Ni baada ya kutoka bunge la katiba kwa mbwembwe na kiburi kama timu ya mpira iliyofuzu mashindano huku wakijua na kuamini Watanzania wa sasa ni wale wa mwaka wa 47, wakaamini lengo lao la kutoka litashangiliwa na kila mtu.
Baada ya kujidhihirishia kosa lao la kukimbia majadiliano, na kukosa support ya walio wengi kuendelea kugoma kurudi bungeni, Sasa wanatamani Sana kurudi ila wanahofia kuzomewa na wabunge na wajumbe ambao hawakutoka, wala hakuna sababu nyingine.
Rai yangu kwa mh. Sitta, awahakikishie kutokuzomewa pindi watakaporudi.
Unajua BMK wamekula mabilion ya pesa wasituchezee kabisa! Bado kuna ishu nimesikia harufu kwa mbaaali ya PPRA ya ununuzi wa BVR kwa $117, zaidi ya Tsh.295 bilion!
Kuna hoja nyingine ni za kijinga sana, kiasi kwamba hata kuzijadili ni kichefuchefu.
Wewe ukizitathmini tamaa zako, na kuzipa nafasi zikutawale, wenzako wanajua namna ya kuziepuka tamaa za kijinga na zinazodhalilisha utu wa mwanadamu,
Hitaji la UKAWA ni hitaji na wananchi kwa muda mrefu, sio hitaji la CCM, CCM hawana mpango na katiba mpya, na tafsiri ya katiba mpya ni kutunga katiba kutokana na maoni ya wananchi, ambapo tangu kuumbwa kwa huu Ulimwengu, Taifa letu halijawahi kupata fursa hiyo
CCM waliunda tume kadhaa za kukusanya maoni, majibu yalikuja, serikali 3! Na kwenye tume zote zilizoundwa ziliongozwa na makada wa CCM, hii ya Warioba ilichanganya wajumbe, ila zilizopita zote ni za wana CCM!
kila hatua, ya tume, Mwenyekiti wa CCM alikuwa anajulishwa
Leo mnataka maoni ya wananchi muyanajisi? Leo mnataka kutueleza tume ya warioba haikutenda kazi ipasavyo? Leo mnataka kutuambia mabilioni ya tume ya warioba yalipotea bure?
Leo mnaringishia eti mnapandisha posho hadi laki saba, ili kuwatamanisha wajumbe wa ukawa, mnadhani wao wanatamaa kama ninyi?
Leo mnataka mbadili kanuni ili mpitishe rasimu yenu ya 'Serikali mbili Zilizoboreshwa' kwa wingi wenu kama mnavyopitisha bajeti zenu feki zenye madosari dosari?
Fanyeni kila mnaloliona linawapendeza machoni penu, ila ipo siku, Wananchi wa Tanganyika na Wazanzibari watapata hitaji lao.
Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibar