UKAWA waungwa mkono mgombea mmoja

UKAWA waungwa mkono mgombea mmoja

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
Ukawa.jpg

Baada ya vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kukubaliana kumsimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu mwakani, baadhi ya wasomi na viongozi wa asasi za kiraia wameunga mkono hatua hiyo.

Aliyekuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu, alisema lengo la kuundwa kwa Ukawa lilikuwa ni kuunganisha nguvu kusaidia mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ambayo alidai kupinduliwa.

Prof. Baregu, alisema maazimio ya Ukawa yatasaidia kuunganisa makundi mengine yaliyokuwa ndani ya Bunge Maalumu la Katiba ambayo yalikuwa na nia moja na umoja huo, hivyo kutia nguvu baadaye.

"Lengo ni zuri, wanahitaji kujipanga upya. Ni uamuzi ambao utaimarisha vyama vya siasa hapo baadaye. Itasaidia katika vuguvugu hilo la katiba mpya kwa kuunganisha asasi za kiraia na wale ambao hawakuridhika na mchakato wa katiba mpya. Itasaidia kuwaunganisha Ukawa na Watanzania kwa ujumla," alisema.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba, alisema: "Mimi ninaafiki, wanaweza wakaleta ushindi mkubwa sana, kwani ninavyoamini umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Kwa mujibu wa Kibamba, Ukawa wakifanikisha kutekeleza malengo hayo, wapigakura katika chaguzi zijazo watakuwa na hamasa kubwa na kutafanya vyama vingine vya siasa ambavyo havikuungana na Ukawa kuweza kufutika kwa kutolea mfano kwa Marekani.

Rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tangayika (TLS), Francis Stolla, aliunga mkono hoja hiyo, kwa kusema: "Sasa hakutakuwa na kugawana kura. Wakitekeleza kweli, litaweza kuleta mafanikio makubwa kwa chaguzi zijazo."

CHANZO:
NIPASHE
 
Ali-Nassoro--October20-2014.jpg

[h=2]Ali Nassoro Moyo: Katiba imevurugwa na wanasiasa[/h]Mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano, Hassan Nassoro Moyo, amesema kuwa mchakato wa kutafuta katiba mpya umeingia dosari kutokana na kukutanishwa kundi kubwa la wanansiasa.

Akizungumza na NIPASHE nyumbani kwake Fuoni visiwani hapa, alisema hakukuwa na haja ya kuwakutanisha kundi la wanasiasa kwani kila mmoja atatetea maslahi ya chama chake badala ya kutetea maslahi ya wananchi.

Alisema rais wa Jamuhuri ya Muungano ndiye aliyeharibu mchakato huo kwani wanasiasa hao baada ya kukutana katika Bunge Maalum la Katiba, waliweka mbele maslahi ya vyama vyao.

Alisema suala la Wazanzibari kudai mamlaka kamili halikuanza leobalimadai hayo yalianza tangu uhai wa Mzee Abeid Amani Karume, lakini Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alimwambia Karume asubiri wakati utakapowadia madai yao yatafanyiwa kazi.

"Wakati sasa umefika wa Wazanzibari kupata mamlaka kamili na katiba iliyopendekezwa na Bunge la Katiba haijazingatia maoni ya Wazanzibari," alisema Moyo.

Alisema zipo kila sababu kwa wananchi kuikataa katiba iliyopendekezwa kwa sababu mambo muhimu wanayoyadai Wazanzibari hayajazingatiwa.

Aliyataja mambo ambayo waliyadai Wazanzibari na yamepuuzwa kuwa ni polisi, uhamiaji, sarafu, mambo ya nje na ulinzi.

Alieleza kusikitishwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoshirikishwa waasisi wa Muungano ambao wakati muungano unaasisiwa walikuwa mawaziri serikalini na kwamba wangeweza kutumia uzoefu wao kushauri vizuri kwa maslahi ya wananchi wa pande zote za Muungano.

Aliwataja alijitaja yeye, Ramadhani Haji Faki, Ibrahim Amani, Balozi Job Lusinde na George Kahama ambao hadi leo wako hai.

Alisema japo kuwa wameshastaafu, lakini bado akili na maarifa wanayo na wanafahamu mambo mengi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo wangesaidia kutoa mchango mkubwa na wenye maslahi kama wangeingizwa katika tume hiyo.

Alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameihodhi katiba na kuifanya kama yao kwani kuna mambo ambayo Wazanzibari na Watanzania hawayataki, lakini wameyarejesha likiwamo la muundo wa serikali tatu na kuweka mfumo wa serikali mbili.

Alisema watawashawishi Wazanzibari kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa na kwamba na kamwe CCM hawawezi kuipitisha katiba hiyo bila ridhaa za wananchi.

CHANZO: NIPASHE

Ni political frustration.
Wengi baada ya kuona kuwa kila wakigombea uraisi wanaona wanashindwa sasa wanataka kwenda kugombea ubunge.Hiyo ni gia ya kutoroka kugombea uraisi waende kugombea ubunge.Wameona kuwaambia wananchi kuwa ugombea uraisi umetushinda wameona aibu.Wakaona wasingizie hilo.Anyway karibuni majimboni.Nyerere aliwaambia vyama vya upinzani bado havijafikia kugombea uraisi mkambishia.Haya leo yako wapi wenyewe mnakimbilia majimboni kugombea ubunge.Uraisi sio lelemama.

Ni kawaida kwa makabila mengi mtu mzima akienda kujisaidia porini huaga kuwa anaenda kuangalia mitego ya wanyama aliyotega.
 
Asante mzee moyo. Tunawaomba ukawa watangaze mkutano wa tarehe 26 uwanja gani watu wanahamu kubwa
 
Ukawa itatufikisha tunakokwenda tunaomba watangaze mahali pa mkutano wa j2 ili tujiandae mpaka barabara zote zifurike,tunataka kuwaonyesha watawala kwamba raia tumewachoka na hatuwahitaji tena
 
Ni political frustration.
Wengi baada ya kuona kuwa kila wakigombea uraisi wanaona wanashindwa sasa wanataka kwenda kugombea ubunge.Hiyo ni gia ya kutoroka kugombea uraisi waende kugombea ubunge.Wameona kuwaambia wananchi kuwa ugombea uraisi umetushinda wameona aibu.Wakaona wasingizie hilo.Anyway karibuni majimboni.Nyerere aliwaambia vyama vya upinzani bado havijafikia kugombea uraisi mkambishia.Haya leo yako wapi wenyewe mnakimbilia majimboni kugombea ubunge.Uraisi sio lelemama.

Ni kawaida kwa makabila mengi mtu mzima akienda kujisaidia porini huaga kuwa anaenda kuangalia mitego ya wanyama aliyotega.
What is your point, exactly? There is only one position of president and not everyone can be president.
 
Swali ni je, ni nani atakuwa mgombea Urais na atatoka chama gani?
 
Hapo ndio kazi ipo.Je awe mkristo au muislamu? Awe Bakwata au Answar Sunna? Awe chama gani? Na gharama zake za kampeni alipe nani au chama gani? Ikifika kuwa labda kila chama kichangie gharama zake za kampeni basio hapo lazima UKAWA usambaratike sababu kila chama kitataka kiwe mweka hazina wa hizo hela za kampeni ili zifisadiwe.Na wakisema kila chama kitoe na kitunze kuna vingine ukiitisha mchango hata wa msiba haviko tayari kutoa hata shilingi mia!
Anyway ni rahisi kusema kuliko kutenda.Hili la mgombea mmoja UKAWA lazima liwasambaratishe likifika kwenye utekelezaji.MARK MY WORDS AND WRITE IN YOUR DIARY.

Waangalie hata nyuso zao tu kwenye picha zinaonyesha urafiki wa mashaka.
 
CCM imeumia maalim seif jana alisema ccm wakitaka 2, 3 au 1 mwaka 2015 ni CUF inachukua Serikali Zanzibar na Dr Sheikh kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar.
 
Ukawa msimamisheni jaji warioba kuwa mgombea wa urais kwa ticket ya ukawa kwani yeye ni muadilifu
 
Ni political frustration.
Wengi baada ya kuona kuwa kila wakigombea uraisi wanaona wanashindwa sasa wanataka kwenda kugombea ubunge.Hiyo ni gia ya kutoroka kugombea uraisi waende kugombea ubunge.Wameona kuwaambia wananchi kuwa ugombea uraisi umetushinda wameona aibu.Wakaona wasingizie hilo.Anyway karibuni majimboni.Nyerere aliwaambia vyama vya upinzani bado havijafikia kugombea uraisi mkambishia.Haya leo yako wapi wenyewe mnakimbilia majimboni kugombea ubunge.Uraisi sio lelemama.

Ni kawaida kwa makabila mengi mtu mzima akienda kujisaidia porini huaga kuwa anaenda kuangalia mitego ya wanyama aliyotega.

muulize aliyesema 'Vyama vya msimu' kama hajajuutia kauli yake
 
Hapo ndio kazi ipo.Je awe mkristo au muislamu? Awe Bakwata au Answar Sunna? Awe chama gani? Na gharama zake za kampeni alipe nani au chama gani? Ikifika kuwa labda kila chama kichangie gharama zake za kampeni basio hapo lazima UKAWA usambaratike sababu kila chama kitataka kiwe mweka hazina wa hizo hela za kampeni ili zifisadiwe.Na wakisema kila chama kitoe na kitunze kuna vingine ukiitisha mchango hata wa msiba haviko tayari kutoa hata shilingi mia!
Anyway ni rahisi kusema kuliko kutenda.Hili la mgombea mmoja UKAWA lazima liwasambaratishe likifika kwenye utekelezaji.MARK MY WORDS AND WRITE IN YOUR DIARY.

Waangalie hata nyuso zao tu kwenye picha zinaonyesha urafiki wa mashaka.

Mheshimiwa nadhani wewe ni mgeni wa siasa ya tanzania kwani hicho ndicho kilio cha wananchi kwa muda mrefu
Sasa kinacho takiwa ni kupanga utaratibu wa kisayansi na wa kijamii ili kuweza kutimiza mawazo hayo ya kuungana
CCM wamezoea kusema huyu mkabila, yule mdini sasa hao wote wako pamoja.

Mimi niwape moyo wanaoamini mabadiliko sasa yanakuja
Kuhusu posho ni jambo rahisi kugawana kwani pale pana mchumi wa kimataifa Prof. Lipumba, wanasheria waliobobea mikataba mfano Tundu lisu, Prof. Safari, Mr Mtatilo, John Mnyika Busara washauri wakuu wa vyama zitawafiksha pazuri
 
Alisema suala la Wazanzibari kudai mamlaka kamili halikuanza leobalimadai hayo yalianza tangu uhai wa Mzee Abeid Amani Karume, lakini Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alimwambia Karume asubiri wakati utakapowadia madai yao yatafanyiwa kazi.

"Wakati sasa umefika wa Wazanzibari kupata mamlaka kamili na katiba iliyopendekezwa na Bunge la Katiba haijazingatia maoni ya Wazanzibari," alisema Moyo.

Alisema zipo kila sababu kwa wananchi kuikataa katiba iliyopendekezwa kwa sababu mambo muhimu wanayoyadai Wazanzibari hayajazingatiwa.
At times you feel ilimradi waongee tu hawa viongozi wazamani. Huyu Nassoro Moyo yupo kwenye rekodi akidai yeye has got nothing to lose anymore hila anasaidia mwamko wa vijana kudai tiafa lao.

Anavyo jichanganya sasa anadai yeye ni Mzanzibari wa kuzaliwa ZnZ wakati akijibu shutuma zidi ya utata wa uraia wake. Hapo hapo anakiri ya kuwa wazazi wake ndio walioamia kutoka bara miaka ya 1930's hivyo wale awakuwa wa ZnZ. Mtu kama huyu anajua maana ya asili ama? jina lake la kinyamwezi na makabila ya kizambia litamsuta milele. Ni kama vile msukumo wake mkubwa ni kutaka akubalike kama yeye ni Mzanzibari halali mbele ya watu kama akina Jussa. Watu ambao wakishindwa uchaguzi kwenye majimbo yenye raia wengi kama akina Nassoro Moyo kwa mujibu wao ni wabara ndio waliowapa ushindi si wazanzibari.

Hatari kwa siasa na akili za namna hii ndio maana wachina wakaona isiwe tabu waidai hong-kong yao kwanza; wazanzibari inabadi watatue swala la identity crisis hilo ndio tatizo lao si muungano.

As for UKAWA ngoja wengine kwanza tusubiri sera yao ya pamoja hapo ndio tutajua wako serious; chama gani kina wenyeviti watatu na makatibu luluki na viongozi wengine ambao hawaeleweki hiyo maana yake ruzuku kwanza misimamo baadae. Mpaka wawe na safu ya pamoja kwenye uongozi inayoeleweka vinginevyo ni wanasiasaconfuseddot.com.
 
Hapo ndio kazi ipo.Je awe mkristo au muislamu? Awe Bakwata au Answar Sunna? Awe chama gani? Na gharama zake za kampeni alipe nani au chama gani? Ikifika kuwa labda kila chama kichangie gharama zake za kampeni basio hapo lazima UKAWA usambaratike sababu kila chama kitataka kiwe mweka hazina wa hizo hela za kampeni ili zifisadiwe.Na wakisema kila chama kitoe na kitunze kuna vingine ukiitisha mchango hata wa msiba haviko tayari kutoa hata shilingi mia!
Anyway ni rahisi kusema kuliko kutenda.Hili la mgombea mmoja UKAWA lazima liwasambaratishe likifika kwenye utekelezaji.MARK MY WORDS AND WRITE IN YOUR DIARY.

Waangalie hata nyuso zao tu kwenye picha zinaonyesha urafiki wa mashaka.

acha fikra mgando wewe,alafu inaonesha ulipata division six wewe
 
Ni political frustration.
Wengi baada ya kuona kuwa kila wakigombea uraisi wanaona wanashindwa sasa wanataka kwenda kugombea ubunge.Hiyo ni gia ya kutoroka kugombea uraisi waende kugombea ubunge.Wameona kuwaambia wananchi kuwa ugombea uraisi umetushinda wameona aibu.Wakaona wasingizie hilo.Anyway karibuni majimboni.Nyerere aliwaambia vyama vya upinzani bado havijafikia kugombea uraisi mkambishia.Haya leo yako wapi wenyewe mnakimbilia majimboni kugombea ubunge.Uraisi sio lelemama.

Ni kawaida kwa makabila mengi mtu mzima akienda kujisaidia porini huaga kuwa anaenda kuangalia mitego ya wanyama aliyotega.

Kubeba mawazo ya Nyerere kama mazuzu ni uchizi. Kama alijua upinzani hauna uwezo kushinda urais kwa nini alijivua "UBABA WA TAIFA NA KUVAA UCCM ILI AMBEBE MKAPA?"
 
Back
Top Bottom