UKAWA wakiingia madarakani, wataanza na haya

Ndugu watanzania, UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKWA tukiingia ikulu ndani ya mwezi mmoja tutaanza na haya:-

1. Kufukuza vigogo ambao ni vibaraka wa CCM
2. Kupiga mnada mtambo wa kuangalia mawasiliano ya watu.
3. Kupiga mnada ndege ya Rais
4. Kukamata watuhumiwa wote wa wizi wote kuanzia wale EPA NA ESCROW yaani Manji, Rostam, Mramba, Yona, Lowasa, Mkape, anna, Yona, Ngereji, Tibai, na wengine.
5. Kurudisha nyumba zilizogawiwa bure

6.Kubadilisha Mabalozi wote wa Tanzania Nchi za Nje.. kama sio wote basi, wabadilishe angalau aadhi ya Mabalozi waliobebwa na Kikwete: Mfano, Balozi Jame Msekela wa Roma. Huyu anabadhilisha mali za wananchi wa Tanzania utadhani kama yeye siyo ni raia wa Tanzania?
 
Hiyo ni mipango yetu ya muda mrefu, hiyo niliyotaja ni short plan.

Ingekuwa mimi ni Rais kupitia UKAWA,wala sihangaiki na hao mafisadi.Nataifisha mali zao za ndani na nje na kuwaacha wawe raia wema,washiriki kuleta maendeleo kwa njia halali.
Ningefocus kwenye kufufua viwanda,kurejesha njia za reli na kuangalia huduma za jamii.Mambo ya kuanza kufukuzana na maccm yatapoteza muda wa kuwatumikia wananchi.
 
Kwenye strategic management kuna long term plan na short term, hizo tulizozitaja ni short term yaani ndani ya mwezi mmoja, long term ni process ndefu ambayo lazima kushirkisha wadau mbali mbali, mfano tutaunda commission ya wataalamu wa uchumi kuishauri serikali jinsi ya kuinua uchumi, pia commission hii itakuwa ina monitor Benku yetu. commision hii ya wataalamu wa uchumi haitakuwa ya kisiasa itahusisha wataalamu wote bila kuangalia vyama vyao, itashauri na kusimamia wizara ya uchumi na fedha. commission hii itasimamia kutengeneza long strategic plan za uchumi na itakuwa na kufanya evaluation kila baada ya mwaka mmoja kuangalia mile stone/perfomance ya plan. hapa ndiyo kutakuwa na mikakati ya kufufua uchumi, km kufufua shirika la reli, viwanda, umeme, maji, shirika la ndege na kadharika.

Kweli chadema ni maboya..unasema utakuja na mikakati baada ya kuingia ikulu? Nilitegemea mpaka sasa mtakuwa na plan ambayo ndo itawasaidia kujinadi mpate kura za kuwaingiza ikulu? Chadema haina sera?? Hatari sana aizeee
 
Back
Top Bottom