwa maelezo yangu nadhani jibu lipo wazi kabisa...
Sent using
Jamii Forums mobile app