At times you feel ilimradi waongee tu hawa viongozi wazamani. Huyu Nassoro Moyo yupo kwenye rekodi akidai yeye has got nothing to lose anymore hila anasaidia mwamko wa vijana kudai tiafa lao.
Anavyo jichanganya sasa anadai yeye ni Mzanzibari wa kuzaliwa ZnZ wakati akijibu shutuma zidi ya utata wa uraia wake. Hapo hapo anakiri ya kuwa wazazi wake ndio walioamia kutoka bara miaka ya 1930's hivyo wale awakuwa wa ZnZ. Mtu kama huyu anajua maana ya asili ama? jina lake la kinyamwezi na makabila ya kizambia litamsuta milele. Ni kama vile msukumo wake mkubwa ni kutaka akubalike kama yeye ni Mzanzibari halali mbele ya watu kama akina Jussa. Watu ambao wakishindwa uchaguzi kwenye majimbo yenye raia wengi kama akina Nassoro Moyo kwa mujibu wao ni wabara ndio waliowapa ushindi si wazanzibari.
Hatari kwa siasa na akili za namna hii ndio maana wachina wakaona isiwe tabu waidai hong-kong yao kwanza; wazanzibari inabadi watatue swala la identity crisis hilo ndio tatizo lao si muungano.
As for UKAWA ngoja wengine kwanza tusubiri sera yao ya pamoja hapo ndio tutajua wako serious; chama gani kina wenyeviti watatu na makatibu luluki na viongozi wengine ambao hawaeleweki hiyo maana yake ruzuku kwanza misimamo baadae. Mpaka wawe na safu ya pamoja kwenye uongozi inayoeleweka vinginevyo ni wanasiasaconfuseddot.com.