Ukiangalia vizuri mpotoshaji mkubwa ni serikali, kwanini inachukuliwa hatua pale tu mwananchi akipotosha?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema?

Tumeshudia mara kadhaa wananchi wakichukuliwa hatua kwa makosa ya "Kusambaza taarifa za uongo" au kufanya "Upotoshaji", mfano wa juzi juzi hapa ni yule dada aliyeimba mnatuona manyani "Tanzania inaelekea wapi?" baada ya kuona shtaka la kusababisa uchochezi ni weak shataka likageuka na kuwa kusambaza taarifa za uongo.

Ila huwezi kukuta serikali ikichukua hatua ikiwa kiongozi kafanya hivyo, kwanini? Wao wanakinga na sheria hiyo?

Mfano mzuri na wengi tunaukumbuka ni kipindi Waziri Mkuu Majaliwa alipotupatia taarifa za tena sio mara moja pale alipotuambia Rais Magufuli ni mzima wa afya anaendelea na kazi.

Yaani alipotosha taifa zima, akiwa anajua fika ni uongo, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake mpaka sasa.

Sasa jichanganye wewe mwananchi wa madongo kuinama, mashariki haisomeki magharibi haieleweki, kula yako mtihani kulala songombingo kusema taarifa ya uongo, kabla hujakohoa umeshafikishwa mahamani!

Kwa msumeno huu umeweka kukata upande wa wananchi pekee, serikali mko na kinga ya kusema uongo mtakavyo ila ikifika kwetu ni kosa?

Sheria hizi zimekuwa zikitumika kubana uhuru wa watu kujieleza (Freedom of Expression) maana watu wanachukuliwa tu hatua wakikosoa serikali, mnataka wote tuwe kasuku kusema ndio tu kwa kila mnachosema.

Habari zikufikie Waziri Nape na TCRA.
 
Back
Top Bottom