Uchambuzi: Kanuni Mpya za Maudhui ya Mtandaoni 2020, Marufuku ya Maudhui yaongezeka

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1596460516854.png
Julai 17, 2020, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilichapisha mabadiliko ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni kwenye gazeti la Serikali kupitia gazeti Na.29 Toleo la 101. Mabadiliko hayo ambayo yalitolewa kupitia notisi Na. 538 yanabadilisha baadhi ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2018 na kuongeza baadhi ya mambo katika kanuni hizo.

Kwa mujibu wa sheria, mabadiliko hayo kitaalamu yanaitwa mabadiliko ya nyongeza (subsidiary legislation) ambayo sheria inaruhusu kufanyika kupitia viongozi na mamlaka zilizopo kwa mujibu wa sheria husika. Katika muktadha wa Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni Tanzania, Waziri wa wizara husika, kwamfano wa sasa ni wa Habari, Sanaa na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe ndiye msimamizi wa masuala ya habari ingawa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ina jukumu la usimamizi wa maudhui mtandaoni haipo chini ya Wizara ya Habari. Mabadiliko hayo ya mwaka 2020 yamesainiwa na Dkt. Harrison Mwakyembe, Julai 1, 2020. Mabadiliko hayo yameongeza aina za maudhui yasiyoruhusiwa kuchapishwa mtandaoni na kufanya kuwepo kwa aina 10 za maudhui ambayo ni marufuku kuwekwa katika mitandao. Makubwa yaliyopo kwenye Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2020 ni pamoja na kuongezeka kwa aina za maudhui ambayo yamezuiliwa kwa mujibu wa kanuni hizo.

Kanuni zinazuia uchapishaji wa maudhui yanayohamasisha vitendo vya ngono. Kanuni zinazuia watumiaji wa mitandao kuweka maudhui yanayohamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ugoni, ukahaba na makosa ya kingono kama ubakaji.

Maudhui yanayohamasisha uvunjwaji wa sheria za nchi na kutishia ulinzi na usalama wa nchi yamezuiliwa. Kanuni zinazuia maudhui yanayowahamasisha watu kupingana na serikali na maelekezo yaliyotolewa na serikali hasa kwa kuchapisha taarifa za uongo au tetesi zenye lengo la kuchafua taswira ya nchi. Mtumiaji wa mtandao pia hatapaswa kuweka taarifa zinazoweza kuleta mtafaruku kuhusu afya ya umma ikiwemo taarifa kuhusu mlipuko wa majanga na magonjwa kama corona.

Pia, kwa mujibu wa Kanuni hizi ni marufuku kuweka mtandaoni maudhui yenye lengo kuhamasisha biashara ya kamari, michezo ya kubahatisha, dawa za binadamu na bidahaa za kifamasia bila kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka husika.

Kanuni zinapiga marufuku maudhui yanayohamasisha uchapishaji wa taarifa zinazohamasisha uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya, na bidhaa zingine ambazo zimepigwa marufuku Tanzania. Kanuni zinazuia watumiaji wa mitandao kunakili kazi zenye hati miliki bila kupata kibali cha mmiliki. Kanuni zinazuia watumiaji wa mitandao kukashifu dini na kutumia dini vibaya kusababisha ubaguzi au kuchochea mambo yaliyo kinyume na sheria. Pia, kanuni zinazuia mtuamiaji wa mtandao kuweka maudhui yayochochea vitendo vya kichawi na ushirikina mtandaoni.

Kanuni zinazuia maudhui yanayotumia utambulisho wa mtu mwingine kwa malengo ya kufanya udanganyifu. Kanuni zinazuia maudhui yanayotweza utu wa mtu mwingine kwa kutumia matusi, au kutoa habari, picha au maoni yanayofichua usiri wa mtu au kuchapisha taarifa za siri na zinazoweza kumuathiri muhusika hata kama taarifa hizo ni za kweli. Kanuni zinazohamasisha udukuzi wa taarifa, wizi wa taarifa za mtu, ujasusi, kufuatilia, kurekodi au kuingilia mawasiliano au mazungumzo ya mtu zimepigwa marufuku.

Kanuni pia zinawazuia watumiaji wa mitandao kutokutumia lugha za kuudhi/matusi na kutokusambaza taarifa za uongo au za upotoshaji.

Kwa ujumla, Kanuni mpya zimeongeza mawanda kwa kuhakikisha maudhui ya wasanii, wanahabari, taasisi za dini, mashirika na watu binafsi katika mitandao ya kijamii yanachujwa chini ya hekaya ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pamoja na kuongeza aina za maudhui ambayo yamezuiliwa mtandaoni, Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2020 zimeongeza baadhi ya vigezo vya mtoa maudhui kujisajili pamoja na kuongeza aina/ vipengele vya huduma za maudhui mtandaoni na kuainishwa kwa ada zake.

Kwa upande wa vigezo, mtoa huduma za maudhui mtandaoni anapaswa kuonesha wazi kama huduma yake ni kwa ajili ya kutengeneza faida au si kwa ajili ya kutengeneza faida. Kwa upande wa vipengele vya huduma za maudhui na ada, kanuni mpya zimeleta ada kwa wazalishaji wa maudhui ya burudani. Wasanii wanaotumia mitandao kama YouTube na majukwaa mengine watapaswa kulipia ada ya shilingi za Kitanzania 100,000 ya maombi ya leseni huku wakilipa shilingi 500,000 kama ada ya leseni kwa kila mwaka.

Kwa watoa maudhui ya elimu na dini na wao pia watapaswa kulipa kiwango sawa na watoa maudhui ya sanaa na burudani kama ilivyooneshwa katika jedwali la ada za usajili na leseni lililowekwa wazi katika mabadiliko ya kikanuni. Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2020 zimeendelea kubaki na vifungu ambavyo vinaiwezesha mamlaka husika kufuta leseni ya chombo chochote kilichosajiliwa chini ya Kanuni. Pia, makosa na adhabu zimebaki kama zilivyokuwa, adhabu ya faini ya 5,000,000 au kifungo cha muda usiopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja kwa anayevunja kanuni.

Ujio wa Kanuni hizi umezua mjadala miongoni mwa wadau hasa watumiaji wa mitandao ambao wengi wanaguswa na Kanuni za Muadhui Mtandaoni. Wadau wana maoni tofauti, wengine wakiendeleza mjadala ambao uliibuka wakati wa kuandaliwa kwa Kanuni za Maudhi ya Mtandaoni 2018 kuhusu watoa huduma za maudhui kulipa ada.

1596460621196.png

1596460649603.png

Mtazamo wa wadau wanaopinga uwepo wa ada na malipo ya leseni ni kwamba ada hizo zinazuia ubunifu na uwepo wa maudhui ya kutosha ya kitanzania katika mitandao kwani Watanzania wengi wanashindwa kulipia leseni ili kuendesha majukwaa kama blogu, YouTube na podcast ambayo ni majukwaa ya bure kabisa. Vilevile, baadhi ya wadau wanachagiza hoja hiyo kwa kusema kuwa Mamlaka za Tanzania hazipaswi kuweka tozo kubwa ya usajili kwakuwa hazitoi huduma ya miundombinu kama vile kikoa na hifadhi kwaajili ya majukwaa, tovuti na idhaa kama za YouTube inayowezesha matumizi ya majukwaa hayo ya mtandaoni miongoni mwa watumiaji.

1596460700033.png
Kwa upande mwingine, watetezi wa haki ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa maoni wameendelea kusisitiza kwamba makatazo mengi yaliyoletwa na mabadiliko hayo yanaweza kuathiri uhuru wa wananchi kujieleza hasa kwa kuzingatia kwamba nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo inasimamia kanuni hizo, imeeleza kuwa lengo la Kanuni hizo ni kuongeza utii wa sheria na kuhakikisha watuimiaji wa mitandao wanaelewa mambo yanayokatazwa mtandaoni.

Andrew Kisaka, Mkuu wa Kitengo kinachohusika na utoaji leseni wa TCRA amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba Kanuni hizo zinaongeza vipengele vya huduma ikiwemo watoa huduma za elimu na dini ambao amesema watachajiwa asilima 50 ya malipo ya leseni kutokana na umuhimu na uhitaji wa huduma wanazotoa.

‘’Pia kanuni hizi mpya zimebainisha na kuelezea masuala yanayokatazwa ili kuongeza uelewa wa raia na kuongeza utii wa sheria’’ Kisaka anasema. Tangu kutungwa kwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni mwaka 2018 baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo vyombo vya habari vya kidigitali vimechukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kupigwa faini, kufungiwa na vingine kupata adhamu zote kutoka na kukiuka kanuni mbalimbali.

Wakati kanuni hizi zinatungwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018, wadau wengi ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walizipinga mahakamani wakidai kwamba zinakandamiza uhuru wa kujieleza hasa kwa kuwanyima watu haki zao za msingi za kutumia mtandao kutafuta na kusambaza habari.
1596460732560.png

Source: Serengeti Post
 
Wasanii wanaopiga kelele namuona nick mbishi tu,wengine wapo kuimba jua literemke
 
Duh. Mambo magumu haya.
 
Swali langu ni moja. Ivi kama mtu anaweka maudhui tu ya elimu ya science kwa mfano udaktari kwenye page ya Instagram, yeye hii page haimuingizii ata shillingi moja, anatakiwa kulipia hizo leseni? Na kama analipa, inakuaje mtu analipa leseni na wakati hii kitu haikuingizii faida yoyote ya kifedha?
 
Uchaguzi ufike haraka ili tuwafurushe hawa CCM madarakani na hizi sheria zao za hovyo hovyo, jamani tukajitokeze kwa wingi hapo Oktoba ili KUMSTAAFISHA JIWE.
 
Swali langu ni moja. Ivi kama mtu anaweka maudhui tu ya elimu ya science kwa mfano udaktari kwenye page ya Instagram, yeye hii page haimuingizii ata shillingi moja, anatakiwa kulipia hizo leseni? Na kama analipa, inakuaje mtu analipa leseni na wakati hii kitu haikuingizii faida yoyote ya kifedha?
Ikifika Oktoba 28 nenda kapige kura kuwakataa hawa WAHUNI CCM, na mahovyo hovyo yao yote.
 
Mmmh, hakika mbele giza nyuma ni mbali nilikotoka nashindwa kufanya maamuzi ila tutafika japo kwa taabu na mashaka..!
 
Back
Top Bottom