UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

UKAWA Wapigwa Bao la Kisigino

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,410
Wadau, amani iwe kwenu.

Mtakumbuka kuwa tarehe 17 Aprili 2014, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wanaojiita kwa jina la UKAWA, walitoka Bungeni Mjini Dodoma wakati wa mjadala wa Rasimu ya Katiba katika sura ya Kwanza na ya Sita kwa madai kuwa wamechoshwa na CCM kutumia uwingi wao kushinikiza muundo wa serikali mbili na kuhamasisha makundi ya kijamii wakiwemo waumini kususia muundo wa muungano wa serikali tatu. Wakati wanatoka, walisema kuwa wanaenda kuishtaki CCM kwa wananchi.

Wadau, wakati UKAWA wanapanga kwenda kuishtaki CCM kwa wananchi, CCM tayari ipo kwa wananchi ikiwaeleza bayana wananchi sababu za chama kupendekeza muundo wa muungano wa serikali mbili huku ikipinga kwa nguvu muungano wa serikali tatu. Tumemuona Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akifanya ziara za kichama huko Kigoma na mikoa ya kanda ya Ziwa. Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeratibu na kuendesha matembezi ya bodaboda katika mikoa kadhaa nchini na ujumbe katika matembezi hayo ni kuuenzi muungano ulioasisiwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika ziara zote hizo, wananchi wameonekana kuelewa na kuwashangaa wale wanaotaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu.

Wadau, UKAWA walipoondoka Bungeni, walitarajia kuwa, Bunge hilo litavunjwa kutokana na wao kutokuwepo. Matarajio yao ni kuwa, Bunge likiahirishwa, azma yao ya kukwamisha mchakato huo yatakuwa yametimia. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Wabunge waliobaki wengi wao wakiwa ni wa CCM wanaendelea na mjadala na kwa takriban wiki mbili sasa, CCM wamepata muda wa kutosha wa kusema yale yaliyo dhihiri huku wananchi wengi wakisikiliza kupitia Runinga, Radio na kusoma kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao huu pendwa wa JF. Hakika wabunge wengi waliopata nafasi ya kuongea wamemwaga nondo za uhakika zilizowashawishi wananchi huku wakiendeleza vijembe vile vile vilivyowakimbiza UKAWA. Nina hakika kuwa wanavipata vijembe hivyo huko huko waliko. Hakika kwa hili, UKAWA wamepigwa bao la kisigino na wananchi wanaendelea kuwalaani katika kona zote za nchi.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, zilisikika taarifa kuwa wamechukua posho zote na kujongomea. Hakika kashfa hii imewachafua sana na hawatakuja kusafishika katu. Watanzania wana hasira nao sana na hakika wasitarajie kuungwa mkono na wananchi wengi. Ingawa jitihada zimefanyika za kuwasafisha na kashfa hiyo kupitia Gazeti la Mwananchi, ukweli ni kwamba wananchi wengi wameamini kuwa wabunge hao wamechukua posho na kutokomea. Hilo ni doa kuu ambalo haliwezi kuondolewa kwa Omo wala Aerial.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataanzisha maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia siku ya pili baada ya kuondoka kwao. Hata hivyo, walipigwa stop hadi tarehe 30 Aprili ndipo watakapoanza kufanya mikutano ya hadhara na si maandamano tena. Tunajua kuwa wakati huo Bunge Maalum litakuwa limesitishwa na wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi watakuwa wanajiandaa na vikao vya Bunge la Bajeti. Hawa UKAWA wataendelea vipi kuwa na mshikamano ilhali wabunge watakuwa busy na bunge la bajeti? Hakika hili ni bao jingine la kisigino. Kwa sasa wamekalishwa chini kama bondia aliyepigwa na mpinzani wake huku akihema asijue la kufanya. Wakati wao wataanza mikutano ya katiba, wananchi watakuwa wameshahamishia mawazo yao kwenye Bunge la Bajeti huku wakisubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali itafanya juu yao. Hakika kati ya bajeti na Katiba, ni wazi kuwa suala la bajeti ndilo hugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na hivyo ni vigumu kwa UKAWA kupata watu wa kuwaunga mkono.

Wadau, wakati UKAWA wanaondoka, walitarajia kuwa wataungwa Mkono na wabunge wengi wa kundi la 201. Hata hivyo siku moja tu baada ya kuondoka kwao, baadhi ya wabunge ambao waliondoka pamoja nao akiwemo Mwalimu Ezekiel Oluoch, walirejea Bungeni huku wakiwakana na kuwananga UKAWA. Hakika hili ni pigo jingine. Imekuwa ni fedheha kwao na sasa wamekuwa mabubu kwa vile hawana avenue ya kusemea.

Wadau, baada tu ya UKAWA kuondoka, kuna shirika moja limejifanya kuendesha utafiti ili kujua mtizamo wa wananchi juu ya mijadala bungeni. Eti katika utafiti huo, kwamba Wazanzibari wengi wanaunga mkono muundo wa serikali tatu kama ilivyo kwa bara. Mbaya zaidi, wakamuita mzee Warioba ili atetee hoja hiyo. Hakika hii ni fedheha kubwa na imedhihirisha ni kwa namna gani UKAWA wametepeta. Badala ya kumuacha mzee wa watu augulie madongo anayopewa bungeni, wao wanazidi kumdhalilisha. Mbaya zaidi, Warioba akajifanya kukemea lugha zinazotolewa bungeni asi if yeye ni Presidaa.

Wadau, Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa Nchi anatarajia kuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Mei Mosi yaani siku moja tu baada ya UKAWA kuanza mikutano yao. Ingawa suala la katiba si moja ya ajenda ya sherehe hizo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Rais anatumia japo muda kidogo kuelezea juu ya mchakato huo. Hakika nitamshangaa sana kama hatagusia hilo. Katika hotuma hiyo, ni wazi kuwa Rais Kikwete atasimamia msimamo wake ule ule alioutoa Bungeni tarehe 21 Machi 2014 wakati akilizindua bunge maalum. Hotuba hiyo ya JK itazidi kuwatokomeza kabisa UKAWA na kwa vile wananchi wengi watasikiliza hotuba hiyo, ni wazi kuwa hata UKAWA watazunguka nchi nzima, hawatabadili fikra za wananchi. Hili ni pigo jingine kwa UKAWA.

Wadau, yapo mengi ila kwa hayo niliyoyasema, ni wazi kuwa UKAWA wamelikoroga na lazima walinywe. Hakika wamepigwa bao la kisigino huku wakibaki hawana cha kufanya.
 
Mpango wa ukawa na matokeo yake yamechemka kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mpango na mategemeo yao yalikuwa wakitoka kuwa bunge litasimama.lakini bkt linaendelea. Kufanya mkutano haraka ili uwe na moto moto lakini umebuma.serikali imepiga chini hadi tarehe 30 muda ambao jambo lenyewe litakuwa limepoa na watu watakuwa hawana habari nao.waliwaza watabembelezwa kama siku zote watoto deko. Wajumbe wa ukawa wameanza lalamika kuwa mbowe anawapelekapeleka na kusababisha wakose pesa ambazo zilikuwa zinawasaidia.ukweli mpango wa ukawa unapiga debe tupu maji kwenye kinu.

Ukiwa MZALENDO huwezi kufurahia kilichotokea.Kususia mchakato huu si jambo jema kwa jamii yetu,na ukumbuke waliobungeni hawawezi kufanya chochote kwenye rasimu hiyo hata kupiga kura hawawezi.Ni vyema ukalijua hilo.
 
Katiba ya Zanzibar: Rais wa Zanzibar ndiye mkuu wa nchi ya Zanzibar na amiri jeshi mkuu wa vikosi maalum vya Zanzibar...Interahamwe upo hapo.? Kwa maana hiyo basi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni jina mbadala la Tanganyika maana kimsingi muungano hakuna labda wakuchanganya udongo!!
 
Mpango wa ukawa na matokeo yake yamechemka kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mpango na mategemeo yao yalikuwa wakitoka kuwa bunge litasimama.lakini bkt linaendelea. Kufanya mkutano haraka ili uwe na moto moto lakini umebuma.serikali imepiga chini hadi tarehe 30 muda ambao jambo lenyewe litakuwa limepoa na watu watakuwa hawana habari nao.waliwaza watabembelezwa kama siku zote watoto deko. Wajumbe wa ukawa wameanza lalamika kuwa mbowe anawapelekapeleka na kusababisha wakose pesa ambazo zilikuwa zinawasaidia.ukweli mpango wa ukawa unapiga debe tupu maji kwenye kinu.

Nyinyi viumbe ni wa kuwahurumia tu,Mnahitaji kupelekwa kwenye makambi maalum kwaajili ya re-education programs maana uandishi wako unakuonyesha kuwa hujui kipi ni sahihi unachokipigania na kipi si sahihi unachokipinga.
 
Katiba ya Zanzibar: Rais wa Zanzibar ndiye mkuu wa nchi ya Zanzibar na amiri jeshi mkuu wa vikosi maalum vya Zanzibar...Interahamwe upo hapo.? Kwa maana hiyo basi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni jina mbadala la Tanganyika maana kimsingi muungano hakuna labda wakuchanganya udongo!!
UN wanasemaje? je wanasema kama unavyofikiria wewe?

bunge linaendelea kufanya nn?sema baada ya ukawa kuondoka bunge limeamua jambo gani?sio kuropokwa tu.
 
UN wanasemaje? je wanasema kama unavyofikiria wewe?

Mpaka mwaka 2016 Zanzibar itakuwa imeshajitangazia uhuru wake kamili ilioanza kuupata kwa nguvu mwaka 2009!
 
Mpango wa ukawa na matokeo yake yamechemka kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mpango na mategemeo yao yalikuwa wakitoka kuwa bunge litasimama.lakini bkt linaendelea. Kufanya mkutano haraka ili uwe na moto moto lakini umebuma.serikali imepiga chini hadi tarehe 30 muda ambao jambo lenyewe litakuwa limepoa na watu watakuwa hawana habari nao.waliwaza watabembelezwa kama siku zote watoto deko. Wajumbe wa ukawa wameanza lalamika kuwa mbowe anawapelekapeleka na kusababisha wakose pesa ambazo zilikuwa zinawasaidia.ukweli mpango wa ukawa unapiga debe tupu maji kwenye kinu.

Huna lolote wewe ni kibaraka wa ccm naona umetumwa ili usikie tutasemaje, waambia baba zako ccm tunawasubiri kwenye kura za wananchi mtaani!! wewe na ccm yako mnawaza matumbo yenu sio haki na masirahi ya wananchi!!
 
Zanzibar itakua kamili tu jana mtoto wa mwinyi nae alichangia kuwa zanzibar ipewe sovereign na muungano eti uendelee ccm walishangilia yani wanatuona wa bara tupo poa hatuna kelele
 
bunge linaendelea kufanya nn?sema baada ya ukawa kuondoka bunge limeamua jambo gani?sio kuropokwa tu.
nimekuambia toka jana,haya mambo yanafuata ratiba,kesho ndo ilitakiwa kura ipigwe.swali ni je,kura itapigwa kesho ama la?
 
Mjengoni hamna ki2 pale nimipasho tu..cjui wanafanya nn kule
 
Unafikiri wangeacha kuendelea na vikao? Halafu 300000 wangezipata wapi? Ukawa kama wataweka maslahi ya posho mbele kama walivyoweka mainterahamwe watakuwa wamefeli! Kama kuna wajumbe wa bunge la katiba kutoka Ukawa wanatamani walipwe 300000 nao watakuwa ni mafisadi walewale! Ukombozi ni kujitoa mhanga!
 
Mpango wa ukawa na matokeo yake yamechemka kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mpango na mategemeo yao yalikuwa wakitoka kuwa bunge litasimama.lakini bkt linaendelea. Kufanya mkutano haraka ili uwe na moto moto lakini umebuma.serikali imepiga chini hadi tarehe 30 muda ambao jambo lenyewe litakuwa limepoa na watu watakuwa hawana habari nao.waliwaza watabembelezwa kama siku zote watoto deko. Wajumbe wa ukawa wameanza lalamika kuwa mbowe anawapelekapeleka na kusababisha wakose pesa ambazo zilikuwa zinawasaidia.ukweli mpango wa ukawa unapiga debe tupu maji kwenye kinu.

Hao wanaoendelea wanakalia posho tu. Watajadiliana sana lakini HAKUNA kitu chochote watapitisha na hilo UKAWA wanalijua. Hatimaye ili kitu chochote kipite inatakiwa theluthi mbili ya Tanganyika na theluthi mbili ya Zanzibar. Bila UKAWA na hasa watu wa CUF toka Zanzibar, hakuna thelufi mbili ya Zanzibar!
 
ujue thelusi mbili inapelea kwa hesabu ndogo sana,na hapo hujaweka wale 201,na bahati mbaya wenje akawambia wamehongwa wali na soda,unadhani wataelemea wapi?.pia kuna wapinzani wamebaki mle mjengoni kama mrema,hamad etc.

Lolote laweza kutokea hiyo kesho.
 
Back
Top Bottom